Kuna Maudhui Mengine kwenye Social Media yanapaswa kuzuiwa Tanzania

Ni kweli, hakukuwa na ulazima wa kuweka hiyo video. Naweza kuifuta ila mada ikabaki inaongelea kitu kilekile
Wewe umetaka kuonesha chuki yako kwa mashoga tu tangu mwanzo. Ndiyo maana ukaweka hiyo video.

Na hiyo video haina explicit content kihivyo, na hata kama hutaki kwa wanao kuna njia za kuwakataza wao wasiangalie, wanaotaka waangakie, wengine wakacheka kwa kuona huu ujinga wa kawaida wa mitandaoni tu. Hususan kwa sababu hujatupa hata standard ya what is explicit and what is allowed.

Kwa hiyo kama hizi ndizo aina za video zinazokutatiza inaonekana wewe una obsession na censorship tu.
 
Tumehoji kwanini kaileta kutokana na maelezo yake kwamba haifai kuwepo kwenye mitandao ya kijamii, haina maadili na bla bla kibao.
Kwa kuileta hapa hana tofauti na walioipost huko maana kama kweli ina maudhui ya kingono kama alovyosema why ailete huku? Kuna watoto wetu humu unadhani wakiona itakuaje?
 
Kwanini ufatilie vitu usivyovipenda? Mbona kwenye hii mitandao kuna vitu ambavyo waweza kuchagua kuvifatilia na usivovipenda unaweza kudhani havipo?

Chagua kile unachoona kinafaa, maana kuna vingine ambavyo hujui kama vipo na nivyakuogofya.
Mkuu hoja yako inaonekana rahisi sana lakini kiuhalisia inaacha pengo kubwa.

Suala hapa sio tu “kufuatilia au kutofuatilia content”, bali ni nani ana-access hiyo content.

Wewe kama mtu mzima unaweza kuchagua unachoangalia, lakini mtoto hana uwezo huo huo wa kufanya filtering sahihi. Algorithm za social media hazichagui umri kwa usahihi, content inaweza kumfikia mtoto bila yeye kuitafuta.

Kwa hiyo kusema “usiifuatilie” ni rahisi kwa mtu mzima, lakini kwa watoto sio realistic.

Ndiyo maana hata duniani kote kuna concept ya age restriction—sio kwa sababu watu wanataka kuingilia uhuru wa wengine, bali kulinda makundi ambayo hayajakomaa kifikra.

Pia hoja ya kuchagua unachopenda inaishia kwa individual responsibility, lakini hapa tunazungumzia public platforms ambazo zinatumika na kila mtu, wakiwemo watoto.

Kwa kifupi:
Sio kila kitu kinaweza kuachwa kwenye “ignore usichopenda”, kuna vitu vinahitaji mipaka (boundaries), hasa vinapohusisha maudhui ya watu wazima yanayoweza kuwafikia watoto.

Hapa hoja si censorship ya kila kitu, bali ni responsibility ya kuhakikisha content inawafikia watu sahihi kulingana na umri wao.
 
freedom of expression doesn’t mean lack of understanding,Wengi hawapingi kwa sababu hoja ni mbaya, bali kwa sababu hawako tayari kufikiria nje ya walivyozoea
So real wisdom ni kujua: not everything you see is meant to fit where you are.
 
Wewe huna hoja, kwanza ulikuwa unaongelea mada ambayo haipo kabisa. Sasahivi unataka kujificha kwenye comments za wenzako. Hebu kwenda 🚮🚮
Wewe ndiye huna hoja umeanzisha uzi mzima kuitaka serikali kuzuia maudhui social media wakati huna hata standard ya nini cha kuzuia na nini cha kuachiwa, uko dangerously vague.

Kwenye nchi ambayo serikali inafanya censorship willy nilly.

Mawazo ya kishamba kabisa.
 
Pia hata huko nchi za nje huwa wanapinga maudhui hayo kuwafikia watoto
Hawa wanaotetea wana mambo yao binafsi tu ila wanajua sio sahihi
Your browser is not able to display this video.
 
Hivi hawa watoto mnaowazungumzia hapa kwamba wanaweza kuona hayo mambo ni watoto wa umri gani?
 
Ngoja tuliweke sawa hili.
Kwahiyo mkuu jamaa alitakiwa afanyaje ili kufikisha duku duku lake humu jukwaani.
 
Mkuu huyu mbona anaonekana kabisa kuwa ni tayari ni ameshakuwa Kisu cha Mkunjo?
 
Hivi hawa watoto mnaowazungumzia hapa kwamba wanaweza kuona hayo mambo ni watoto wa umri gani?
Sikuhivi all ages zina access na social media. So anyone below 18 yrs hapaswi kuona baadhi ya content
Kama ni sawa kupost hayo maudhui basi at least yasiwe yanapostiwa carelessly, at least yawe restricted to certain accounts, labda za age 18 na kuendelea
 
Hii ni video yenye homosexual content, so ni sexual content and any sexual content is 18+.
Dunia nzima inajua hilo suala
Homosexual content ni nini? Unapimaje hii ni homosexual content?

Sexual content ni nini?
Unapimaje hii ni sexual content?
 
Anyway hao watoto wanaangalia wapi hayo maudhui? i mean wanamiliki simu?
Yeah, simu, iPads nk
Sikuhizi watoto wanamiliki hivyo vifaa, na sikuhizi kwenye social media hadi maudhui ya watu wazima yanawafikia watoto kupitia vifaa vyao
 
Damn you went hard.
 
Wewe mwenyewe mbona umepost hapa JF video ambayo unasema haifai kwa watoto?

Unajua unataka nini wewe?
 
Mzazi kumpa simu mtoto under 15 ni kosa la mzazi mwenyewe. Kama wewe umeshimdwa kumlinda usitegemee dunia ikakusaidia kumlinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…