Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Mtu kuleta homophobic slur ni ushahidi kwamba yeye ni homophobic.Mkuu umeleta mambo mengi kwa pamoja, lakini mengi yako yanaondoka kwenye hoja ya msingi.
Kwanza, kama kuna mtu ametumia lugha ya kuudhi au slur, hilo ni suala tofauti na linaweza kushughulikiwa kivyake. Lakini hilo halibadilishi hoja iliyopo hapa kuhusu maudhui ya watu wazima kufikika kwa watoto.
Pili, umeuliza “adult content ni ipi?” — hili si jambo jipya wala lisiloeleweka. Ndiyo maana kuna mifumo ya age rating duniani (kama 18+, R-rated n.k.) ambayo inaainisha maudhui yenye mambo kama ngono ya wazi, uchi, au ukatili uliopitiliza. Hatuanzi upya kufafanua kitu ambacho tayari kina standard zake kimataifa.
Tatu, hoja ya censorship imechukuliwa nje ya muktadha. Hakuna aliyesema kila kitu kifungiwe bila utaratibu. Kinachozungumziwa hapa ni kuweka mipaka ya nani anaweza kuona nini — hasa kulinda watoto. Hata kwenye platforms zenyewe kuna age restrictions; hilo si jambo jipya wala la kipekee.
Mwisho, kusema mtoa mada “anasambaza adult content” ni hitimisho lisilo na msingi bila ushahidi wa moja kwa moja. Kujadili uwepo wa maudhui fulani si sawa na kuyasambaza.
Tujaribu kurudi kwenye hoja:
Je, ni sawa au si sawa kwa maudhui ya watu wazima kufikika kwa urahisi kwa watoto?
Hapo ndipo mjadala ulipoanzia.
Kwa hivyo naweza ku conclude kwamba mleta mada ni homophobic.
Homophobia ni sehemu ya mada hapa. Huwezi kuitoa, mtoa mada kaanza kuwabagaza mashoga tangu post ya kwanza. Usitake kuifuta hii.
Kwa definition yake mtoa mada ya maudhui ya watu wazima, aliyoyaleta hapa, mtoa mada hana nia ya kuwalinda watoto dhidi ya maudhui ya watu wazima. Ndiyo maana hata yeye kaeneza hayo anayoyaita maudhui ya watu wazima mpaka hapa JF, mtandao ambao hauna age verification, na nilipomuonesha contradiction ya yeye kuleta maudhui hayo hapa huku akijinadi anawalinda watoto wasiyaone, mpaka sasa kakataa kuyaondoa.
Ukichunguza hapo utaona mtoa mada nia yake ni kuwabagaza mashoga, hana nia ya kuwalinda watoto na anachokiita sexual content. Angekuwa na nia ya kuwalinda watoto na anaamini kweli hii ni sexual content, angeitoa.
Kuhusu censorship.
Huwezi kuondoa hoja ya censorship bila ya kuweka standard nini ni adult content na nini si adult content. Bila ya hiyo definition na standard utaipa serikali nguvu ya kufanyia censorship chochote kwa kusema ni adult content. Huna standard, huna definition, utakataa kwa msingi gani kuwa speech ya upinzani ya kisiasa ya kuibana serikali si matusi yenye adult content?
Mtoa mada anasema hii video ni adult content, haifai kuangaliwa na watoto, kisha anaisambaza hapa JF, mtandao ambao hauna age verification.
Huoni kuwa, kama kweli hiyo video ni adult content, na yeye mtoa mada anachangia kuisambaza hiyo adult content kwa watoto pia na angeweza kujadili hoja bila kuisambaza hiyo video?
Huelewi wapi jambo la simple contradiction hili?
Mtoa mada kaambiwa mara kadhaa kuhusu contradiction hii, kagoma kuondoa hiyo video.
Mpaka hapo hujaelewa kuwa mtoa mada hana nia ya kuwalinda watoto na adult content, ana nia ya kuwabagaza mashoga tu?