Kuna mbegu nimenunua eti inasafisha tumbo na kuondoa sumu, bado sijaitumia nataka ushauri kwanza

Muda sahihi wa kuitumia hiyo 'Habbat Mulk' ni muda gani, asubuhi? au hata usiku baada ya kula?

-Kaveli-
The best time ni asbh kisha fanya vikazi vya hapa na pale ili dawa i respond mapema,ingawa itakuendesha kwa masaa not less of 8hrs!!!
 
Hiyo dawa ni hatari kuna wakati nipo dodoma nilikutana na Dawa hiyo inaitwa mnyoo..... niliambiwa inapunguza uzito pamoja na kupunguza mafuta nilipewa mbengu tatu nilianza kutafuna mbegu moja ilianza kuwasha kooni na baada ya dk mbili kabla cjatafuna ya pili tumbo likaanza kusokota na kuanza kuharisha muda huo... kwa mbegu moja ilinichukua siku 2 hadi nilipoenda hospital baada ya kuona kitu hakikati

Ushauri usitumie dawa hizo nenda hospital upate maelekezo ya daktari na nilipowailimulia wenzagu walisema umejitahidi sana wao waliishia kulazwa na kuongezewa dilipu Za maji
 
huyo mtu nilimkuta kwenye nyehunge ya mwanza moro...akawauzia watu hiyo kitu, mm nikisikia mtu anasema nitaharisha nikitumia...ujue siwezi nunua. yaani niharishe wala sitaki hata kusikia aisee!
 
Nadhani itakuwa mbegu ya mnyonyo au castor bean embu tupia picha
 
Ungeweka picha yake tuone kama ni mlonge

Vinginevyo kuna mbegu kwetu wanaita ngenzi ukila ni mawili ufe au upone. Be careful.
 
Yaani hiyo ni habbaatil mulk. Ni dawa nzuri sana kwa kusafisha tumbo, kama una mafuta mwilini inapunguza. Tunakula vyakula vingi sana na tunaingiza sumu nyingi sana mwilini. Kama kweli ingechukua beseni ungeona jinsi ulivyo jaa uchafu mwilini, maana ungeona mauchafu yanayotoka mwilini mwako yaani hutoamini.Ni nzuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nilimeza usiku nimeharisha tu kidogo asubuhi kama mara tatu hivi.
ila wanashauri umeze asubuhi kabla ya chochote .kesho nitameza tena nilinunua za buku zipo kama 20

mmh aisee hujipendi wewe za buku!!!!!!! utaharisha mpaka utumbo.
 
Hizo zitakuwa mbegu za Moringa Oreifela. Ni nzuri sana kwenye kusafisha uchafu kwenye mfumo wa chakula. Natumia sana mimi. Na kwa sasa nina unga wa majani ambao unatumiwa kwenye supu, chai, mboga n.k. Jari afya zenu ndugu
 

Sijui sana, ila nakushauri wakati wa kutumia uwe nyumbani na uwe na mwanagalizi wa karibu ambaye atakumonitor wakati wote uendapo msalani maana waweza arisha ukaishiwa nguvu na husipopata msaada waweza poteza maisha.

Pia uwe na maziwa karibu, ili mambo yakiaribika unyweshwe.
 
Ulichemka sanaa [emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitumia dawa hii hakikisha unakua na machungwa pembeni, utakapohisi umechoka kuharisha kula machungwa itakata hapohapo na utajiskia poa.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…