Kuna mji wenye usafiri mzuri wa daladala na elimu nzuri kuliko Mbeya?

Karibu sana Mbeya, Ahsante kwa kuitambua Mbalizi Sec pia.
 
Ukiweka uwiano wa majiji hapa Tanzania Mbeya ni jiji la hovyo sana hasa katika mpangilio wa nyumba yaani kila sehemu ni slum tu vinyumba vya matope vimesongamana sana. Kwa upande wa vyakula Mbeya ni Super 100% unaenjoy sana ukiwa Mbeya
Katikati ya mji (Mwanjelwa,Soweto,Mabatini,Simike,Nzovwe.......)ndiyo zipo nyumba za aina hiyo na zinaharibu muonekano wa mji kwa kweli.
 
mbeya ni chafu sana mzee, wala usiitaje kabisa. naongea kwa ufahamu mzuri kwasababu mbeya ni mojawapo ya makazi yangu, among others.
 
Mbeya kuna barabara mbaya sijawahi kuona kwanza ni nyembamba sana jiografia yake ni mbaya sana milima mingi yani kwa wale wenzangu na mie wa Daslam wapenda mbio hiku kudanja ni dakika sifuri ukitoka tu barabarani umeingia kwenye miti au korongo biashara imeisha...mfani barabara ya kutoka mbeya kwenda kyela mbaya sana
 
Taka taka. Yaani kibarabara kimoja hicho chenye kusumbua watu, unaona basi wana system nzuri ya public transport?
 
Duu! Kweli mbaya hana sababu yaani mbeya-kyela barabara mbovu?wivu mbaya saaana!
 
Hili ndilo wengi wasilolijua, Mbeya ndiko mmoja wa marais wa makaburu alipata elimu yake, na hapo si pengine ila ni Mbeya European Boarding School, (Mbeya School au Iyunga).
 
mkuu, labda mbeya ya zamani, siku hizi daladala nyingi ni costa kubwa tu
Vi hiace vipo sana hasa mwanjelwa-uyole.
Costa amsha amsha asubuhi wamama wanyaki wakiamka biashara njia nzima toka kyela hadi tunduma zinakula mzigo.
Usiku mwingi hamna movement watu saa tatu kule wanajifungia.
Kuna wazee wa nondo mtaani.
Yaani kule kaa ndani tu baada ya muda huo ukijifanya mzururaji jiandae kwa lolote usiku.
 
Mbeya barabara ni nzuri acha ujinga
Uzuri sijakataa ila hali ya hewa pia!

Nikikwambia utembee Ubungo flyover unikute External sahizi unaweza ukaamua ukodishe boda boda njiani๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚!

Dar hapafai kutembea kwa mguu mzee unaeza kufia njiani!
 
Uzuri sijakataa ila hali ya hewa pia!

Nikikwambia utembee Ubungo flyover unikute External sahizi unaweza ukaamua ukodishe boda boda njiani๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚!

Dar hapafai kutembea kwa mguu mzee unaeza kufia njiani!
Hali ya hewa imefanyaje? Huko kwenu Dar masika shida kiangazi tabu kila sehemu harufu..

Dar ndio hakufai kwa kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ