Kuna muda kumtetea Ommy Dimpoz ni ngumu sana

Hio gari ni customized... kuna garage maalumu wana customize..

Mercedes hawana toleo hilo..
Hio ni G63 ambayo imekuwa customized kwa kuongeza luxury na perfomance...

Ni expensive...

Lakini siwezi kusema ana miliki hilo gari kwa sababu yeye ni shoga...
 
Kwa hiyo ina maana unaona wivu kumtetea mtu mwenye gari hilo hata kama kaonewa?

Unakuwa na kijiba fulani cha roho hivi cha kufurahia na yeye aonje machungu ya dunia kwa kuwa anakutesa sana ukimuona kwenye hilo gari sio?

Hilo si gari tu, tena kimsingi mostly ni liability, with fast depreciation and bad fuel economy, wala si asset, tatizo liko wapi?

Pia, mwaka 2023 hakuna Mercedes Benz Maybach G-Class hiyo ni ya kuchongwa wapi, au wewe ndiye umebumba?

Fafanua vizuri, maana sijakuelewa😂😂😂
 
Wakati mwingine Busara ni kuacha mambo yaende tu, haisaidii kumchunguza sana mtu nini anamiliki.

Kama anamiliki vitu vya thamani kwa sababu ya kujihusisha na vitendo vya Ushoga tu basi watu wengi wangefanya hivyo vitendo. Ili nao wamiliki vitu vya thamani
 
Ukitaka kuishi na wabongo bila kelele, usionyeshe kama unapesa au mafanikio. Kuwa low key, kula bata kimya kimya wasijue, hakuna haja ya kuonyesha lavish lifestyle, jifiche, ficha pesa. Kinyume na hapo wabongo, watakupa kila aina ya kashfa.

Huyu dogo hajajua kuishi na wabongo, wabongo hawataki hizo za kuwaonyesha kama una vitu.
 
Wabongo wengine unaweza kuwapa pressure hata kwa gari la kukodi, hata kwa Maybach la Mchina.

Na mimi nimeangalia nikaona hakuna Maybach G-Wagon ya 2023.

Watu wengi wana status anxiety sana Bongo.

Yani G-Wagon limepata umaarufu kwa sababu ya uzito wake wafanyabiashara wa Marekani wameweza kulinunua na kupata faida kwa kuli claim kwenye tax returns (Internal Revenue Service, TRA yao) kama gari la kazi, halafu anakuja Mndengereko naye anaiga kwa sababu kaliona kwenye music video bila kuelewa kwa nini gari hili ni maarufu, bila kuelewa kuwa wale wenzake Marekani gari linawalipa, TRA yao inawalipa kwa kutumia gari hili kama la kazi kwa sababu limepita uzito fulani, na yeye akilifakamia kwa fuel economy ya 17 miles per galon, bila kuweza kupata tax return kutoka TRA, na sisi tunamuonea wivu anaendesha G-Wagon kwa Status Anxiety.

That is second hand Status Anxiety.

Ni kama mtu ambaye havuti sigara, lakini anapata saratani kwa kukaa karibu na mtu anayevuta sigara yeye anapata moshi tu 😂😂😂
 
Hiyo kanuni haswa wenye nazo hawaijui.. halafu sio Tz tu ni karibia maeneo mengi duniani.... Usione pia wazungu wakija kula Bata huku Afrika au popote wana post post kama show offs... Sho offs zina attract jealous sana
 
Acheni kuwazia mabaya
Nasikia kuna biashara za unga wa Sembe, soya nk huko Sudani ya kusini zinatoa watu
Watu wana wivu kwa sababu ya umasikini wao na roho zao mbaya tu.

Yani wanaona kwa nini huyu aendeshe gari hili wakati mimi hata baiskeli sina?

Sasa hapo ndiyo utapata stories zote za kuungaunga, mara msenge, mara anauza sembe.

Kabla hata ya kujiridhisha ukweli uko wapi.

Yani unaweza kutungiwa stories hizi hata kwa gari la kuazima tu.
 
Daah bongo ukimiliki mali unapewa kesi zote mara kaua ndugu sijui shoga kazi ipo ni uwezo wa kufikiri wa kimasini sana Watannzania wengi tena wenye majina wana mawazo ya karne ya 17 au 18 huko najiuliza hawa Wastwana wametuzidi nini mbona wao hivyo vitu kawaida tu na hakuna anaeshangaa hapa nimesimama sehemu zimepita mashine tena za maana wanaenda kula bata Tlokweng huko bongo nzima tupo tunajadili gari moja ni kiwango cha mwisho cha Umasikini.
 
Hiyo kanuni haswa wenye nazo hawaijui.. halafu sio Tz tu ni karibia maeneo mengi duniani.... Usione pia wazungu wakija kula Bata huku Afrika au popote wana post post kama show offs... Sho offs zina attract jealous sana

Huyo dogo Omari, anachotakiwa kujua ni mindset za wabongo, show off zina attract envy and bad energy. Kibongo bongo ili uwe salama na hela zako lazima ujue namna ya kuzificha,huku unakula bata kimya kimya wasijue wabongo.
Wabongo wanapenda kukuona una struggle, upo nao sawa sawa na una shida hivi. Hapo hutawasikia wakisema wewe unauza poda, firimsaoni au kua upinde.
Kuwa tajiri kwenye kundi la watu masikini sio salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…