Wabongo wengine unaweza kuwapa pressure hata kwa gari la kukodi, hata kwa Maybach la Mchina.
Na mimi nimeangalia nikaona hakuna Maybach G-Wagon ya 2023.
Watu wengi wana status anxiety sana Bongo.
Yani G-Wagon limepata umaarufu kwa sababu ya uzito wake wafanyabiashara wa Marekani wameweza kulinunua na kupata faida kwa kuli claim kwenye tax returns kama gari la kazi, halafu anakuja Mndengereko naye anaiga kwa sababu kaliona kwenye music video bila kuelewa kwa nini gari jili ni maarufu, bila kuelewa kuwa wale wenzake Marekani gari linawalipa, TRA yao inawalipa kwa kutumia gari hili kama la kazi kwa sababu limepita uzito fulani, na yeye akilifakamia kwa fuel economy ya 17 miles per galon, bika kuweza kupata tax return kutoka TRA, na sisi tunamuonea wivu anaendesha G-Wagon kwa Status Anxiety.
That is second hand Status Anxiety.
Ni kama mtu ambaye havuti sigara, lakini anapata saratani kwa kukaa karibu na mtu anayevuta sigara yeye anapata moshi tu 😂😂😂
Kiuhalisia mimi kuamini ukwasi wa msanii kwa kuangalia gari anazomiliki ama mali flani huwa nakosa uhakika... haswa hawa wasanii wa Tanzania.
Kuna utofauti wa kuonekana tajiri(looking rich) na kuwa na utajiri (being wealthy) hawa wasanii wengi wanapenda kuonekana matajiri.
Kwanza ni mabingwa wa kuongeza sifuri mbele..
Si wakweli, unakuta gari kapewa aitumie , ama amekodi anasema yake...
Huyu Ommy alipougua koo aliomba mchango akafanyiwe matibabu.. leo hii anamiliki gari ya bilioni 2 na pointi...?
Kwenye burudani muonekano wa nje ndio unaouza, hata Diamond kumiliki ile rolls royce inasaidia kwenye mikataba yake ya endorsements, brand value inaonekana ipo juu hivyo anaokula nao mikataba na wao wanaongeza malipo...
Sasa na hawa wengine unakuta wana fake wapate deals nzuri nzuri..
Kwanza gari ni depreciating asset, hilo gari baada ya miaka mitatu atauza robo ya pesa alionunulia...
Kama ni lake kweli basi hio ni financial suicide, huwezi kuwa na bilioni 10 bank halafu ununue gari ya bilioni 2.. ni ujinga.. na huyo Omary sidhani kama ana hio bilioni 10 kwa jumla ya mali zake...
G Wagon uendeshaji wake kuanzia matengenezo, bima, mafuta , vipuri ni ghali...
Kama una bilioni 10, ukamiliki gari ya bilioni 2, unakuwa umetumia 20% ya ukwasi wako kwenye liability, halafu ni kitu kinachoshuka thamani ndani ya miaka miwili, hakuna tajiri mjinga hivyo...