Kiuhalisia mimi kuamini ukwasi wa msanii kwa kuangalia gari anazomiliki ama mali flani huwa nakosa uhakika... haswa hawa wasanii wa Tanzania.
Kuna utofauti wa kuonekana tajiri(looking rich) na kuwa na utajiri (being wealthy) hawa wasanii wengi wanapenda kuonekana matajiri.
Kwanza ni mabingwa wa kuongeza sifuri mbele..
Si wakweli, unakuta gari kapewa aitumie , ama amekodi anasema yake...
Huyu Ommy alipougua koo aliomba mchango akafanyiwe matibabu.. leo hii anamiliki gari ya bilioni 2 na pointi...?
Kwenye burudani muonekano wa nje ndio unaouza, hata Diamond kumiliki ile rolls royce inasaidia kwenye mikataba yake ya endorsements, brand value inaonekana ipo juu hivyo anaokula nao mikataba na wao wanaongeza malipo...
Sasa na hawa wengine unakuta wana fake wapate deals nzuri nzuri..
Kwanza gari ni depreciating asset, hilo gari baada ya miaka mitatu atauza robo ya pesa alionunulia...
Kama ni lake kweli basi hio ni financial suicide, huwezi kuwa na bilioni 10 bank halafu ununue gari ya bilioni 2.. ni ujinga.. na huyo Omary sidhani kama ana hio bilioni 10 kwa jumla ya mali zake...
G Wagon uendeshaji wake kuanzia matengenezo, bima, mafuta , vipuri ni ghali...
Kama una bilioni 10, ukamiliki gari ya bilioni 2, unakuwa umetumia 20% ya ukwasi wako kwenye liability, halafu ni kitu kinachoshuka thamani ndani ya miaka miwili, hakuna tajiri mjinga hivyo...
Wakati nakua, when I was about 14-15, nilikuwa na tabia ya kupitia bookshelf ya nyumbani. Kulikuwa na vitabu fulani vya management na business baba yangu alikuwa anapenda kusoma, nikawa navipitia vile rahisi rahisi zaidi.
Kimoja kilinivutia kilikuwa kinaitwa "Swim With The Sharks Without Being Eaten Alive: Outsell, Outmanage, Outmotivate and Outnegotiate Your Competition".
Kitabu hiki cha Mmarekani Harvey Mackay kilinivutia sana kwa sababu kilikuwa kinaenda straight to the point kikielezea mambo makubwa, kwa maneno machache sana, kimantiki sana.
Moja ya somo kubwa nililojifunza mpaka leo nakumbuka, bwana Mackay alifundisha somo kuwa, gari kwa kiasi kikubwa ni liability inayopungua thamani kila muda unavyopita, na nyumba ni asset inayopanda thamani muda unavyopita. Akasema nunua magari yasiyo na thamani kubwa sana, lakini nyumba za thamani kubwa. Sababu yake ilikuwa gari mostly ni liability, linapungua thamani kila muda unavyopita, na nyumba inapanda thamani.
Sasa baada ya kuelewa somo hilo tangu nikiwa na miaka hiyo, nikiona watu wanashobokea magari kama utajiri nashangaa.
Naam, kuna watu wanapenda magari kwa sababu ya performance, legacy, etc. Mimi pia naendesha German cars BMW X5 na Mercedes Benz GLE 450 4Matic. Lakini si kwa showoff wala Status Anxiety. Sioni kuwa gari ni utajiri. Haya yapo kwenye uwezo wangu, napenda the features, pia haya ni magari nayajua yalikuwapo nyumbani tangu nakua, siigi kwa kuona kwenye music video.
Ila wabongo wengi wana ulimbukeni wa kuona gari ni utajiri bado.