Sijajua haswa ni fundi kwa fani gani, lakini kwa vyovyote fundi bila kuongeza thamani unaweza ukabaki kuwa fundi msaidizi wakati wote.
Sote tumepitia kuwa saidia fundi, hio ni kwa sababu huyo fundi nae alikua msaidizi pia ila alijiongeza na kukuza thamani ya ufundi wake na akapata connection kubwa badala ya kufanya kazi mwenyewe akatafuta wasaidizi.
Huko kufanya kazi na fundi ndiko kunakokupa conection, huko kufanya kazi na fundi ndiko kunakupa uzoefu, kunakukutanisha na watu wengi wakiwemo mafundi wengine wenye conection kubwa,
Katika tasnia nzima ya ufundi huwezi kufanya kazi peke yako ni lazima uwe na mjumuiko wa mafundi wengine wengi ili kazi iwe bora, usione shida kufanya kazi za usaidizi kwa sababu ndio mzunguko wa ufundi ilivyo.
Cha kufanya katika kile unachokifanya fanya kama chako, kiongezee thamani, jifunze mbinu mpya za kiufundi.
Nasisitiza kuongeza thamani kwa sababu ukiwa wa thamani hata fundi akikuhitajia kwa kazi yake, kama ulikua wa kumi atakulipa kumi kushuka chini, ila ukiongeza thamani ukawa wa mia basi hata malipo yako yatakuwa ni mia mia hivi.
Ukiisha kupata thamani anza kuweka mikakati ya kuwa na ofisi yako.
Ukiwa na ofisi hali wewe ni fundi utakua unapata kiasi kikubwa sana cha faida .
Ujue kuna watu wana ofisi za kiufundi lakini sio mafundi ila wana mitaji na connection, hao ndio wanaowatuma mafundi na kuwalalia sana, imagine wewe ni fundi, una mtaji una conection! Lazima upige hatua nyingi sana mbele.
La muhimu pia achana kuwa kama mshumaa kubwa angaza wengine hali wewe unateketea , hao ndugu jamaa na marafiki na pengine wazazi wawe sehemi ya mwisho kwenye mapato yako, kipaombele kwenye mapato yako kiwe nikiongeza thamani na kukuza mtaji.