Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

🤔,Kazi kweri kweri
 
Hivi ni lini Tanzania iliishiwa pesa? na ilichukua hatua Gani? Kufulia Kwa nchi sio mchezo kama Tanzania ikifulia Kuna rasilimali nyingi za kuzipush kuanza na zile pembe za ndovu za kwenye Royal tour.
Kipindi mwinyi anakamata madaraka 1985,, naskia zimbabwe na nchi gani sijui wakaokoa jahazi
 
Kipindi mwinyi anakamata madaraka 1985,, naskia zimbabwe na nchi gani sijui wakaokoa jahazi
Hata sasa imefuria. Ninwiminya tatu sasa hakuna malipo yoyote yanayoendelea katika nchi kwani fedha zimepelekwa kwenye uchaguzi ndani ya chama.
 
Kuna muda unapigika unazurura ukimuona mtoto anatafuna hata kachori unamtamani.😂😂🙌 Unaona hata kakipande ka nanasi unakatamani ila ndio hvyo huna hata 200.

Kuna siku niko ndani nimebakiwa na buku mbili tu. Mtoto wa jirani kaja kunigongea mama yake ananiita. Kutoka anasema hana hata mia mbovu hajua watoto watakula nini. Nikajikuta namuhurumia nikampa ile buku mbili. Then nikarudi zangu ghetto siko hiyo nilikula usiku kwa mbinde.
Siku nyingine niko nimetoka home sina kitu nina buku mbili tu tena nikasema ngoja nikapate chai. Nakatiza mtaa nakutana na dada ana mtoto anasema njaa inauma na hana hata kitu. ikabidi nichenchi ile buku mbili then nikampa buku ikabidi nirudi home then ile buku iliyobaki nikaitumia mchana nikaua winga.

Mwenye nyumba ananidai kodi ya miezi mitatu. Kaja home nikamshindilia na kibomu. Japo alinipatia ila ilibidi kwanza acheke😂😂🙌 Tukabaki kucheka wote maana ilikuwa inachekesha.
 
Shida ni mbaya sana Mungu aendelee kutusaidia wapambanaji nakosa hata maneno ya kusema.
 
Hahah
 
Mimi mpka sahizi kuna mdada mmoja

anauza bar ndio ananisahidia ,[emoji1787] juzi kanunua nyama ya ngombe nusu kaja kapika geto,.

Naipigia bajeti hii mboga acha kabisa kila siku nakula kipande kimoja na mchuzi wakutosha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] jan kaja akaniuliza mboga haiishi tu
 
sorry bro nimecheka sana
 
Huwezi jua, pengine anajiwekea akiba, na akakusaidia usogeze siku.
 
Unakosa pesa hadi unamwambia landlord nkopeshe kodi nlokulipa mwezi wa kwanza.
 
Ulichosema ni kweli, sikia jambo lingine lakini sio kuchacha, hata bendi ya Wanamsondo waliwahi kuimba. "Maradhi yote ugua lakini kuchacha usiombee"
Ni kheri nichache, ila sio kuumwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…