Dah wakuu! Hii situation ya kuishiwa ni mbaya sana na ndo ninayoipitia sasa. Yaani hapa ninavyoandika hii comment mfukoni nimebaki na buku 3 tu! Then ndani stock ya chakula imekata, umeme imebaki unit 1.63 alafu sijala chochote toka asbh na harakati zangu zimeyumba kwa kipindi hiki sio mchezo, mbaya zaidi wife kuanzia kesho siku yoyote anarudi home maana alienda kwao kusalimia mara moja.
Yaani hapa nilipo nimechill gheto nawaza vitu vingi hadi kichwa kinauma. Nilichoamua hapa nimeenda kuchukua unga nusu nitoe kitu badae mishale ya jioni then unga utakaobaki wa kesho, nitachukua na fungu la dagaa, najua kwenye buku 3 itabaki kama 1300 hv hii nitaamka nayo kesho na akili mpya.
Ila ndugu zangu kuishiwa kubaya sana, hapa nimezima kila kitu kinachotumia umeme ili tu usije kukata maana muda wote naichungulia hiyo unit ili inifikishe kesho nijue nafanyaje kusurvive na siku mpya.
NB: Najua hii changamoto ninayopitia mm kuna mtu pia mahali anaipitia at the same time, hivyo cha muhimu ni kujua na kuamini kila jambo linatokea kwa kusudi maalumu na litakwisha tu.