Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Kufulia kunaleta akili ya ziada, kuna zile hela huwa zinaanguka chini ya kitanda hasa sarafu 100, 200 au 500 sasa ukitaka kujua thamani yake siku ufulie mazima huwa zinatafutwa kila kona ya chumba.. unapitia nguo moja moja kujua kama kuna akiba yoyote hapo orodha ya watu wa kukusaidia inazidi kujipanga kichwani na sababu za kuwapa.. "ipo siku tu.."
 
PESA PESA PESA Dah Sijui nani alievumbua haya mambo

Nilishinda siku 6 bila ya kula chakula chochote. Ulikua ni mwendo wa kunywa maji tu dumu za kuogea nilizimaliza zote. mwisho niliumwa na tumbo vibaya mno, ilikua ni michubuko tumboni.
Kwamba ukae siku sita bila kula chochote halafu usife?
 
Kufulia kunaleta akili ya ziada, kuna zile hela huwa zinaanguka chini ya kitanda hasa sarafu 100, 200 au 500 sasa ukitaka kujua thamani yake siku ufulie mazima huwa zinatafutwa kila kona ya chumba.. unapitia nguo moja moja kujua kama kuna akiba yoyote hapo orodha ya watu wa kukusaidia inazidi kujipanga kichwani na sababu za kuwapa.. "ipo siku tu.."
hahhh yaani kasheshe mkuu
 
Mie nilipigika ile kisawa sawa nikamwomba x afanye backup hahaha sharti ikawa turudiane daaah nikakubali akanipa 300k

Baadae nikawa kwale kama wiki 2 nikarudisha na cha juu 400 hataki anataka turudiane

Wacha siku nipigike nimcheki akanikazia hahahaha
Cha muhimu maisha yaendelee, tungekuwa wezi, akili ingekimbilia kwenye kuiba ili kutatua tatizo.
 
umenikumbusha wakati nasoma advance likizo nilikuwa nabaki hapo mkoani kwa ndugu. tuition walikuwa wananilipia ila kuna likizo waliishiwa mama akaniomba nimkope [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaah
 
Daah..maisha haya..nimeshawah kushinda takriban masaa 60 bila kula..na masaa 12 ya mwisho nikanywa maji ya moto tuu..hapo nimepanga nyumba moja hivi..na ndan ya hyo nyumba kuna wapangaji 3 tofauti na mim nikiwa wa tatu kwa hyo ni kaya tatu ndani ya nyumba moja...yaan nimeishiwa kila kitu..sina hata ndururu! Kaya moja kati ya tatu..wanaishi familia ya watoto wawil wadogo mama baba na mfanyakaz..kaya nyingine anaishi dada mmoja na boyfriend wake..na kaya nyingine naishi mim peke yangu..na kipind cha nyuma nilikuwa na manz angu tukatibuana..na baada kama ya miez 5 nikasikia anatembea na jamaa mwingine huku akiwa na ujauzito wa huyo jamaa...hapo ndani maji mnalipa flat rate haijalishi ww unaishi peke yako au vip.. ikija bill kama ni 30,000 itakubid mlipe sh 10,000 kwa kila kaya..umeme tu ndio nilikuwa nachangie na yule dada mwenye jamaa ake caz ndio tulishare meter...kuondoa aibu naamka asubuh sana nabeba vyeti nasambaza sana...unatoka gongolamboto mpaka mbagala kwa mguu..unarudi kuna jamaa mmoja pale posta nyuma ya chuo kimoja hivi(sitakitaja) ni fundi viatu na kwa jina anaitwa samora..yule jamaa ana connection nying sana za kaz..sasa nilikuwa nikifika pale tunapiga story za hapa na pale na thn ananipa abc's za kaz ..hapo msoto haswa unajiweka hali ya kufurah yaan kama huteseki vile..lakin moyon unajijua...so akiniambia mtafute hyu bas bila kuchelewa..nitamtafuta mdau kwa njia yyte ile..nitahangaika wee ikifika saa mbil ya usiku narud geto..naoga thn natoka naenda kushinda kwenye yale majumba ya kubetia..yaan pale najua kuna mipira wanaonesha so nitapoteza muda mpaka wanapo karibia kufunga..,.na hapo kuna makamaria wakila utasikia mkuu chukua buku hii..au jelo bas tunaishi..sasa bas nikupe siri yaan ni bora nisile siku nzima lakin sio kukosa vocha au dk za maongez kwenye simu...na hii dhana ninayo mpaka leo..maisha yakawa magumu kiasi kwamba nataka kurudisha mpira kwa kipa..lakin dah moyo unagoma..na kipindi hicho kuna ile kauli ya mkuu alisema atakae weza kukaa kwenye mkoa huu mpaka mwez wa sita yy ni mwanaume..basi ile kauli ilinipiga kwenye utosi sio kawaida..ilikuwa inarudia rudia sana kila ninapo ptia changamoto....hali bado ikawa bila bila kula yangu ni ya shida sana..ikafika kipind nyumba nayokaa nabaki mim na yule mfanyakaz wa kaya nyingine anae lea wale watoto wadogo..akiwa anapika tuu natoka ndan kwangu nampigisha vistory vya hapa na pale ili anizoee tuu..basi nikafanya hivyo kama wiki tatu mfululizo akawa amenizoea..sio sanaa..sasa kuna siku sikutoka kabisaa ndan na akajua..akaja dirishan kwangu na kuniita ilikuwa mida ya saa nane mchana..nikaitika akasema njoo nikasema poa..natoka pale nakuta ana sahan ya wali kuku..Mungu wee umejuaje..nikanena kimoyo moyo..nikamshukuru sana..niliufinya ule wali ndn ya dk 3..nikaenda bomban nikanywa maji na kuiosha sahan..ile namrudishia akaniambia umekula? Nikamjibu ndio na nimeshiba sana..akabak ananishangaa kwa kumaliza chakula haraka...binafsi nilishukuru sana..siku hyo ikapita..kesho yake nikaenda kutana na mshksji wangu ambae tulisoma nae chuo lakin alinitangulia madarasa mawil yaan nikiwa mwaka wa kwanza yy alikuwa watatu...na tulikuwa tumepanga kwenye hostel moja huko kwa josee mtambo mzee wa kiga...no.. so ninapomaliza mwaka wa tatu yy alikuwa anamalizia research caz aliunganisha masters..so hyo siku tulipanga tuonane..nae dah kwanza anaish hostel ya chuo nae kapigika haswa..lakin akaniambia kuna mtu nakuunganisha nae akupe laki 3..yupo equity sasa sikua mbal sana na eneo nilipo mpaka hyo bank..ingawa hyo jamaa aliniunganisha nae namfaham..caz walisoma wote na mshkaj wangu..so nikasema poa ngoja nimcheki..nikatoka zangu maeneo ya chuo mpaka ppf tower pale pemben ndio ilipo eqty..sasa nafika pale dah nakutana na manz angu niliye zinguaga nae..mimba yake kubwa haswa..dah roho ilinipasuka paa..kwa kweli nilipata maumivu makal sana..ingawa sikumuonesha..tukasalimiana pale na akaniuliza unaenda wap nikamjibu naenda bank ya hapo juu..sasa jengo hilo lina banks mbili juu ndio ipo eqty na chin ndio ipo bnk nyngne..ambayo yy ndio alikuwa anafanyia..akanambia ukitoka utanikuta hapa..nikasema poa nikapandisha..nikakutana na jamaa tukaongea thn akanipa ahadi..ile nashuka nikamkuta pale pale..thn akaniuliza unaelekea wapi sasa..nikamjibu naelekea kkoo kuna mzigo naenda funga..nikamdanganya..kula yangu tuu ya manga..khee! Akaniambia na yy anaelekea huko kwan kuna mzigo wa vipodoz anaenda funga..looh sasa siku zote nikiwa na mtt wa kike ingawa ni nadra sana kutoka nao..huwa kama ni nauli nitalipa na hata ikitokea akinikuta hotel basi nitamlipia thn nitasepa..bwans eeh posta pale bajaji wengi chibaa..nikajifanya namuuliza hivi mazoez unafanya kwel maana kwa hali yako inabid ufanye mazoez..akajibu huwa nafanya..nikamwambia hya sasa twende taratibu mpaka kkoo..kumbe kidume sina kituu..yaan kama hamna kitu vile lakin moyon naumia sana..alikataa katu katu..akafika tuu kwenye bajaj akaingia akakaa..ikabid na mim niingie..mfukoni nilikuwa na 8,00 tuu..akamwamrisha yule mzee tupeleke kariakoo..basi tukatoka pale tukafika..ile nashuka najifanya natoa pesa mfukon ..akaniita aah aah natoa huku..kabla hajashuka akampa dereva 5,000 kimoyomoyo nikasema asante Mungu..basi nikasema ngoja nikusindikize ww kwanza thn mishe zangu nitazimsliza baada ya zako kuishaa...tulifika mpaka mtaa wa msimbaz pale.. maduka ya vipodoz akanunua kama mzigo wa mil 6 hivi.. dah thn akaniambia nimefungua duka mkoan huku akinionesha picha..duh ni duka kubwa..nikamuuliza mbona kama limezid mil 20 akajibu alianza na mil 35.. nikamwambia hongera mwaya..bas nikamsaidia pale alipo maliza ...yy ananunua anaacha afu kuna kijana anakuja kukusanya..basi nikamsindikiza akapanda bajaj kurud ofisin..na mimi nikaanza mdogo mdogo..nilifika geto nikiwa na mawazo mengi sana! Baada ya pale niliichukia nafsi yangu..niliingia kufanya biashara ya risk sana ingawa ilikuwa legal bt baadae mbeleni ile biashara ikaja pigwa vita kali sana na serikal..(mkaa) hapa hakuna nyota niliacha kuiona..
Andika vizuri khaaah
 
Kufulia hakujawahi muacha mtu salama! Iwe mtu, kampuni au Serikali. Hata serikali pamoja na kwamba inakusanya kila kitu lakini ikiishiwa huwa inawaza kukusanya kodi kwenye barabara na madaraja wakati yamejengwa kwa kodi zao!

Kuna wakati vyuma vinaweza kukaza kila kona hadi ukatamani kumkopa pesa dada wa kazi ilihali hujamlipa mshahara.
Alafu katu Haina taarifa, shida huingia shida Bila hodi sio kwa mkubwa wala mtoto wote shida. Pia haikosekani hata ikiwa siku ya harusi, si masikini wala matajiri wote shida. Kikubwa marufuku kukata tamaa.
 
Alafu katu Haina taarifa, shida huingia shida Bila hodi sio kwa mkubwa wala mtoto wote shida. Pia haikosekani hata ikiwa siku ya harusi, si masikini wala matajiri wote shida. Kikubwa marufuku kukata tamaa.
 
Hivi ni lini Tanzania iliishiwa pesa? na ilichukua hatua Gani? Kufulia Kwa nchi sio mchezo kama Tanzania ikifulia Kuna rasilimali nyingi za kuzipush kuanza na zile pembe za ndovu za kwenye Royal tour.
 
Kuna Siku nilikwama sana, kila nikiwaza sipati jibu, la hela. Nikaona nimwangushie zigo mama watoto, ambae tumeachana miaka minne iliyopita kipindi hicho nina Shida.

Pamoja na kuachana, huwa tunawasiliana mara kwa mara kama wazazi, ingawa tunaishi mikoa tofauti, hivyo baada ya kukosa pesa nikamjaribu, aniazime Tsh 200,000 kama anazo he, akaniambia ndani ya masaa matatu atanitumia, kweli akanitumia yaani nilishukuru sana, alinifanya niendelee kujiamini Siku ile.
Daaaaah sa c mrudiane tu mnakwama wap ujue ndo ashakuombamsamaha hivo!
Maisha yanapiga Mwaisa mpaka Maji tunaita Mmma.
 
Sitaisahau Manzese Argentina, pale kulikua na mzee mmoja ana uza maandazi mia na chai mia, usiku kibao nimelalia mia tano, kuna wakati unakua una mia tano tu mfukoni, unasema hii jero ntaenda zangu jioni kwa mzee nile maandazi manne na chai moja. Enzi izo nilikonda kama mbwa, hali mbaya.
 
Back
Top Bottom