Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Vincious circle of poverty. Familia maskini, mtoto anazaliwa kwenye umaskini, anakosa elimu Bora na ujuzi anapata shida kupata kazi na anaendelea kubaki kwenye umaskini mpaka apate external force to push out from poverty
Hyo external force ni ipi mkuu?
 
Kuna mwaka nilikua nimefulia sina hata sumni nikafanya kosa la mwaka nimeongea na mwanangu mmoja akaniita sehemu njaa inagonga vibaya badala ya kunipa hela ananinunulia bia tu .Mwisho tukaanza nyagi nikawaka vibaya sana akanidrop gheto ye huyooo kwake.Kimbembe nimestuka usiku mnene ile njaa ikawa imejidabo .Simu haina kifurushi,ndani hamna kitu kuna gesi tu.Nguvu sina .Kwa mara ya kwa nza nilikua supu ya marando.Kwa wasiojua marando ni majani yale ya viazi vitamu .Na niliyala asubuhi ,mchana na jioni .Kwa bahati nzuri bi.mkubwa jioni akanipigia ndio pona yangu .Vinginevyo nilikua nafia ndani.
Daah...imenibidi nicheke tu[emoji16]...maana kadhia ya njaa naijua
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
PESA PESA PESA Dah Sijui nani alievumbua haya mambo

Nilishinda siku 6 bila ya kula chakula chochote. Ulikua ni mwendo wa kunywa maji tu dumu za kuogea nilizimaliza zote. mwisho niliumwa na tumbo vibaya mno, ilikua ni michubuko tumboni.
 
PESA PESA PESA Dah Sijui nani alievumbua haya mambo

Nilishinda siku 6 bila ya kula chakula chochote. Ulikua ni mwendo wa kunywa maji tu dumu za kuogea nilizimaliza zote. mwisho niliumwa na tumbo vibaya mno, ilikua ni michubuko tumboni.
Duh pole... inawezekanaje aisee...siku zote hizo bila kula
 
hakuna kushuka heshima kama unalipaaa...heshima inashuka kama unakopa alafu unakuwa msumbufu...!! me kuna ndugu nlimkopa laki akasema atanilipa hakunilipa hadi kesho lakini akiwa na shida mimi huwa namsadia bila kinyongoo

Hivi unajua kuna tendency hile ukimkopa mtu kwa mara ya kwanza ukamlipa kwa wakati, sasa siku ukipata tatizo utamuwaza yeye akusaidie tena sasa hapa lazima hata kama atakupa kuna hali inakua sio ya kawaida na heshima aliyokua anakupa awali anaweza ishusha binadamu banah
 
Daah nakumbuka msoto niliwahi kupitia kipindi hiko nilivyomaliza form 4, nikakutana na sister yangu mtoto wa mama mkubwa slay queen kipindi hicho ameukwaa u misss Morogoro, maktaba DSM pale navuka zebra yupo kwenye harrier yake mbele na tumeonana kabisa akaangalia pembeni, hapo mfukoni nina 200, nikagonga kioo nimpe hata salamu, akauchuna haangalii kabisa, mara taa zikawaka akainua, aisee iliniuma sana ila Mungu alivyo mwema baada ya kuvuka taa tuu hatua mbili tatu nikakutana na mjomba wangu akaniambia twende hivi, tukaishia mgahawa flani nikapata heavy breakfast na laki moja cash, cha ajabu huyu mjomba ni bahili kinoma kwa ndugu zake wengine.

Nilijifunza kuacha kuhukumu kabla hujamjua mtu, mimi na uncle wangu ni du damu kwa muda huu na huyu sister sijawahi kuacha kumsaidia akija na shida zake, na anakuja mara kwa mara, nilisamehe lakini sijawahi kusahau hii scenario... ipo siku nitamkumbusha
Akija wikiendi ijayo mkumbushe,nipe namba zako niwe nakupigia ili umkumbushe hio scenarios
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] huu uzi nimecheka sana, maana umekuja wakati muafaka kabisa. Mimi ijumaa, jumamosi na jumapili nilikuwa sina hata mia, ninaposema mia mnielewe...ni ile mia yenye moja na sifuri mbili. Nilianza kusachi mikoba, mabegi kabatini labda kuna siku nilisahau hata buku wapi...bahati nzuri jana nimeenda kanisani nikakutana na mtu nilikuwa namdai elfu tatu ndio akawa mkombozi wangu. Maisha haya yasikie tu

Kama kweli vile [emoji2955]
 
Unakopaje kwa dada wa kazi hana uwezo wowote haka kukupa 50K, 100k.
Kuna housegal unamlipa 100k mbona ni kitu kinawezekana, hosuegal wa siku hizi sio wale wakulipwa elfu20, au elfu 30, maisha yamebadilika
 
Kwa kweli hapo mtu unatakiwa ujifikirie kama kuna umuhumi wa kuleta viumbe wengine dunia hii.. Lakini kama hali inaruhusu hata wasizidi wawili...ili waweze kusaidiana mbele kwa mbele sio unaleta mmoja halafu ghafla wote mnavuta....sipati picha....
Man,Maisha saa nyingine Ni upuuzi linapokuja swala la watoto,Mobutu alikuwa na watoto wanne wa kiume wakaanza kufa kwa kufuatana wakiwa watu wazima,wa Kwanza kuzaliwa kafa 1993,wa pili 94,wa nne 98 na wa tatu 2006
Kwa kweli hapo mtu unatakiwa ujifikirie kama kuna umuhumi wa kuleta viumbe wengine dunia hii.. Lakini kama hali inaruhusu hata wasizidi wawili...ili waweze kusaidiana mbele kwa mbele sio unaleta mmoja halafu ghafla wote mnavuta....sipati picha....

Fikiria maisha magumu unaenda kutoa msongo kwa papuchi ya wife na unamalizia humo
unategemea matokeo yake ni nini..

Tuliwahi kupitia masha magumu sana kifamilia bado wadogo, mpaka nikawa nawaza kwanini baba alituzaa wengi hivi...

Kwa kweli kama sina uwezo sitaleta viumbe vingine kuja kuteseka duniani..
 
Kuna housegal unamlipa 100k mbona ni kitu kinawezekana, hosuegal wa siku hizi sio wale wakulipwa elfu20, au elfu 30, maisha yamebadilika

Naona Wengi wanalipwa 50,000- 70,000. Wana matumizi yao ya kama wanawake wengine, nguo, viatu, sanitary items, kanisani, msikitini, vocha, Kutuma pesa kidogo nyumbani.

Anyway labda inawezekana.
Nani kakwambia
Amefanya kazi 12 months anapata 60,000 yake
Hatumii hovyo anashindwa kukukopesha laki?
Niambie.
 
Back
Top Bottom