EEX
JF-Expert Member
- Oct 19, 2014
- 3,781
- 12,091
Kuna mwaka nilikua nimefulia sina hata sumni nikafanya kosa la mwaka nimeongea na mwanangu mmoja akaniita sehemu njaa inagonga vibaya badala ya kunipa hela ananinunulia bia tu .Mwisho tukaanza nyagi nikawaka vibaya sana akanidrop gheto ye huyooo kwake.Kimbembe nimestuka usiku mnene ile njaa ikawa imejidabo .Simu haina kifurushi,ndani hamna kitu kuna gesi tu.Nguvu sina .Kwa mara ya kwa nza nilikua supu ya marando.Kwa wasiojua marando ni majani yale ya viazi vitamu .Na niliyala asubuhi ,mchana na jioni .Kwa bahati nzuri bi.mkubwa jioni akanipigia ndio pona yangu .Vinginevyo nilikua nafia ndani.