Ila
Mshana Jr mimi niseme jambo moja tu kuwa hayo ni matokeo ya kirithi tabia. Unajua tabia zinaambukiza kama magonjwa mengine.
Watoto huwa wanatazama waliowakuta Duniani wanaishi kwa mfumo gani kisha nao wanaukopi na kuishi vile vile sio jambo linawakuta kimiujiza. Kwa mzazi ukiona mtoto wako anatabia za hovyo au nzuri jua ni copy yako hiyo. Watoto huwa wachukui tabia mbali, an apple [emoji520] doesn't fall far from the tree.
Nitakupa mifano miwili. Wa kuna ndugu yangu wa kike upande wa baba kipindi cha usichana wake alikuwa na boyfriend ambaye alikuwa anajitoa sana kwake. Ila huyu ndugu yangu alikuwa ni wale wanawake machepele.
Akaruka na jamaa m'moja mlugaliga mixer jamaa ni mganga wa miti shamba, akanasa ujauzito wa jamaa. Alipoona hali sio nzuri akamuwahi jamaa yule anayempenda kwa dhati akampa mchezo kisha akabambikia ule ujauzito kuwa yeye ndie baba.
Jamaa akakubali ila still akawa hataki kuishi nae maana alitaka amtumie. Jamaa akakubali kuwa mpango wa kando. Huyu ndugu yangu akajakuolewa na mtu mwingine kabisa. Sasa tazama huo mchoro. Baba mzazi ni muhuni fulani ambaye hana ramani, halafu mtoto kaja kupewa jina la baba ambaye si mzazi, kisha mtoto anashuhidia mama anaishi na baba mwingine wa tatu.
Picha sasa ni mtoto nae kaja kurudia mfumo ule ule. Alikuwa na boyfriend wake mjeda, jamaa akawa ameenda huko mbali kikazi , mama yake anamwambia kuwa askari wa jeshi wanaroho za umauti kwahiyo asimuwekee kuwa watakuwa na maisha ya familia amtumie kupata mahitaji. Binti akaenda kulala na mwanaume wa mtu na kupata ujauzito wake, halafu amekuja kumbambikia jamaa mwingine kabisa na mtoto kaandikwa jina la huyu jamaa wa tatu.
Sasa uone namna tabia zinarithishwa na sio maswala ya miujiza wala kurogwa.
Upande mwingine kuna swala la mifumo. Ndio maana wazazi zamani walikuwa wanachagulia vijana wao koo za kuoa na mabinti walikuwa wanachaguliwa na wazazi koo za kuolewa ili kulinda mifumo isikutane na changamoto za kurithishwa kama hizo.
Watu wengi leo kitu cha kwanza wanazaa halafu ndipo wanaanza kutazama kazaa na mtu wa aina gani. Kimsingi tafuta mtu ambaye unaelewa anatoka familia ya namna gani na ina mifumo gani.
Kuna familia wana tabia za ubinafsi na tamaa. Kuna familia zina asili ya uchapa kazi na kutafuta mafanikio na kujijenga, kuna familia zina ajizi iliyopitiliza, kuna familia wanatabia za umalaya uliojificha na unafanywa kwa coordination kali sana kiasi kwamba usipowachunguza utasema ni watu waliostaarabika kumbe ni malaya wa haswa.
Kuna familia wizi ni sehemu ya maisha yao wanaiba hadi ukweni na kitapeli ndugu na jamaa zao. Kuna familia ndugu kuchukiana ni mtindo wamezoea kiasi kwamba ukiingia utashangaa wanaanza kuwaingiza na nyie katika utamaduni wa kuchukiana na kufitinishana, kuna familia wana asili ya uharibifu na kurudi nyuma, ukioa au kuolewa huko utashangaa ndani ya miaka kadhaa umechakaa na kufilisika kama haukuwa na kitu.
So yote kwa yote chunguza na kutazama nature ya familia unayokwenda kuoa au kuolewa.