Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

Meditation inayoongelewa ktk Psalms19:14 ni kutafakari neno la Mungu.

Meditation ya Yoga ni tofauti na hiyo ktk BIBLIA, meditation ya Yoga lazima ukunje miguu ktk mkao Fulani na kuweka mikono ktk pause Fulani Ili kucomnect na Ulimwengu mwingine.

Meditation na uchawi hauna tofauti, anayemeditate anachelewa Kutoka ktk mwili sababu anafanya ktk uwazi bila kificho ukilinganisha na mchawi ambaye huingia ktk Siri.

Mungu amekataza watu kupractice uchawi au kujiconnect au Kutoka mwilini Kwa kutumia jicho la Tatu la Shetani.
SAWA.
 
Ila Mshana Jr mimi niseme jambo moja tu kuwa hayo ni matokeo ya kirithi tabia. Unajua tabia zinaambukiza kama magonjwa mengine.

Watoto huwa wanatazama waliowakuta Duniani wanaishi kwa mfumo gani kisha nao wanaukopi na kuishi vile vile. A
Hizo tabia ndio mapepo yenyewe sasa
 
Hiyo sauti ya ndani utaisikia kadiri ya IQ. Kama uwezo wako wa kufikiria umeegemea zaidi kwenye imani za kishirikina, basi sauti utakayoisikia ndo kama ya mleta mada.

Ila kama umejizoesha kufikiria Kwa mawazi huru yenye kuleta logic, huwezi kuhusianisha changamoto zako na habari za mapepo Bali utajibidiisha kuumiza kichwa kuangalia umekosea wapi urekebishe
Kuna mambo ni magumu sana kueleweka na akili za kawaida, yapo mambo ili kuyatambua yanahitaji ufahamu wa ziada. Mambo mengine akili ya kawaida haiwezi kuyatatua mkuu
 
PSALM 19:14

14 May these words of my mouth and this MEDITATION of my heart be pleasing in your sight, LORD, my Rock and my Redeemer.
ZABURI 19:14

14 Maneno haya ya kinywa changu, na KUFIKIRI kwa moyo wangu, na yapate kibali machoni pako, Ee Yehova, Mwamba wangu na Mwokozi wangu.[emoji1548][emoji1545]
 
ZABURI 19:14

14 Maneno haya ya kinywa changu, na KUFIKIRI kwa moyo wangu, na yapate kibali machoni pako, Ee Yehova, Mwamba wangu na Mwokozi wangu.[emoji1548][emoji1545]
Vijana wanasema meditation na yoga ni ushirikina mkuu.
 
Mifano hai ipo.
 

Attachments

  • Screenshot_2023-04-17-07-06-37-57.png
    Screenshot_2023-04-17-07-06-37-57.png
    136.5 KB · Views: 9
Kuna vetting huwa inafanyika kwa mtu anayetaka au anayeteuliwa kwenye nafasi nyeti serikalini.

Kuna baadhi ya familia ukitaka kuingia lazima ufanyiwe vetting ya kutosha, usipokidhi vigezo huingii kwenye hiyo familia ama kwa kuoa au kuolewa....

Na wakuu wa koo/familia wako makini na hilo lengo ni kutopoteza mali na kuingiza mipenyo itayowatafuna kama magonjwa nyemelezi, umaskini, laana, ukichaa/kurukwa na akili, ulevi n.k.
Hii ilikuwa zamani sana na baadhi ya makabila/koo, siku hizi pesa mbele vetting kuleee.....
 
Labda niseme "dini ni umasikini" kwa nini? Katika familia kama kuna mshirikina na anawatafuna, mnaishia kusema "tunamuachia Mungu" mtaisha, weka imani chini ili mpambane nae, ama zake ama zenu. Afutike katika uso wa dunia.
 
Ila Mshana Jr mimi niseme jambo moja tu kuwa hayo ni matokeo ya kirithi tabia. Unajua tabia zinaambukiza kama magonjwa mengine.

Watoto huwa wanatazama waliowakuta Duniani wanaishi kwa mfumo gani kisha nao wanaukopi na kuishi vile vile sio jambo linawakuta kimiujiza. Kwa mzazi ukiona mtoto wako anatabia za hovyo au nzuri jua ni copy yako hiyo. Watoto huwa wachukui tabia mbali, an apple [emoji520] doesn't fall far from the tree.

Nitakupa mifano miwili. Wa kuna ndugu yangu wa kike upande wa baba kipindi cha usichana wake alikuwa na boyfriend ambaye alikuwa anajitoa sana kwake. Ila huyu ndugu yangu alikuwa ni wale wanawake machepele.
Akaruka na jamaa m'moja mlugaliga mixer jamaa ni mganga wa miti shamba, akanasa ujauzito wa jamaa. Alipoona hali sio nzuri akamuwahi jamaa yule anayempenda kwa dhati akampa mchezo kisha akabambikia ule ujauzito kuwa yeye ndie baba.

Jamaa akakubali ila still akawa hataki kuishi nae maana alitaka amtumie. Jamaa akakubali kuwa mpango wa kando. Huyu ndugu yangu akajakuolewa na mtu mwingine kabisa. Sasa tazama huo mchoro. Baba mzazi ni muhuni fulani ambaye hana ramani, halafu mtoto kaja kupewa jina la baba ambaye si mzazi, kisha mtoto anashuhidia mama anaishi na baba mwingine wa tatu.

Picha sasa ni mtoto nae kaja kurudia mfumo ule ule. Alikuwa na boyfriend wake mjeda, jamaa akawa ameenda huko mbali kikazi , mama yake anamwambia kuwa askari wa jeshi wanaroho za umauti kwahiyo asimuwekee kuwa watakuwa na maisha ya familia amtumie kupata mahitaji. Binti akaenda kulala na mwanaume wa mtu na kupata ujauzito wake, halafu amekuja kumbambikia jamaa mwingine kabisa na mtoto kaandikwa jina la huyu jamaa wa tatu.

Sasa uone namna tabia zinarithishwa na sio maswala ya miujiza wala kurogwa.

Upande mwingine kuna swala la mifumo. Ndio maana wazazi zamani walikuwa wanachagulia vijana wao koo za kuoa na mabinti walikuwa wanachaguliwa na wazazi koo za kuolewa ili kulinda mifumo isikutane na changamoto za kurithishwa kama hizo.

Watu wengi leo kitu cha kwanza wanazaa halafu ndipo wanaanza kutazama kazaa na mtu wa aina gani. Kimsingi tafuta mtu ambaye unaelewa anatoka familia ya namna gani na ina mifumo gani.

Kuna familia wana tabia za ubinafsi na tamaa. Kuna familia zina asili ya uchapa kazi na kutafuta mafanikio na kujijenga, kuna familia zina ajizi iliyopitiliza, kuna familia wanatabia za umalaya uliojificha na unafanywa kwa coordination kali sana kiasi kwamba usipowachunguza utasema ni watu waliostaarabika kumbe ni malaya wa haswa.

Kuna familia wizi ni sehemu ya maisha yao wanaiba hadi ukweni na kitapeli ndugu na jamaa zao. Kuna familia ndugu kuchukiana ni mtindo wamezoea kiasi kwamba ukiingia utashangaa wanaanza kuwaingiza na nyie katika utamaduni wa kuchukiana na kufitinishana, kuna familia wana asili ya uharibifu na kurudi nyuma, ukioa au kuolewa huko utashangaa ndani ya miaka kadhaa umechakaa na kufilisika kama haukuwa na kitu.

So yote kwa yote chunguza na kutazama nature ya familia unayokwenda kuoa au kuolewa.
 
Kuna familia naifahamu mabinti wote wsmeachika kwa waume zao. Vijana wa kiume wote wamezaa nje ya ndoa....

Mnyororo
Ipo hapa mtaani mzee ana watoto tisa, wakike ni saba wa kiume wawili. Wadada wote wamezalishwa tena sio mtoto m'moja wamezidiana idadi ila kila m'moja ana watoto zaidi ya wawili. Wamerudishwa nyumbani wote na watoto. Mzigo anabeba bibi yao.
 
Kuna vetting huwa inafanyika kwa mtu anayetaka au anayeteuliwa kwenye nafasi nyeti serikalini.

Kuna baadhi ya familia ukitaka kuingia lazima ufanyiwe vetting ya kutosha, usipokidhi vigezo huingii kwenye hiyo familia ama kwa kuoa au kuolewa....

Na wakuu wa koo/familia wako makini na hilo lengo ni kutopoteza mali na kuingiza mipenyo itayowatafuna kama magonjwa nyemelezi, umaskini, laana, ukichaa/kurukwa na akili, ulevi n.k.
Imagine unatoka familia ambayo baba yako ni Dereva wa daladala na hakuna aliyesoma hata kufika darasa la saba halafu mtoto wako awe bishoo akutane na mjukuu wa kimei club wapendane , siku ya kutambulishwa lazima mpigwe chini kama fuko la mzoga.
 
Yeah, kuna kila sababu na haki kwa watu kulinda watu wao kutokana na wasiojulikana na wakijulikana wana mawaa shurti kuwaweka mbali na watu wako wa karibu.

Kujichanganya na kama mbalimbali kumeharibu na kuvuruga mipango ya wengi ya maendeleo.

Unatafutiwa mke/mume unachaguliwa ujuzi wa kuwa nao kujkendesha kimaisha, unaandaliwa kujitegemea na kuinua wengine .......
Huwa nawaambia watu kinachoweza kukuangusha mwanaume /mwanamke unapokwenda kuoa /kuolewa ni aina ya familia anayotoka mwanamke/mwanaume wako.

Kama ni watu wa hovyo tegemea ule upuuzi wao utakuja hadi sebuleni kwako. Unless uamue kuwa kauzu na mkeo au mumeo akusapoti muwe kitu kimoja kukataa upuuzi usije katika familia yako unayotengeneza.

Familia huwa ndizo zinaharibu Ndoa na mahusiano sababu ya kuingiliwa na muingiliano wa tamaduni ambazo hazimatch.

Imagine wewe labda unatokea kwenye familia decent, baba mzazi akija anakutembeleeni kisha halali hapo unapoishi sababu ya udogo wa nyumba au mwingine ni maadili yake tu hawezi lala kwenye mji wa watoto sababu ni mwiko. Halafu ukaoe au kuolewa familia za kiswahili ambazo baba na mama mkwe na watoto wao wanaweza kuja sehemu unaishi tena ya chumba na sebule wakajiachia comfortable kabisa. Mkwe analala chumbani au sebuleni. [emoji23][emoji23][emoji23]

So kuna mambo ni ya kuchunguza kwanza tamaduni. Unaweza kutana na binti mzuri sana au kijana mtanashati sana ila familia anayotoka ni hovyo bin vuluvulu.
 
Back
Top Bottom