Kuna sababu kubwa za Marekani kutokuingilia vita ya Israel - Iran

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
2,375
Reaction score
4,784
Siku tatu zilizopita ilionekana kwamba US angeingia vitani, ila kwa hali ilivo sasa hiyo option inaenda ikipotea. Atachofanya US kuipa silaha Israel lakini sio direct involvement.

Kuna jambo limemuogopesha US kuingia kichwa kichwa, na hapo ni baada ya Iran kupiga Hypersonic bomb na pia intensity ya mashambulizi ya Iran kule Israel ni kama inazidi kuwafikirisha US kutokana na Iron Dome kuonekana kuelemewa kazi.

Wakiingia vitani US, maana yake zile bases zote za US middle East zitakuwa under attack, kitu ambacho kitawalazimu US kufanya land invasion ambayo ni vita kamili.

Sasa kulingana na experience yao ya Afghanstan, kule Iran land invasion itakuwa very costful kwa US na kuna hatari ya wao kushindwa kufanikisha malengo yao.

Kuingia kwenye vita kamili na Iran, ni jambo ambalo US administration hailitaki kwa sasa ukizingatia ya kwamba Federal Debt ipo katika record high 37 Trillion na kuingia vitani maana yake itawabidi deni liendelee kuwa kubwa zaidi, kitu ambacho kinaweza break american economy na kusababisha dollar iweze ku crash.

Lakini kuna suala lingine tata, nalo ni, Russia na China. Mpaka sasa inaonekana wapo kimya strategically, na inaonekana wanajipanga kimya kimya kuona ikiwa US atajiingiza vitani ili nao wa declare sides. Na inapojiingiza Russia dhidi ya Marekani, tutashughudia vita ya tofauti kabisa ukifananisha na Ukraine.

Kwa hiyo, hakuna probability ya US ku join directly hii vita, ingeweza kuingia mazima endapo kama Iran ingeonesha sign of weakness, ila resilience ya Iran imewatisha wakubwa wa NATO, unaweza kusema hivo.
 
Israel bado ina turufu kubwa katika vita hivi ambayo ni kuwaua viongozi wakuu wa Iran uwezo ambao wanao sana na ikitokea hilo itabadilisha kabisa mwenendo wa mambo.

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa sana ya wananchi wa Iran wamechoka kabisa na utawala huu wa sasa na wangependa kuona mabadiliko ya kiutawala yakifanyika nchini Iran.

Viongozi hao wakilengwa na kuuliwa hakuna uongozi mwingine utakaokuja na kuendeleza hayahaya yanayoendelea sasa.
 
Amka usingizini.
Iran Kuna maandamano makubwa Sana ya kuwapinga Marekani na Israel.
Wananchi wa Iran wameungana sana sasa kuliko wakati mwingine wowote.
 
Ukiacha makombora ya Iran kushindikana kutunguliwa kuna kingine ambacho ni kuhit taget.
Kingine ni nguvu ya mlipuko ambao unaonekana kuwa na nguvu kama yale mabomu ya Urusi kule Ukraine... Wewe fikiria bomu likilenga sehemu linasasambua hadi kilichoko karibu kitu ambacho haikutegemewa Iran kuwa nacho.
Mataifa ya kiarabu yaliandaliwa kwa vita na Iran ila walipoona kinachowapata Israel inayoaminika kudaka kila kitu ilibidi wamwambie uncle Sam atafute uwanja mwingine ndipo anawabembeleza Pakistan

Wamezoea kuharibu bila kuharibiwa ila kwa Iran wakiharibu wanaharibiwa pia
 
USA naye analiwa taiming akijichanganya kuingia kwenye hii vita direct Usuper power ndo bye bye na mchina Anachukua atamu
Mwandishi wa makala hii ameandika ukweli mkubwa sana.
Tena hapa Urusi anatamani sana USA na hata hao akina UK na EU wafanye kosa la kuingilia vita hii,nadhani watajuta kuwepo duniani.
Kwa sababu Urusi inatafuta kulipa kisasi kwa kile Wanachoifanyia katika vita yake na Ukraine.
Wanachofanya hao NATO huko Ukraine,Urusi nae atawafanyia kwa Iran.
Yaani wamekua wakimpa Ukraine misaada ya silaha, intelligence,mafunzo ushauri,fedha n.k ili kumdhoifisha Urusi,nae Urusi atawafanyia hivyohivyo kwa kumpa Iran Kila kitu atakachotaka kijeshi ili kumbomoa USA na NATO wake kwa lengo la kuwapunguza nguvu kama wafanyavyo wao.
Nafasi hii Urusi alikua anaitafuta sana na Sasa ameipata.
Kama utakumbuka kauli ya Putin kua nao wataanza kuwapa silaha maadui wa USA na NATO popote duniani kama vile wao wanavyompa Ukraine.
Urusi ilisema huenda Houth ikawa ya kwanza kupewa misaada hiyo baada ya kuona wa Houth Wana uthubutu na sio waoga.
Kumbuka lengo la NATO ni kutaka kumdhoifisha Urusi nae Urusi kapata nafasi ya kuwadhoofisha.
Urusi alitamani sana kumpa misaada kama hiyo Wa Houth lakini wa Houth ni wadogo sana hawana nguvu kama aliyonayo iran,Sasa ni kama wasemavyo waswahili kua upele umempata mkunaji.
Vivyohivyo kwa uchina nae ataitumia nafasi hiyo kumdhoifisha USA Kwa sababu ili ikitokea China akaivamia Taiwan USA asiwe na nguvu za kumchallenji.
Naona kitu watakachofanya Urusi na china ni kumpa Iran sophisticated weapons za kuweza kupiga target za silaha za USA ,UK na wengine popote zilipo middle east na hata deep sea,mfano aircraft carriers na makambi ya kijeshi.
 
Siku tatu zilizopita ilionekana kwamba US angeingia vitani, ila kwa hali ilivo sasa hiyo option inaenda ikipotea. Atachofanya US kuipa silaha Israel lakini sio direct involvement.

Kuna jambo limemuogopesha US kuingia kichwa kichwa, na hapo ni baada ya Iran kupiga Hypersonic bomb na pia intensity ya mashambulizi ya Iran kule Israel ni kama inazidi kuwafikirisha US kutokana na Iron Dome kuonekana kuelemewa kazi.

Wakiingia vitani US, maana yake zile bases zote za US middle East zitakuwa under attack, kitu ambacho kitawalazimu US kufanya land invasion ambayo ni vita kamili.

Sasa kulingana na experience yao ya Afghanstan, kule Iran land invasion itakuwa very costful kwa US na kuna hatari ya wao kushindwa kufanikisha malengo yao.

Kuingia kwenye vita kamili na Iran, ni jambo ambalo US administration hailitaki kwa sasa ukizingatia ya kwamba Federal Debt ipo katika record high 37 Trillion na kuingia vitani maana yake itawabidi deni liendelee kuwa kubwa zaidi, kitu ambacho kinaweza break american economy na kusababisha dollar iweze ku crash.

Lakini kuna suala lingine tata, nalo ni, Russia na China. Mpaka sasa inaonekana wapo kimya strategically, na inaonekana wanajipanga kimya kimya kuona ikiwa US atajiingiza vitani ili nao wa declare sides. Na inapojiingiza Russia dhidi ya Marekani, tutashughudia vita ya tofauti kabisa ukifananisha na Ukraine.

Kwa hiyo, hakuna probability ya US ku join directly hii vita, ingeweza kuingia mazima endapo kama Iran ingeonesha sign of weakness, ila resilience ya Iran imewatisha wakubwa wa NATO, unaweza kusema hivo.
Kwani wewe ndiye msemaji wa serikali ya Marekani? au unadhani zile ndege kubwa za kivita zinazo safiri umbali mrefu za Marekani,ni kwanini zimesogezwa kwenye Base yao wamarekani iliyopo visiwa vya Diego Gasia?
 
Ulaya hawataki kabisa US kuingia vita ya moja kwa moja
Huyu mzee asitupangie mambo ya kufanya
Uchumi utaporomoka sana duniani
Na pia wakiingia vita hii
Makombora ya Iran yanafika had Ulaya kwa hiyo huyu sio wa mchezo
Kiduku,Putin na Mchina wako upande wa Muajemi

Hakuna anaetaka vita ya tatu
Israel atulie tu sasa
Kuisambaza Iran na kusema democracy itakuja kwao ni kujidanganya

Kwani makundi yatazaliwa kama Iraq ile na watauwana sana
 
Israel bado ina turufu kubwa katika vita hivi ambayo ni kuwaua viongozi wakuu wa Iran uwezo ambao wanao sana na ikitokea hilo itabadilisha kabisa mwenendo wa mambo.

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa sana ya wananchi wa Iran wamechoka kabisa na utawala huu wa sasa na wangependa kuona mabadiliko ya kiutawala yakifanyika nchini Iran.

Viongozi hao wakilengwa na kuuliwa hakuna uongozi mwingine utakaokuja na kuendeleza hayahaya yanayoendelea sasa.
Hakuna muiran aliechoka na utawara wa sasa wa Iran, hizo unazoleta wewe ni propaganda za kimagharibi, jibidishe kutafuta ukweli na ukweli uo usitegemee kuupata kupitia vyombo vya hbr vya kimagharibi bro.
 
Usipinge Kwa hoja nyepesi,ukweli ni kwamba utawala wa Iran,Kuna mambo yanayolalamikiwa na wananchi mfano ukatili wa Police wa maadili,imekuwa ni kero,wamekuwa wakitoa adhabu ambazo hazina uwiano na kosa, mfano unakuta mtu hajavaa hijab, halafu unampa adhabu ya kummaliza
 
Siku tatu zilizopita ilionekana kwamba US angeingia vitani, ila kwa hali ilivo sasa hiyo option inaenda ikipotea. Atachofanya US kuipa silaha Israel lakini sio direct involvement.

Kuna jambo limemuogopesha US kuingia kichwa kichwa, na hapo ni baada ya Iran kupiga Hypersonic bomb na pia intensity ya mashambulizi ya Iran kule Israel ni kama inazidi kuwafikirisha US kutokana na Iron Dome kuonekana kuelemewa kazi.

Wakiingia vitani US, maana yake zile bases zote za US middle East zitakuwa under attack, kitu ambacho kitawalazimu US kufanya land invasion ambayo ni vita kamili.

Sasa kulingana na experience yao ya Afghanstan, kule Iran land invasion itakuwa very costful kwa US na kuna hatari ya wao kushindwa kufanikisha malengo yao.

Kuingia kwenye vita kamili na Iran, ni jambo ambalo US administration hailitaki kwa sasa ukizingatia ya kwamba Federal Debt ipo katika record high 37 Trillion na kuingia vitani maana yake itawabidi deni liendelee kuwa kubwa zaidi, kitu ambacho kinaweza break american economy na kusababisha dollar iweze ku crash.

Lakini kuna suala lingine tata, nalo ni, Russia na China. Mpaka sasa inaonekana wapo kimya strategically, na inaonekana wanajipanga kimya kimya kuona ikiwa US atajiingiza vitani ili nao wa declare sides. Na inapojiingiza Russia dhidi ya Marekani, tutashughudia vita ya tofauti kabisa ukifananisha na Ukraine.

Kwa hiyo, hakuna probability ya US ku join directly hii vita, ingeweza kuingia mazima endapo kama Iran ingeonesha sign of weakness, ila resilience ya Iran imewatisha wakubwa wa NATO, unaweza kusema hivo.
Maneno yako ni 💯

View: https://youtube.com/shorts/TJfwcq5pLYk?si=E74zqxjDT6fW11oU
 
Kauli za Putin
. Iran anapambana na tunaopambana nao
. regime change haikubaliki Iran

Zina ujumbe ndani yake
-Kaishia kutoa kauli,then nini atafanya? Subiri hadi afanye
- influence ya Russia world wide ni kiasi gani? Ana economy ya kutosha compared to USA?
 
Kwani mgogoro umefika wapi hadi afanye lolote?..hili ni suala la silaha na intelijensia siyo ushawishi wa kiuchumi,china hana ushawishi wa kiuchumi?
 
Back
Top Bottom