Kuna siku utakutana na Mungu ukiwa peke yako

Hoja yako ina nguvu kama tukikubali kwamba Mungu mwenye uwezo na upendo wote hana sababu yoyote ya kuruhusu uovu. Lakini hapo ndipo mjadala ulipo: kuwepo kwa uovu hakuthibitishi moja kwa moja kutokuwepo kwa Mungu; kunahitaji kwanza kuthibitisha kwamba hakuna sababu yenye mantiki ambayo Mungu angeweza kuwa nayo ya kuuruhusu. Hivyo umeonyesha tatizo la uovu, si uthibitisho wa mwisho kwamba Mungu hayupo.
 
Umeshindwa kuelewa, au huna kabisa uwezo wa kuelewa, au unabisha kwa ligi tu.

Uovu kuwapo ulimwenguni una contradict sifa za Mungu. Hii ni contradiction ya core characteristic za Mungu si suala superficial tu.

Nimeeleza kirefu kwamba nimekuonesha kuwa sababu yoyote ambayo Mungu angeweza kuwa nayo ya kuuruhusu uovu ina contradict sifa zake za uungu, ujuzi wa yote, uweza wa yote na upendo wote.

Ngoja niweke mjadala huu katika Euclidean geometry labda utaeleweka zaidi.

Yani katika Euclidean geometry ukishakubali na kuthibitisha hili ni duara, kukubali na kuthibitisha tu kuwa hili ni duara kumesha contradict uwezekano wa hilo duara kuwa pembetatu, kwa sababu sifa za duara zina contradict sifa za pembetatu.

Duara lina nyuzi 360, pembetatu ina nyuzi 180.

Duara halina pembe, pembetatu ina pembe tatu.

Sasa, wewe unachosema hapo ni kwamba, sifa za duara ku contradict duara hilo hilo kuwa pembetatu kwa wakati huohuo si uthibitisho kwamba hakuna duara ambalo hapo hapo ni pembetatu.
 
Nimekuelewa vizuri. Lakini tofauti iko kwenye hatua moja: contradiction unayoonyesha inategemea premise kwamba Mungu mwenye sifa hizo hawezi kabisa kuwa na sababu yoyote ya kuruhusu uovu. Hilo ndilo linalohitaji kuthibitishwa, si kuchukuliwa kama hitimisho.

Kwa hiyo hoja yako inaonyesha changamoto kubwa kwa dhana ya Mungu huyo, lakini bado si contradiction ya kimantiki mpaka premise hiyo ithibitishwe. Hapo ndipo tunatofautiana.
 
Umejuaje tutakutana na Mungu?🤔

Unajua hayo masuala ni 50/50

Who knows? Labda after death ndiyo the end, the end of you and your existence.
Ni kweli, hakuna mwanadamu aliye na uhakika wa moja kwa moja kuhusu yatakayotokea baada ya kifo. Ndiyo maana tunaita suala hili imani, si jambo tuliloliona kwa macho.


Lakini kutokuwa na uhakika hakuthibitishi kwamba baada ya kifo hakuna chochote—ni swali ambalo kila mtu anapaswa kulichunguza kwa mtazamo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…