MKuu Nimeanza kupractise Numerologists au kusoma Numerologists Mwaka 1998 wakati nimemaliza Medical studies..(First Degree Ya Medical "MD")
Sijawahi kubadilika na kuwa corn I just Love the numbers na jinsi zinavyocheza na energy na frequency..
Sikushangai Hata Galileo Alipingwa sana Aliposema Dunia Inazunguka Jua..
Waliona kwao ni idea mpya na Kama Uongo scam au cult tu..
Lakini ilikuwa Kuthibitka yuko sahihi miaka mingi baadaye..
Watu Kama pythgoras na ramanujan ni wanasanyansi wa Kimahesabu Waliowahi kuwepo Duniani Na walikuwa Numerologists je waliwahi kuwa con artist..
Tusikariri maisha
Acha mambo yako basi.
Mimi ni mvuvi lakini ninaelewa namba kama nilivyofundishwa na mwalimu wangu wa primary na sijasahau hadi leo.
Nakushangaa ujue Mr Scientist.
Numerology haina mashiko yoyote.
1. Inawezekana vipi scientist kama wewe kuamini kitu ambacho HAKIPO kinaweza kuathiri maisha ya mwanadamu?
Au hufahamu namba kwa uhalisia hazipo?
Namba hazipo sehemu yoyote ile zaidi ya kwenye mawazo yetu.
Nikuulize Mr scientits. Je, nikisema kuna sita kwenye hiyo meza mbele yako, hiyo itakuwa na maana yoyote?
Hapana, kwasababu namba 6 haina maana yoyote na pia haipo mpaka niiassociate na kitu mfano kuna machungwa 6 kwenye meza. Sisi wanadamu tuna AKILI tunafahamu namna yakuelezea idadi ya vitu na kwa maana hiyo tunatumia namba.
2. Namba inategemea unatumia system gani. Kama unatumia decimal system basi tutatumia base 10 lakini ukiingia kwenye binary system inakuwa kitu kingine vilevile kwenye octal system. Inategemea sana.
3. Nasema soon utageuka scam artist kwasababu unatoka flawed arguments na unajua kabisa vichwa vibovu vitaamini hii dunia yetu inatawaliwa na namba na kila kitu duniani na kila namba inga nguvu blah blah blah.
4. Namba kama namba haina nguvu yoyote. Point yakurudi nayo nyumbani leo ni uliwengu wetu huu unatawaliwa na sheria za kihesabu na si namba kama namba kama unavyojaribu kusema Mr Doctor.
5. Tena kwasababu unadai hapa wewe ni scientist ungefahamu jinsi unavyoenda ndani zaidi katika mathematics namba zinakuwa replaced na variables.
6. Kwa maana rahisi hakuna namba yenye nguvu zaidi ya nyingine au uspecial wowote ule Mr Doctor.