Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

Ukifa inaende hivyo hivyo kwa watakaokuwa hai huko mbele si ndio? Hata miaka 2000 mingine, 5000, 10,000 haijalishi.

NJOO KWA YESU UUPOKEE WOKOVU. Wokovu unapatikana bure kabisa!

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Kuna taarifa za kushangaza huko USA inasemekana mwisho wa Dunia (doomsday) ni karibu mno na kizazi hiki kitashuhudia Yesu anarudi stay tuned kwa ushahidi.
Hizo taarifa za kushangaza ni zipi? Na chanzo chake ni kipi? Na ni kwa nini isemekane badala ya kutoa ushuhuda wako hapa. Kwa nini USA na sio Djibut, Eswatini au Mongolia, au Equatorial Guinea kule kwa Baltasar Egonga?
 
Kuna taarifa za kushangaza huko USA inasemekana mwisho wa Dunia (doomsday) ni karibu mno na kizazi hiki kitashuhudia Yesu anarudi stay tuned kwa ushahidi.
Sio tetesi! ni kwamba tuko karibu na mwisho kabisa. Najua humu wengi wanachojua ni kubeza. Kifupi tu ni kuwa;
1) Ukigawanya nyakati ambazo Mungu anashughulika na wanadamu, hizi za leo ni nyakati za mwisho lakini zilianza zamani tangu baada ya sikukuu ya Pentekoste. Around 33

2) Miaka hii tuliyonayo ni siku za mwisho mwisho kabisa katika nyakati za mwisho

3) Dalili kubwa ya siku hizi zilianzia kuundwa kwa taifa la Israeli 1948

4) Tukio linalofuata ni unyakuo, Katika hili Yesu hatakanyaga dunia, ataishia mawinguni na kanisa litanyakuliwa

5) Kitakachofuatia ni dhiki kuu, utawala wa mpinga Kristo na dunia yenye utaratibu mpya (NWO)
 
Acha kujidanganya mkuu, Yesu hawez kurudi.

Tena Kwa wayahudi tulionao sahivi, watampiga Yesu makombora mpk achakae.

Bora kina Pilato walimhurumia wakamgonga misumari nchi 6 mikonini na miguuni Ila wakauacha mwili wake angalau unatambulika ukiutizama

Ila Kina Netanyau hawacheki na kima, wataulipua,kuuchakaza na kuufukia na vifusi vya Gaza.
Hakika na hawatamvalisha nepi tena.SAA HII NI BIKINII
 
Lisemwalo lipo (na yalishasemwa kwenye vitabu)!
Kama halipo linakuja (Yesu atakuja kama mwizi hakuna aijuaye siku wala saa)!
Dalili alizosema,Vita,Magomjwa yasiyo na dawa,Njaa,kukithiri kwa maovu(Uzinzi,Ulawiti na Usagaji,Mauaji,Ufisadi,Wizi,nk ),Matetemeko ya nchi mahali mahali (mabadiliko ya tabia nchi),Habari za kutisha,nk
Kifanyike kipi?
Ni Kujiandaa wakati wote!
Tubu dhambi zote na kuacha!
Sasa akija si tunamuua mwizi wa nini sisi.
 
Jibu swali basi mkuu.

YESU ajapo wakati wa unyakuo kuna watakatifu watakaokuwa hai atawanyakua (japo hawatawatangulia wale waliokwishakulala mauti). Hao watakaokuwa hai inawezekana ni Mimi ama ni mwingine.

kwani wewe umekwama wapi boss
 
YESU ajapo wakati wa unyakuo kuna watakatifu watakaokuwa hai atawanyakua (japo hawatawatangulia wale waliokwishakulala mauti). Hao watakaokuwa hai inawezekana ni Mimi ama ni mwingine.
Hapa umejibu swali, kwamba watakaokutwa hai. Meaning hilo tukio kama lipo linaweza kuwa hata miaka 100,000 ijayo au b5 au 1,000 au siku 1. Kila la heri.
kwani wewe umekwama wapi boss
Sijakwama popote, nilikuuliza swali ukaanza kusisitiza wokovu badala ya kujibu swali.
 
Acha vitisho uchwara mkuu,
Yesu Hana jipya, keshajifia zake uko.
Keshageuka mzimu Kama mabibi na mababu zetu
Ajabu ni kwamba aliyeoza jina lake linatoa pepo na kuziseta nguvu za giza. Unaonekana unasikia Tu kuhusu Yesu but huna ushuhuda nae!
 
Kuna taarifa za kushangaza huko USA inasemekana mwisho wa Dunia (doomsday) ni karibu mno na kizazi hiki kitashuhudia Yesu anarudi stay tuned kwa ushahidi.
Akirudi nishtue ndugu,huyu mwamba nimesikia mastory yake sana.
 
Rabbi wewe si leo umetuandukia ile ndoto yako murua ya Yesu kuwa mawingini na Jeshi la watakatifi na malaika akiwa njiani kuja? Hapa unataka kutuambia ile ndoto yako nzuri ilikuwa ya shibe ya mahagwe Ya Mbeya?? yaani uataka kutuambia tusubiri tena hadi baada ya miaka elfu moja na ushee tena?
Miaka elfu Moja ni baada ya WATAKATIFU kunyakuliwa.

Mfano Unyakuo ulifanyika Leo, wataondoka WATAKATIFU pekee na kubaki wasiojiandaa, ndipo watapitia mateso MAKALI wakati huo WATAKATIFU wakipitia karamu.

Halafu ujue Ile haikuwa ndoto, ni halisi nilikuwa katika Roho.
 
Back
Top Bottom