Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Washua wengi wameondoka hayo maeneo na kugeuza nyumba zao kuwa sehemu za biashara au utakuta wamebakia watoto ambao na wao wanavuta mkwanja kupitia nyumba za urithi then unakuta wanaishi huko mbweni, na maeneo mengine
Masaki, Obey, Mikocheni huko ni kwa senior citizens & elites waliokamata pesa ndefu kuanzia awamu ya kwanza, pili na kidogo ya tatu.. Hawa wengi kwa sasa washakuwa wazee au washatoka nje ya uringo wa mapambano. Wale wazee wengine wameamua either kwenda kujenga nyumba za kawaida nje ya miji ili wapate utulivu au kurudi kabisa kijijini kwenda kumalizia maisha huko wakati huo hizi nyumba walizoacha kwenye hayo maeneo either wameuza ama zinabaki kama collateral kwenye banks (ndio maana mnaona nyumba zimebaki na walinzi na mahouse maids tu). Mtu atakayenunua nyumba Masaki kwa 700m mpaka 1b huko huyu anakuwa amenunua kwa ajili ya biashara, so ni either abomoe ajenge ghorofa kwa ajili ya appartments na ofisi au aweke kitu chochote kitachorudisha pesa yake (hotel, club n.k)

Elites & Senior citizens walioanza kukamata pesa awamu ya 4 na ya 5 na kuendelea ndio hawa wanajenga Ununio, Bahari Beach, Mbweni n.k na ndio maana hayo maeneo sasahivi ni hot cakes na ndio maana mfanano wake ndio kama ule wa Masaki na Obey za enzi hizo..
 
Mabadiliko haya yanatokana na kukua kwa mji pamoja na ongezeko la watu mjini. Nakubaliana na wote kuwa Masaki imebadilika sana lakini si Masaki peke yake hata maeneo mengine nayo yamebadilika kutokana na kukua kwa mji

Sinza leo badala ya makazi imegeuka kuwa sehemu ya biashara kama Kariakoo. Maeneo ya Kimara ambako kulikuwa ni nje ya mji watu walikuwa wanaenda kule kujenga makazi na ufugaji leo hii ni makazi tena overpopulated. Mji umesogea mpaka mkoa wa Pwani Bagamoyo na Kibaha imeungana na DSM
 
Kwanza kabisa naomba mnisamehe kama Uzi wangu unaofanania na kudhihaki ila hii si shabaha yangu!Shabaha yangu kubwa ni kutoa taswira ya namna mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya maeneo husika yalivyotofautiana sana na mpango wa awali wa matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kabla;
Enzi hizo wakati naishi mimi:

Masaki ilikuwa ni Residential Area pekee huwezi kuta ofisi yoyote iwe ya serikali au taasisi binafsi ikifanya shughuli zake maeneo hayo.

Miaka hiyo Masaki huwezi kuta jengo lenye urefu wa ghorofa zaidi ya ghorofa tatu kwa uchache na upekee wake utakutana na mazingira ya namna hiyo kwny maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya flats yakiwemo maeneo kama ya TIB,THB na kule Harbors.

Masaki ya wakati huo wahudumu walikuwa hawarudi makwao zaidi ya kuishi kwenye nyumba za servants zilizokuwa nyuma ya nyumba kubwa za maboss wao

Wakati huo Masaki huwezi kuta watu wakiwa wamezagaa zagaa hovyo asilimia kubwa kwenye mtaa husika watu tulikuwa tukifahamiana kwa sura hata kama tulikuwa hatusalimiani.

Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.

Huu ujinga ulikuwa unanikera na kunanifurahisha
"watu tulikuwa tukifahamiana kwa sura hata kama tulikuwa hatusalimiani".
 
Iko hivi miji inatanuka masaki ya zamani au sinza ya zamani au kinondoni ya zamani sio ya sasa hiviipo hivi watu wanahamia na watu wanaondoka kwaiyo miaka 20 ijayo masaki itakuwa ya kawaida kama sinza ya zamani kwaiyo mji mwingine utaibuka kuwa wakishua maana siku hizi wengi wanaamia kigamboni uko kuna mijengo ya maana au bagamoyo siku hizi mjini kuna makelele sana
Kigamboni kuna mijengo ya kistaa ajabu 🤣 halafu tulivuuu! Ila ushenzini still kupo kupo. Kuvuka vuka maji ndio kitu kimenishinda kuishi kisiwa cha Kigamboni
 
Tanzania hatuna mipango Miji sikuhizi hamna tofauti ya makazi ya watu,soko, makazi ya watu yamezungukwa na bar na Kila mtu kwenye nyumba yake anajenga fremu tu. In short sikuhizi makazi mazuri ya watu hamna, na hata aliyeanzisha wazo la fremu na wote kuiga sijui nani Yani fremu nyingi kuliko wateja
Hahahah hili kwa kweli hata mimi sielewi inabidi tuanzishe uzi kabisa tuulizane. Kwanini kila mtu akijenga nyumba kama ana eneo anaweka fremu mbele ya nyumba? In most cases nyingi zinakuwa useless sababu hamna wapangaji.
 
Miaka ya zamani 80-90s ukisema unakaa Masaki ,Oysterbay,Upanga,Posta au Mikocheni ulikuwa unaogopeka......Ila kwasasa ukisema unakaa Mbweni(Zile Plots elfu 20 za Mkapa) unaogopeka....Masaki/Oysterbay wanakaa walinzi/wfanyakazi wa ndani tu siku hizi.
😀 Wenyeji walishakufa, watoto wao wako Ulaya nyumba zinafanyiwa upkeep tu na kupangishwa kwa wazungu wa ubalozini.
 
Hahahah hili kwa kweli hata mimi sielewi inabidi tuanzishe uzi kabisa tuulizane. Kwanini kila mtu akijenga nyumba kama ana eneo anaweka fremu mbele ya nyumba? In most cases nyingi zinakuwa useless sababu hamna wapangaji.
Yani na vile watanzania tunapenda kuiga iga mambo,honestly nyumba ya kuishi siwezi kuweka ma fremu hovyo ilichangia na maeneo yenyewe Huwa finyu kweli yani. Mbona nchi za wenzetu zimepangwa na maeneo kutengwa ka ni soko, makazi huku kwetu vurugu Kila corner imekuwa ka uchafu
 
Utabiri wangu, Dsm ya kishua ya miaka ijayo itakuwa Kigamboni, watu wanachelewa kujua tu.
Niko na wewe, Kigamboni inakuwa vizuri sana eneo kubwa sana liko surveyed serikali ingetia nguvu kidogo tu kigamboni nzima ingekuwa imepimwa kwanza kabisa matajiri wakubwa wanaojielewa wamechukua maeneo makubwa mahekari kwa mahekari na wanayaendeleza kwa mikakati na sio holela holela,siku Kigamboni ikipata barabara za lami za uhakika tutasahau kbs njia ya kuelekea Bagamoyo! Kigamboni ina kila sifa ya kuwa juu.
 
Kwanza kabisa naomba mnisamehe kama Uzi wangu unaofanania na kudhihaki ila hii si shabaha yangu!Shabaha yangu kubwa ni kutoa taswira ya namna mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya maeneo husika yalivyotofautiana sana na mpango wa awali wa matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kabla;
Enzi hizo wakati naishi mimi:

Masaki ilikuwa ni Residential Area pekee huwezi kuta ofisi yoyote iwe ya serikali au taasisi binafsi ikifanya shughuli zake maeneo hayo.

Miaka hiyo Masaki huwezi kuta jengo lenye urefu wa ghorofa zaidi ya ghorofa tatu kwa uchache na upekee wake utakutana na mazingira ya namna hiyo kwny maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya flats yakiwemo maeneo kama ya TIB,THB na kule Harbors.

Masaki ya wakati huo wahudumu walikuwa hawarudi makwao zaidi ya kuishi kwenye nyumba za servants zilizokuwa nyuma ya nyumba kubwa za maboss wao

Wakati huo Masaki huwezi kuta watu wakiwa wamezagaa zagaa hovyo asilimia kubwa kwenye mtaa husika watu tulikuwa tukifahamiana kwa sura hata kama tulikuwa hatusalimiani.

Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.
Masaki imekua ni ya kipuuzi sana. Masaki sasa hivi kwa population mitaani na mishemishe imekua kama motaa ya Kinondoni kasoro ubora wa nyumba.
Maghorofa yamerufushwa kama Posta, tatizo ni hela kuingia mikononi mwa waliokosa exposure.
 
Back
Top Bottom