Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Hahahaha kbs noma sana!neno lilokuwa likitumika ni hovyo sana utaskia eti "Wanafugwa" [emoji23]
Saa tatu usiku watoto wa uswaz tuko nje,washkaji zetu watoto wa kishuwa wakisikia hivyo wanashangaa dah
Usiku nyie mko nje [emoji1]
Sema tuliwapaga mchongo wawe wanacheza na wafanya kazi zao
Beki tatu na mlinzi wa getini

Ova
 
Trend ya miji ya Kibongo ni kwamba pesa ikifumuka watu wanaanzisha ka-mji ka kishua wanafunga kuta na mageti makali. Watoto wanalelewa kishua kila kitu kipo.

Wazazi Wakizeeka na kuaga dunia watoto wanaishi kwenye majumba mazuri lakini ukute hawana kipato.

Mwisho wa siku wanauza majumba au wanaishi humo wakiendesha biashara haramu nao wanaaga dunia nyumba zinakaliwa na wajomba na mashamgazi ndo hao mnaowaona Masaki.
Noma sana!
 
Hahaha

Wengine sisi tulikulia uswazi na watoto wa kishuwa tulikuwa tunawaleta uswazi wanakuja na kujichanganya
So ikawa wao kuna mambo walikuwa wanajifunza kwetu na sisi tunajifunza makwao
Sema watoto wa kishuwa wengi ilikuwa kupewa rahusa ya kutoka makwao ndiyo ilikuwa mtihani
Watoto wa kishuwa wengi mwisho ilikuwa saa 12 wako ndani
Sasa hapo ndiyo ikaanzaga mishe za wao kutoroka,na wengine kuiba magari ya baba zao

Ova
Safi sana! Vizuri kuwachangamsha
 
Hiyo inaitwa land use succession🙏 mabadiliko katika matumizi ya Ardhi katika miongo ,kutokana na mabadiliko ya kiuchumi wa nchi,Ina mazuri na mabaya yake hasa kwa nchi maskin Kama Tanzania,ambapo bajeti ya kuregulate hayo mabadiliko haipo,so raia wanajiamulia mabadiliko hayo yaende vipi bila kufuata mastaplan ya mji/jiji husika.
 
Wa
Mbona TMK kuna maeneo yako poa sana especially Chang'ombe!
Walikuwa wanakuja maduka mawili wanasema mbona lami yenu humu mitaani imechakaa sio Kama Chole road?ukiwaambie tukanywe soda TTC club wanasema Kuna mavumbi sio Kama Slipway nyieeeeeeeee 🤣🤣🤣🤣sijui na vitoto vya siku hizi vinajidai hivyohivyo
 
Ishu sio maghorofa ya makazi.

Ishu ni pamoja na maghorofa ya ofisi.

Kingine ni ukosefu wa mipango.

Ingewezekana ikawepo mitaa maalum ya high rising blocks na kwingineko kukawa nyumba za chini ...sio hapa nyumba ya chini ..jirani ghorofa la maofisi
[emoji2956]
 
In a very serious note,Dar ni Tatizo kwenye issue ya makazi holela...yaani mtu anaamua anajenga chochote popote
Tena ajenge hata level ya kiuno na hata akitelekeza miaka ishirini eneo hilo hakuna wa kumuuliza watalamu wa sensa mtuambie ni majengo mangapi hayakamilika?! na je kuna matumaini ya kukamilika kweli?!
 
Tena ajenge hata level ya kiuno na hata akitelekeza miaka ishirini eneo hilo hakuna wa kumuuliza watalamu wa sensa mtuambie ni majengo mangapi hayakamilika?! na je kuna matumaini ya kukamilika kweli?!
Hii nchi bado inahitaji kurekebishwa mifumo ya kiutendaji,unless otherwise tutaendelea kuona mapya Kila siku na hao wanajiita wataalamu hawana Cha kutusaidia
 
Nimetia timu hapa kuona labda nitawapata street mates wangu maana hiyo ni mitaa yangu .

Kitambo sana Masaki sio sasa kuna mpaka boda boda , mara hostel za wanafunzi wa Muhimbili mh sio patamu tena .

Kwasasa ni uswazi na tunaowapangisha ni maisha ya kawaida ndiyo maana kodi ikikaribia kuisha tunakuja walau wapangaji watastuka wakumbuke kulipa maana kwenye simu janja nyingi.
 
Na wale wazee waliyokuja kushtuka kuingia ubia ya maeneo yao kidogo ndiyo walijiokoa,maana kuna familia zingine zilikuwa zinakaa kule badaye walitoka kwenda sehemu nyingine walikuja kupigika hasa

Ova
Kweli kabisa maana unaingia kwenye flat na mashuka tu kila kitu unakikuta wengine wakajisahau
 
Tulikuwa tunatoka mabibo,tunapiga polish yani tunajifanya wasanii wa bongo fleva kisha tunazama masaki na Coco beach kwenda kuwinda watoto wa geti kali duh sitasahau siku tumetolewa nduki kwa bastola na wanangu.
Maana manzi alinambia kesho tisa kamili nkifika nigonge geti atakuwepo getini tusepe coco tukale upopo , aisee niko na wana tumetupia full unyunyu mapiko dah alitoka mshua akatusalimia kwa upoole kisha akatoa ndude(tulikuwa tunaijua maana tulikwishaiona kwenye movie za kihindi) duh ndukii kila mtu na njia yake tukakutana posta mida ya saa moja hoi.
Hakuna simu hapo
 
Hii nchi bado inahitaji kurekebishwa mifumo ya kiutendaji,unless otherwise tutaendelea kuona mapya Kila siku na hao wanajiita wataalamu hawana Cha kutusaidia
Dada kuna nyumba ambazo hazitoisha kujengwa forever lazima tufikie kwenye makubaliano nyumba ijengwe kwa miaka mingapi kwa level yetu ya maisha na iwe kwny hatua gani?!usipofikia malengo vunja mpk utakapoweza kumudu!inasikitisha baadhi ya watalamu wetu wapo kwa ajili ya kuuza viwanja tu. Ni huzuni kubwa mno.
 
Back
Top Bottom