fimboyaasali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 8,617
- 8,244
Usidanganywe na hoja za hivi japo wote waliotajwa siwajui,hii inaweza kuwa uongo mtupuSerikali Ichukue hatua haraka
Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usidanganywe na hoja za hivi japo wote waliotajwa siwajui,hii inaweza kuwa uongo mtupuSerikali Ichukue hatua haraka
Naam mentality ya wakimwaga mboga mimi namwaga ugali mwisho wa siku itatuacha wote na njaa...,changamoto ni mfumo mbovu, angalia Sabaya alikuwa anavunja maduka ya watu na hakuna mtu wa kumgusa isipokuwa Rais pekee, hakuna kitu wewe ukipata nafasi piga pesa kaa pembeni.
Nini kimewasibu?Kuna ufisadi Mkubwa unafanyika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha (AUWSA). Ufisadu huu unafanywa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi AUWSA, Eng. Justine Rujomba kwa kushirikiana na Waziri wa Maji Ndg. Juma Aweso na Katibu Mkuu Engineer Sanga.
Kuna Mradi wa Ujenzi wa Mtandao wa Uondoaji huduma ya Majitaka Eneo la Kisongo A to Z wenye thamani ya Tzs 3.5 bilion amepewa Mkandarasi 'Tumaini Engineering' bila tenda kutangazwa huu ni ukiukwaji wa taratibu za Ununuzi pamoja na Waziri wa Maji Ndg. Aweso, Katibu Mkuu Eng. Sanga na Bodi ya AUWSA chini ya Dr. Masika kuwa na taarifa juu ya Ufisadi huu wameshindwa kuchukua hatua yoyote.
Watumishi wa AUWSA waliandika barua kwa Waziri Aweso kumtaarifu juu ya Ufisadi wa Mradi wa Majitaka wa A to Z cha kusikitisha Waziri alimpatia barua MD wa AUWSA na kumtaadharisha kukaa mbali na Technical Manager Eng. Humphrey Mwombelwa badala ya Waziri kuifanyia kazi barua yeye akamchonganisha MD na TM hivyo kumlazimisha TM kuacha kazi. Ni aibu na Kinyume cha Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Waziri kutoa taarifa za siri kwa mhusika.
Serikali ilitoa TZS 3 billion zitumike kujenga mtandao wa majisafi Longido hadi Namanga kwa kutumia Force Account, cha Kusikitisha MD wa AUWSA ameipatia kazi ya Ujenzi kampuni ya Tumaini Engineering bila kufuata taratibu za Ununuzi zabuni haikutangazwa kama taratibu zinavyotaka.
Pamoja na Serikali kuzuia Posho, Management ya AUWSA na wasimamizi wa mradi kila mwisho wa Mwaka wanajilipa posho kila Mmoja TZS 1 Million hadi 5 Million za Sikukuu ya Noeli (Christmas) huku upotevu wa Maji NRW ukiwa ni asilimia 54. Serikali ilishapiga marufuku Posho za Sikukuu.
Ofisi ya Rais, Waziri Mkuu, PCCB Makao Makuu (PCCB wa Arusha wamewekwa Mfukoni) tuna imani sana na ofisi zenu; tumeni wakaguzi huru wachunguze Ufisadi unaondelea AUWSA.
Waziri na katibu Mkuu ni wanufaikaAndaa nakala itume kwa katibu mkuu kiongozi ikulu,kama waziri ameshindwa kutatua hio changamoto
Ushauri MzuriAchana na katibu mkuu wizara,nakala ya hayo iende katibu mkuu kiongozi ikulu
Hata nyie wa kada ya chini ni mafisadi mnao waungia wateja mtandao wa maji
ukiitwa front utakuwa tayari kutoa haya maelezo
Ushaidi upo Serikali imetoa Fedha AUWSA ijengeukiitwa front utakuwa tayari kutoa haya maelezo kwa undani?
Huyu Waziri namjua vzr mamlaka nyingi za maji ameweka watu wake wa karibu sn, kimsingi mkuu hii nchi ni shamba la bibi kila mtu ale kwa urefu wa kamba ake hakuna namna maana pamejaa
Rujomba hana Sifa za Kuwa MD amepewa UKurugenzi ili kutengeneza chakula cha waziri na Katibu Mkuu , Scheme of Service ya Auwsa inataka MD, Wakuu wa Idara na Sehemu wawe na Masters ( Shaada ya Uzamili) Rujomba ni Technichian hana Masters ,maswali ya kujiuliza imekuwaje ameteuliwa kuwa MD wakati kuna wahandisi wenye Sifa ( Masters) waliomba ukurugenzi , Mfano Engineer Ezron wa Bonde la pangani ana PHD na wengine wengi.Huyu Waziri namjua vzr mamlaka nyingi za maji ameweka watu wake wa karibu sn, kimsingi mkuu hii nchi ni shamba la bibi kila mtu ale kwa urefu wa kamba ake hakuna namna maana pamejaa uozo tupu kila kona.
Mkuu hizi masters zenu hatuzitaki tunataka hata kama mtu ana certificate apewe badala ya haya makaratasi ambayo hayana faida kwetu, mhimu mtu afanye kazi kwa kufuata sheria na taratibu, kama ameenda kinyume mpelekeni mahakamani, vinginevyo itakuwa ni majungu tupu, mbona kuna watu wana PhD ni majizi?Rujomba hana Sifa za Kuwa MD amepewa UKurugenzi ili kutengeneza chakula cha waziri na Katibu Mkuu , Scheme of Service ya Auwsa inataka MD, Wakuu wa Idara na Sehemu wawe na Masters ( Shaada ya Uzamili) Rujomba ni Technichian hana Masters ,maswali ya kujiuliza imekuwaje ameteuliwa kuwa MD wakati kuna wahandisi wenye Sifa ( Masters) waliomba ukurugenzi , Mfano Engineer Ezron wa Bonde la pangani ana PHD na wengine wengi.
Kama Scheme of Service inataka MD awe na Masters ilitokeaje jina la Rujomba likafika katika panel ya interview? Nani alifanya Shortlisting ( usahili) ?
Na Je Board ya Wakurugenzi ya Auwsa chini ya Dr. Masika awakulioma ili?
Takukuru ( PCCB) mkoa wa Arusha wana Taarifa zote hizi kwanini awazifanyi kazi?
Ofisi ya Rais utumishi na Msajili wa hazina inakuwaje mnaachia Scheme of Service mliyoidhinisha inachezewa na Waziri na Dr. Masika?
Kama Scheme of Service inataka MD , wakuu wa idara wawe na Masters inakuwaje inavunjwa?
Ofisi ya Rais , Waziri Mkuu tumeni wachunguzi Mapema
kuna mambo ya ajabu sana mfano Matofali ya Kujenga Tanks za Karatu zinatoka Moshi na tofali moja Auwsa inanunua kwa Shilingi 3200. Inakuwaje tofali zinatoka Moshi? Ina maana karatu hakuna matofali? Makuyuni hakuna tofali? Arusha mjini je? Na ni sahii kununua tofali Moja kwa Shilingi 3200?
Auwsa kuna Upotevu wa Maji 54% bila aibu ikifika Chrismas Management na wasimamizi wa Miradi wanajilipa Milion mbili hadi tano za Sikukuu kwa kila Mmoja alafu wafanyakazi wa Chini ambao ndiyo engine ya taasisi wanapewa pilau na Tzs 50,000.. Hii ni dharau kubwa kwa wafanyakazi kada ya chini.
Management wanapewa 14 Milion za kununua Sofa kila Mwaka.. hizi pesa zikitumika kufanya extension ya mtandao wa Maji inatosheleza kujenga kilomita 200
Inakuwaje wakaguzi wa CAG awatoi ripoti hizi?
Angalieni hii piga piga yenu mwisho mtatutoa roho !!Rais alisema anataka kuongeza mzunguko wa pesa mtaani mlidhani anaenda kuzitupa barabarani? mzunguko wenyewe ndiyo huu watu wapiga pesa haswa kwenye miradi wanakuja kununua bia, kuhonga, kula mbuzi katoliki na mengine
Kama Serikali iliruhusu force account kutumika, mambo ya kutangaza tenda inatoka wapi? Unaelewa utaratibu wa force account vizuri?Serikali Ichukue hatua haraka
Tetetete mkuu acha watu wale kidogoAngalieni hii piga piga yenu mwisho mtatutoa roho !!
Wewe sio Lutindi kweli? Muhasibu nilisikia naye alinyimwa Mgao???Tatu, Serikali ilishapiga marufuku Posho Management ya AUWSA na Wasimamizi wa mradi Mkubwa wa Majisafi Arusha Disemba kila Mmoja anavuta Shilingi Milioni mbili hadi tano za sikukuu christmas, Pasaka wanavuta Milioni Tatu tatu kila Member wa management na wasimamizi wa miradill, Jumla ni Tzs 500 Milion zikitumika kufanya Extensiom ya Maji Arusha ni zaidi ya kilomita 200