Rujomba hana Sifa za Kuwa MD amepewa UKurugenzi ili kutengeneza chakula cha waziri na Katibu Mkuu , Scheme of Service ya Auwsa inataka MD, Wakuu wa Idara na Sehemu wawe na Masters ( Shaada ya Uzamili) Rujomba ni Technichian hana Masters ,maswali ya kujiuliza imekuwaje ameteuliwa kuwa MD wakati kuna wahandisi wenye Sifa ( Masters) waliomba ukurugenzi , Mfano Engineer Ezron wa Bonde la pangani ana PHD na wengine wengi.
Kama Scheme of Service inataka MD awe na Masters ilitokeaje jina la Rujomba likafika katika panel ya interview? Nani alifanya Shortlisting ( usahili) ?
Na Je Board ya Wakurugenzi ya Auwsa chini ya Dr. Masika awakulioma ili?
Takukuru ( PCCB) mkoa wa Arusha wana Taarifa zote hizi kwanini awazifanyi kazi?
Ofisi ya Rais utumishi na Msajili wa hazina inakuwaje mnaachia Scheme of Service mliyoidhinisha inachezewa na Waziri na Dr. Masika?
Kama Scheme of Service inataka MD , wakuu wa idara wawe na Masters inakuwaje inavunjwa?
Ofisi ya Rais , Waziri Mkuu tumeni wachunguzi Mapema
kuna mambo ya ajabu sana mfano Matofali ya Kujenga Tanks za Karatu zinatoka Moshi na tofali moja Auwsa inanunua kwa Shilingi 3200. Inakuwaje tofali zinatoka Moshi? Ina maana karatu hakuna matofali? Makuyuni hakuna tofali? Arusha mjini je? Na ni sahii kununua tofali Moja kwa Shilingi 3200?
Auwsa kuna Upotevu wa Maji 54% bila aibu ikifika Chrismas Management na wasimamizi wa Miradi wanajilipa Milion mbili hadi tano za Sikukuu kwa kila Mmoja alafu wafanyakazi wa Chini ambao ndiyo engine ya taasisi wanapewa pilau na Tzs 50,000.. Hii ni dharau kubwa kwa wafanyakazi kada ya chini.
Management wanapewa 14 Milion za kununua Sofa kila Mwaka.. hizi pesa zikitumika kufanya extension ya mtandao wa Maji inatosheleza kujenga kilomita 200
Inakuwaje wakaguzi wa CAG awatoi ripoti hizi?
Ila nadhani kwenye suala la elimu utakua unamuonea bure,kua na elimu kubwa masters au PHD sio kwamba ndio kua na uwezo wa kuongoza taasisi,hizi masters,PhD mara nyingi hua ni rubish tu,na sijui kwa nini hua zimewekwa kwenye kupima uwezo wa kuongoza,na labda nachoona kuna watu hapo wanaomuonea Wivu kwa kua wao hawajapewa huo ukurugenzi.
Sometimes kwenye maisha sio lazima ukisoma sana ndio uje kua kiongozi, kuna watu ni gifted na inatokea tu pamoja na kua wana elimu ndogo, kama Nyerere,Mwinyi,Samia, JK.
Mtu akiwa na bachelor degree safi,uwezo wa kuongoza anao,ametulia kiakili, exposure anayo,mvumilivu kwenye maamuzi,hivyo hua vinatosha, ila kibongo bongo yaani mpk mtu awe na masters ndio anaonekana ana uwezo.
Nchi hii imeongozwa na viongozi wengi wenye one degree only na nchi imetulia,Mawaziri wengi wana bachelor degree na wanaongoza wizara sembuse taasisi?
Kigezo cha elimu kubwa ndio kua na uwezo wa kuongoza ni upuuzi wa kiwango cha lami, kuna masters, Phds kibao ila ni ovyo.Masters,PHDS hizi zinatakiwa watu wawe nazo huko kwenye Academic institutions ambao ni ma lecturer wazitumie kufundishia watu huku kwenye taasisi za serikali bachelor inatosha sana,degree moja inatosha kuongoza hataa nchi km mtu uwezo anao, mtu atapata course mbili tatu za management/leadership na mambo yanaenda.
Kwenye suala la elimu hapo utakua unamuonea na madai yako yataonekana yanaongozwa na hatred ,may be kwa kutumwa au wewe mwenyewe labda mambo mengine.
Serikali mara nyingi hua uteuzi unapofanyika haujali sana hizi mnazoita masters,PhD,uprofesa ki serikali degree moja na uwezo binafsi inamtosha mtu kua kiongozi popote pale nchi hii.