Kuna Ufisadi wa kutisha Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA)

Mkurugenzi wa AUWSA jana alijitetea katika kikao cha Menejinenti kuwa Posho za Milioni mia tano wanazojilipa kipindi cha Christmas na Pasaka ni sahii , Maswali ya Msingi

Kama ni sahii kwanini Payment Voucha zinafichwa , wakaguzi wa Nje kutoka ofisi ya CAG awaonyeshwi

2. Wanatumia Vigezo gani kupanga Amount?

Tatu ni sahii Kutumia Mkopo wa Serikali kutoka AFDB kulipana Posho?

Nne kwanini Bodi ya Menejimenti ya Auwsa chini ya DR. Masika ilifichwa Juhuu ya hizi Posho?

Tano, kama bodi ilifichwa katika matumizi ya Posho ya Shilingi 500 miloni na awajagundua hadi sasa kuna sababu ya bodi kuendelea kuwepo?
 
Na huku wewe unakandamizwa na TOZO na mpaka vizazi kumi vijavyo vitakuwa vinalipa Madeni ya Mikopo iliyotokana na huu ubadhirifu, mbaya zaidi badala ya mabomba kutoa maji yanatoa hewa.

Harafu hili la kutoa hewa nadala ya maji linakera sana.Hiyo hewa inakua na pressure kubwa sana lkn maji hamna harafu bili inakuja kubwa sana….Kiseriani yote kuna shida kubwa sana ya maji….maji hayatoki kabisa lakini bili ikija ni kubwa mnoo mpaka una shangaa!
 
Menejimenti ya Auwsa ni Mandezi sana , Badala ya Kueleza Mkandarasi wa Mradi wa A to Z amepatikanaje wameamua kukabidhi TAKKURU barua za Waziri Aweso na katibu Mkuu zilizoelekeza utekelezaji wa Mradi wa A to Z kama utetezi

Maswali ya Msingi ni

1. Tumaini Engineering alipatikanaje?

2.kwanini Pesa za Mradi wa Longido Namanga alizotoa Rais Samia zimeamishiwa A to Z?

3. Menejimenti ,bodi ya Auwaa na Waziri Aweso kwanini wameruhusu
Sumu kutoka Kiwanda cha A to z kuingia katika bwawa Jipya la Majitaka lilogarimu Bilion 86 wakijua majitaka kutoka A to z yana Sumu ambazo zinaua wadudu wanaosagisha taka?

Mandezi ya Auwa badala ya Kujibu hoja wamekabidhi barua za maelekezo ya Utekelezaji mradi kutoka kwa waziri na katibu Mkuu TAKUKURU .. Barua ya waziri imeagiza utekelezaji wa mradi aikusema Tumaini Engineering apewe kazi ya ukandarasi.
 
Andiko linaweza kuwa na nia njema lakini limeandikwa kwa kutanguliza chuki, husuda na hasada,kwanza katika jambo la kawaida tu Mamlaka za Maji zina siasa zake, kuba tabia ya kushughulikiana, ila changamoto nilioiona hapa ni kumhusisha Kiongozi Mzalendo na mwenye maono alieonesha dira katika sekta hii ngumu Aweso, hiyo haitoshi anachafuliwa mpaka Katibu Mkuu ambae weledi wake kwass tunaomfahamu tangu akiwa Mwanza si wa kutia shaka hata kidogo.
Andiko limewekwa kimkakati ili viongozi hawa wapate panic wamshughulikie anae windwa hapa hapa Mhandisi Rujomba,
Kosa kubwa sana tunafanya kuwakatisha tamaa viongozi makini na wenye nia ya dhati na nchi yetu, ukitaka kujua andiko lina matatizo unawezaje kumtuhumu Waziri kuwa ameweka watu wake kwenye mamlaka za maji wakati tangu awe Waziri kamili miezi kadhaa hii hajabadili Md’s wa Mamlaka za Maji kabisa na ameendelea kufanya kazi na watu walewale wa Kamwelwe, Mbalawa na Kitila.
Ni hoja inayolikosesha credit kabisa bandiko hili kwasabaabu kama hizi za ovyo.
Unaweza kumtaftia zengwe Aweso lakn utakesha maana ni kijana asie na tamaa, anaeishi maisha ya kawaida na mnyenyekevu Mchapakazi na mwana mapinduzi katika utendaji wake.
 
Hili linatakiwa lipate jukwaa la kipekee. Hivi ina maana watalii na wananchi wa Arusha wanatumia maji ya sumu ya A to Z? Aisee hii ni hatari sana. Baada ya muda Arusha itakuwa na mazuzu na mandezi wengi sana. Hivi Mh. Mbunge anayo taarifa?
 
Mkuu umeshasema walitakiwa kujenga kwa force account, fahamu kwamba miradi ya namna hiyo ni "kanyaga twende", haizingatii kanuni za zabuni
Msimamizi anatakiwa kufanya kile anachoona ni sahihi kuokoa muda na gharama, tutampima huko mwisho wa kazi.
The end justify the means
 
Hapana. Sheria ya Manunuzi ipo wazi na haipindishi kwenye taratibu za manunuzi. Afisa Masuuli hana mamlaka ya kununua kile apendacho au kwa utaratibu aupendao. Kuna vyombo vya maamuzi na taratibu zaka hapa nagusia Bodi ya Tenda, Kamati ya Uthamini na pia manunuzi ya Taasisi hubainishwa kwenye Mpango wa Mwaka wa Manunuzi.
 
Wee mchaga bila shaka wewe ni mtumishi wa hapo! Acha kupiga kelele kamwarifu Mkuu wa mkoa kwa barua na nakala wape takukuru
Inawezekana kabisa ila wenye akili tunakuona hata bila ya kuambiwa wewe ndiye mmojawapo kati ya wale wanaofaidika na wanaolalamikiwa na huyu unayemtaja kama mchaga….vinginevyo sioni sababu ya wewe kukerwa na malalamiko ga huyu bwana hadi kufikia hatua ya kumkejeli kwa ubia wake

na badala yake kama huna nafasi ya kushughulikia malalamiko haya basi ungekaa kimya ili wenye nafasi na uwezo wa kuyashughulikia wayafanyie kazi kwa faida ya wengi.
 
Wezi wakubwa na wabambikiaji bill hawa! Iweje familia yangu ya watu watatu na mbwa mmoja kila mwezi bill inakuja kwa wastani wa Tsh. 70,000.00? Pamoja na malalamiko yangu kila mara hawajawahi hata leta fundi kujakuchunguza nini tatizo!
 
Awesu ni mpigaji Sana huwa nashangaa Sana watu wanaomsifia huyu Wazir, tatizo ndio hivyo hatuna watu Wa kuchukua hatua tutaishia kulalama tu, nchi ya ajabu sijawahi kuona
 
Ww ni chawa wa Awesu, Ni wakuja tu ndio wasiomjua huyo Wazir kwamba Ni mpigaji Hana uzalendo wowote ule
 
Ungekuwa na akili usingetoa huu uharo wako hapa! Ungekuwa na akili ungegundua huyu aliyelalamika ni mpika majungu ofisini, hajui nini kinaendelea ofisini na wala hajui taratibu za ofisi aliyopo na ni mvivu, hajui majukumu yake! Hivyo wamemuacha na kumpuuza bila kupangiwa kazi yo yote. Na hiyo ni kwa kumsaidia astaafu salama vinginevyo atafukuzwa kazi ili ale jeuri yake!
 
MD wa Auwsa Engineer Rujomba amekiuka maelekezo ya Serikali ya Kupeleka magari TAMESA kwa ajili ya Matengenezo amepeleka Magari ya Shirika Garage bubu Majengo Moshi kwa Fundi John ,
Gharama zilozotumika kukarabati magari garage bubu ni Tzs 460 Milion na ayatembei yapo yard AUWSA… yalienda Moshi yakitembea yamerudi AUWSA yakivutwa

Magari yaliyopelekwa Garage bubu kwa John ni gari No SU35236 Isuzu , Gari No SU 36603 Fodi, Gari No Su 35246 Land Cruiser na Gari No Su
36201 Nisan Patrol, SU 35253 Land Cruiser

Dr. masika na Wakaguzi nendeni idara ya Fedha
Ombeni Mafaili ya matengenezo ya haya magari yametumia zaidi ya Shilingi za Kitanzania 460 Milion na ayatembei yamepaki yard

Maswali ya Msingi
1. Kwanini magari ya Shirika yamepelekwa Garage bubu kwa Fundi John wakati kuna waraka wa Serilali wa Magari kutengeneza magari TAMESA …

2.Fundi John alipatikanaje? Walitumia Mfumo hupi wa Procurement
Kumpata?

3. Engineer Steven Msesega aligoma kupeleka magari garage bubu mkamtimua..? Kwanini mlikataa ushauri wake mkamtimua?

4. Mkamdarasi wa Tzs 120 milion wa kuweka Paving AUWSA
main office alipatikanaje?

Auwsa imegeuzwa shamba la bibi
 
Kuna Gari No SU 39976 Toyota land Cruiser Black ya Driver kimaro Alinyanganywa Techinical Manager Humphrey Mwiyombelya katika Juhudi za Kumfrustrate aondoke imebaki na Jukumu la Kununua mboga nyumbani kwa Md na
Kupokea wageni wake..

Gari hii aiendi site na aifanyi kazi za AUWSA imegeuzwa Private Car ya MD

Acheni Ujinga Mpeni Technical
manager Mpya gari aitumie kusambaza maji.

Dr. Masika wewe ni Mwenyekiti wa bodi agiza TM Mpya apewe gari yake
 
Eng Rujomba Mpatieni TM gari msiyemtaka Eng Myombela ameshaondoka ila
dhambi mliyofanya Kamwe aitaisha katika Vizazi Vyenu …Au
Mnataka kumchomoa na TM mpya ?

Gari number 39976 land Cruiser na Driver Winstom Kimaro awana majukumu katibu Mkuu Pangia gari Kazi na mpangie winston Kimaro kazi mikoa mingine ,

kesho tuma wachunguzi utakuta hii gari imepaki au hipo Soko kuu
Inanunua Nyanya za MD na Driver Wiston anazurura kwenye Yard…Ukimkosa yard Utamkuta Kantini kwa Pendo.. Hivi akuna Mamalaka yenye Upungufu wa Gari muipelele?
 
 
Kama auoni tatizo una Shida sina Muda wa kubishana na wewe Mjinga

Kesho ninaleta Ufisadi Visima 15 vyenye Fluoride Vinavyochimbwa meru vyenye thamani ya Shilingi 6 bilioni ..

Fluoride ni changamoto
Kubwa duniani WHO na Wizara ya Afya wameshatoa maelekezo ya kiwango cha Fluoride 0.5% kinachoruhusiwa , Visima vinavyochimbwa Meru vina Zaidi ya Asilimia 15% ya Fluoride wajasirimali wa Wizara ya Maji na Rujomba wamevuta pesa awajali
Meno ya wakazi wa Arusha kuoza.. Wao wanaangalia pesa kwanza..

Wakaguzi wakiwauliza wanasema watafanya Mixture huu ni uhuni.
 
Ila nadhani kwenye suala la elimu utakua unamuonea bure,kua na elimu kubwa masters au PHD sio kwamba ndio kua na uwezo wa kuongoza taasisi,hizi masters,PhD mara nyingi hua ni rubish tu,na sijui kwa nini hua zimewekwa kwenye kupima uwezo wa kuongoza,na labda nachoona kuna watu hapo wanaomuonea Wivu kwa kua wao hawajapewa huo ukurugenzi.

Sometimes kwenye maisha sio lazima ukisoma sana ndio uje kua kiongozi, kuna watu ni gifted na inatokea tu pamoja na kua wana elimu ndogo, kama Nyerere,Mwinyi,Samia, JK.

Mtu akiwa na bachelor degree safi,uwezo wa kuongoza anao,ametulia kiakili, exposure anayo,mvumilivu kwenye maamuzi,hivyo hua vinatosha, ila kibongo bongo yaani mpk mtu awe na masters ndio anaonekana ana uwezo.

Nchi hii imeongozwa na viongozi wengi wenye one degree only na nchi imetulia,Mawaziri wengi wana bachelor degree na wanaongoza wizara sembuse taasisi?

Kigezo cha elimu kubwa ndio kua na uwezo wa kuongoza ni upuuzi wa kiwango cha lami, kuna masters, Phds kibao ila ni ovyo.Masters,PHDS hizi zinatakiwa watu wawe nazo huko kwenye Academic institutions ambao ni ma lecturer wazitumie kufundishia watu huku kwenye taasisi za serikali bachelor inatosha sana,degree moja inatosha kuongoza hataa nchi km mtu uwezo anao, mtu atapata course mbili tatu za management/leadership na mambo yanaenda.

Kwenye suala la elimu hapo utakua unamuonea na madai yako yataonekana yanaongozwa na hatred ,may be kwa kutumwa au wewe mwenyewe labda mambo mengine.

Serikali mara nyingi hua uteuzi unapofanyika haujali sana hizi mnazoita masters,PhD,uprofesa ki serikali degree moja na uwezo binafsi inamtosha mtu kua kiongozi popote pale nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…