Kuna uhusiano gani? kati ya kuzaa watoto wachache na utajiri versus kuzaa watoto wengi na umasikini

Kuna uhusiano gani? kati ya kuzaa watoto wachache na utajiri versus kuzaa watoto wengi na umasikini

Kwenye kundi la kuzaa watoto wengi naomba tuwatoe wazee wetu waliozaliwa 1950's maana wao kulikuwa na mashamba ya kukidhi mahitaji

Tujadili kuhusu kizazi cha 1960's-2024's

👉Aslimia kubwa ya wengi wanaomiliki mali wanaishia kuzaa watoto maximum watatu ni
u-busy?, uoga wa kuwagombanisha watoto siku mzazi akitangulia?

👉Asilimia kubwa ya masikini wanazaa watoto wanne na kuendelea nini sababu? Ni ufahari, uzazi mzuri?,


Naomba kuwasilisha
huu ychaguzi shida kweli, sasa hii ni hoja gani ya kijinga hivi
 
Easy Just live within your means..., Na utajiri ni nini ? Hata kama ukiwa na mtoto mmoja au wawili kama huwezi kufanya obligations zako basi utakuwa masikini...

Tatizo la umasikini kwa sasa root cause wala sio individuals bali watunga Sera sababu wameshindwa kabisa kuweka Sera za watu kupata Ujira..., Hao so called masikini wamehangaika kuwapa elimu watoto (kwa kuuza kila kitu na kwenda mpaka kwenye vikoba) matokeo yake hata watabibu na waalimu (ambao ni wachache na hawatoshi) wanaishia kitaa kuuza bidhaa za mchina...

Time have change and we need to change as society..., zamani watoto walikuwa nguvu kazi ukiwa nao wengi hence watumwa (wakulima) / watafutaji wanakuwa wengi..., sasa hivi ambapo hakuna uhitaji wa nguvu kazi imekuwa vice versa

Thus tatizo la Ufukara (kutokuwepo kwa middle income, bali matajiri wachache sana na masikini wa kutupwa wengi sana) ni kutokuwa na a sustainable system ambayo ni compatible na dunia ya automation na sayansi na teknolojia...
 
Masikini anaamini watoto watamletea utajiri,watamtunza mbeleni.Tajiri anaamini atajitunza mwenyewe
 
Matajiri wengi wanaogopa kuzaa watoto wengi maana ikitokea wakiachana na wake zao watasulubishwa sana.Pia wanataman watoto wao wawe kama au zaid yao kiuchumi hivyo ili kuwamudu lazima wawe wachache.
Kwa maskini wengi wameeidhika na hawana future,wana amini uzazi wa mpango ni dhambi na ni mpango wa wazungu kuwafanya wawe tasa/ wagumba.
Pia wana imani kazi ya malezi na mafanikio ya watoto wao ni kazi ya Mungu kwakuwa alisema wazae waijaze dunia.
 
Back
Top Bottom