Kuna uhusiano gani kati ya Pesa, Umasikini na kelele

Kuna uhusiano gani kati ya Pesa, Umasikini na kelele

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Mara nyingi mahala ambapo kuna Pesa au watu wamefanikiwa huwa kuna utulivu.

Masoko ya matajiri (supermarkets na Malls) huwa ni patulivu kuliko uswahili masoko yetu.

Wanapokaa matajiri (masaki, Oysterbay, Kapripoint (mwanza) ) huwa ni patulivu kuliko kwetu uswahilini.

Maskini huwa wanakelele nyingi sana, maneno maneno hata ukifika kwenye duka au ofisi kubwa utamjua tajiri kwa utulivu. Mfano yule jamaa anayepiga promo ya magari (Doi Macehicle) na Bosi wake Issa.

Mtu yeyote akiwa hajatoboa huwa anakelele kelele ila akizipata unaona anapoa anakuwa mkinya hakurupuki.

Siasa za nchi masikini zinakelele nyingi balaa, ila kwa matajiri zinaenda softly tu kimyakimya.

Hii ni dunia nzima.

Wakuu kuna uhusiano gani kati ya Pesa/Mali umasikini na kelele.
 
Pesa na Kelele havikai nyumba moja

We hujawahi kusikia wakisema maskini akipata makalio hulia mbwata.... Pesa sabuni ya roho

Ukiwa huna hela ukipigiwa kelele unaona usumbufu na ni sawa tu, kwa sababu huna hela ila wenye hela zao kelele huwa hawataki na wanatafuta utulivu
 
Back
Top Bottom