Kuna Ukweli gani juu ya mafuta na maji ya upako?

Tukuweke kundi gani sasa.. wewe unaamini kutapika hirizi ila sio kutapika misumali. Mimi vyote naona maajabu.
Ningeona hata mtu akitapika hirizi.
Ningeamini mtu anaweza tapika rozi royce ya diamond
[emoji3][emoji3][emoji3]watu wanameza hirizi sembuse kutapika?
 
Tunamkufuru Sana mungu kutumia jina lake kudanganya watu
 
Hiv unajua
1.magonjwa
2.vifo

Ni kati ya mfumo/mpango ambao upo ili dunia iweze kwenda mbele na maisha yaendelee...endapo binadam hatokufa

Hii dunia itafika mwisho...so Alieumba vyote alijua hawa lazima wafe ..wapokezane maisha...imagine wanadam wasingekua wanakufa..

Na ndomana wanasayansi wanajaaribu kuiweka dunia kwenye equilibrium kwa kutengeneza hata magonjwa ilimrad mwanadam afe ili kubalance ecosystem...

Sabab ya maendeleo ya technolojia..mwanaadam amekua anachelewa sana kufa..so hii si sahih

Mwanadam na wanyama wengne lazima wafe ili dunia iendeleee

Kwahyo unaponambia alieyumba huo mpango tena aende kinyume kwa kuwa save tena hawa watu wasiumwe or kufa..haingii akilin

Virus.bacteria.fungi..etc...waliumbwa sio kwa bahat mbaya kaka...wapo kwa kazi maalum..ya kutuua

Nmemaliza
 
Umeongea kisayansi Zaid, ongeza nyama kidogo
 
Yesu alitumia udongo na mate akampaka kipofu akaona
Mitume wa Yesu walitumia kitambaa pia, chumvi pia na mafuta yalitumika katika ishara na uponyaji Aina tofauti tofauti.
Kanisa katoliki hutumia maji ya baraka ambayo ni maji ya chumvi ambayo walokole huita maji ya upako, kwa katoliki sio nongwa isipokuwa walokole ndio nongwa, mafuta ya upako yamekuwa yakitumika sana na kanisa katoliki kuwapata wagonjwa mbalimbali na wale wa upako wa mwisho, siku ya kipaimara kanisa katoliki na Protestant mafuta hupakwa Kama ishara ya kumpokea Roho Mtakatifu.
Walokole wamefanya modification ya codes zilizokuwa zikitumika na Wakatoliki miaka dahari, shida ya walokole wameweka bayana wakati wakatoliki ilikuwa Kama Siri ya kambi.
Hata kwa waponyaji wa kiroho hutumia chumvi kuondosha nguvu hasi mwilini kwa binadamu.

Imani sio dini
Dini Zina mambo mengi yanayokinzana na uhalisia ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wao SI ndio wanajiita manabii sijui wapakwa mafuta?
Amosi-3: 7
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

Wao wanajiita manabii, wala hawajaitwa na Bwana Mungu.
Wale manabii walioitwa na Bwana Mungu daima hufunuliwa siri.
Hao manabii wa Tanzania kwani waliwahi kufunuliwa siri gani?
 
Ni ujanja ujanja na wizi.
 
Unasadiki
 
Hapa hapana ndugu yangu,mpango wa awali haukuwa kufa ,Mungu hakutaka watu wafe au waumwe.Kulingana na Biblia kifo kilikuja baada tu ya mwanadamu kukosa.

Pia pamoja na kuwa kifo kiliingia duniani Mungu bado akataka watu waishi wakiwa na afya njema.Kuthibitisha hilo tumeona all over Injili Yesu akiponya magonjwa ya kila namna.

Suala la kusema binadamu wasipokufa duniani hapatatosha nadhani Mungu aliyeumba dunia na akataka tusife tayari alishakuwa na mpango.Kama ameweza kuumba dunia out of nothing asingekosa jibu juu ya swala hilo.
 
Viwete wanatembea vipofu wanaona
 
Kwahyo..virus..bacteria fungi na gems wengne wametoka wap...au ndo sabab ya kula tunda ndo wakaumbwa..

Au kipind cha adam na eva kabla hawajala tunda .vitu vilikua havioz nn..hahaha

Matango pori ni meng kuliko ukwwl halis....

Mungu wa kwel anatuangalia anasema hiiiiiiiiiii wamedanganywa watu wangu

"Ulivyoongea haviko logicaly correct mkuu..."
 
Sijajua hapo sasa unachobishia wewe ni kipi,ni kwamba Bible imedanganya au mimi sijaelewa inasema nini?
You can't lecture me kuhusiana na Logic,i am well verse in all three laws of logic na katika post zangu nimetumia Law of non contradiction if you have noticed. Usijaribu kuweka limit ya uelewa wako ukataka kusema its Logic.Thats not true.

What i said is simply biblical.
 
Hizo 'Mafuta' zinkaguliwa na TBS??
 
Upo vizuri, nguvu za kiroho kwa mtu yeye kama yeye ndo zimefichwa ila mtu mwenyewe akizijua akatumia kweli zinatenda na hakuna haja ya kwenda kununua hayo mafuta na vitambaa ambavyo mtu hajui yana nguvu za Mungu au shetani, na ndo maana watu wanaangamia kwa kukosa maarifa ya Imani na vitendo vya kuipa nguvu hiyo Imani na yote hayo yanasabishwa na kuzaa hovyo au kutokujua umuhimu wa kuleta kiumbe dunia na kukifanya kuwa na nguvu za kiroho tangu tumboni mwa mama na makuzi yake na kuelekezwa nini ukitumia katika Imani unavunja nguvu mbaya ndo maana hayo mafuta na vitambaa yanapata wafuasi wengi maana maarifa ya kiroho hasa Yale mazuri ya Mungu watu wameyapa kisogo kwa kujua ama kutokujua na kufanya Imani ihamie kwa mitume na siyo kwa Mungu aliyeifanya mbingu na dunia.
 
Ongeza nyama kidogo kwenye matanur ya kichaawi
Ngoja nikusaidie Ili upate nguvu za kiroho ambazo zipo mbili za kishetani au Mungu lazima wewe kama mhusika uwekwe wakifu au kufanyiwa matambiko ila yaliyo na nguvu unatakiwa ufanyiwe unapozaliwa Sasa ikitokea huna hizo nguvu za kiroho na ukashindwa kujifanyia mwenyewe ndo Kuna watu wametengeneza vitu vyao kwa nguvu wanazojua wao Ili utumie upate nafuu ya muda ila shida hazitaisha maana wewe kama wewe hujawekwa chini ya uangalizi wowote wa kiroho.
 
Tatizo lililopo tumemwekea Mungu mipaka watu weng wanaamini Mungu anaweza kuponya Homa Malaria na magonjwa madogo madogo nasio kansa ,Ukimwi ndio maana zikitokea shuhuda kama hzo inakuwa ngumu kusadiki lakin Mungu anaweza kufanya mambo makubwa katika maisha yako pindi unaposadiki
Kaka watu wanapona kbsa cha msimgi n Iman tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…