Kuna ulazima hayo mashindano ya Quran yafanyike Mkapa Stadium? Siku ya mchezo Simba vs Orlando!?

Kuna ulazima hayo mashindano ya Quran yafanyike Mkapa Stadium? Siku ya mchezo Simba vs Orlando!?

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Tunajua sote jinsi mchezo huu ulivyo muhimu kwa Simba na Taifa kwa ujumla, ndio wa kwanza katika historia ya Nchi yetu kutumia teknolojia ya usaidizi wa Video kwa Mwamuzi (VAR).

Zaidi ya hayo Sheria za CAF zinataka uwanja kuwa wazi angalau saa 72 kabla ya mchezo.

Pamoja na kwamba Wanasema saa 7 kamili hao washindani wa Quran watatolewa kwa usaidizi wa Polisi...

Lakini naona kabisa hapa kuna lawama zinaenda kutengenezwa sisi Waswahili tunajijua katika kutunza muda.

Lakini vipi kama mtu akaingia then akagoma kutoka ili aangalie mechi?

Lakini vipi kama hayo mashindano yakachelewa kwisha baada ya saa 7?

Ndio maana nauliza kuna ulazima haya mashindano kufanyika Lupaso?

N.B
Sina nia ya kukashifu Dini ya mtu.

Zaidi soma hapa..

 
Mtu mmoja huko Twitter akatweet hizi dini mbili zina kutafutiana na kuzimana Kiki km diamond na harmonize

Wakristo wakati wanasherekea sikukuu Yao ya pasaka, waislamu wanakuja kuizima Kwa mashindano ya Qur'an

Nikacheka sn..Ila tungekuwa na viwanja zaidi ya kimoja vyenye hadhi ya mkapa hii ratiba isingeingiliana

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Hayo mashindano ya Quran ni ya msingi kuliko mchezo wa mpira, ni jambo jema kuliko hata maadhimisho ya kitaifa yanayofanyika hapo.Takbiiiir

Binafsi ni mkatoliki kindaki ndaki lakini napingana na mtoa mada, huwezi kulinganisha mchezo na jambo jema linalomhusisha Mwenyezi Mungu na kuwaongoza watu ktk njia ya haki na unyoofu.
Tumsifu yesu kristo...
Kanisa la kisinodi.....
Mwana kondoo ameshinda...
Salam aleykum...
 
Hayo mashindano yanakuwaga hapo miaka yote...Japo mimi siyafagilii mashindano yanayoendeshwa na huyu kishki...Labda ya huyu mama aisha sururu...

Kishki amekaa kisanii sanii sana...Na ndio maana Allaah kampa mtihani yamegongana na mechi...

Wakati wanapanga hayo mashindano...Caf walikuwa hawajapanga tarehe ya mechi ya simba ya robo fainali...Kwahiyo hapo kishki na uongozi wa uwanja hauna kosa...Caf ndio wameingilia ratiba ya uwanja...


Na kuna mpuuzi mmoja hapo juu...Eti waislam na wakristo wanazimiana kiki kama sijui monaizi na nani sijui...

Nikupe tu taarifa...Waislaam tunapopanga mambo yetu huwa hatuangalii wakristo wamepanga nini watasema nini...Hayatuhusu ya wakristo...Kuwa na akili ya kiutu uzima...
 
Hayo mashindano yanakuwaga hapo miaka yote...Japo mimi siyafagilii mashindano yanayoendeshwa na huyu kishki...Labda ya huyu mama aisha sururu...
Lakini Uwanja ni kwa ajili ya Mpira,
Hata huko FIFA inajulikana ni uwanja wa mpira sio Dini..

Kwahiyo Busara hapo ingetumika walau yafanyike siku moja kabla au baada,

Lakini siku ya mechi hapa Kuna lawama zinaenda kutokea..

Takbiiir
 
Back
Top Bottom