Sol de Mayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 6,515
- 6,230
11 April 2022
CAF, TFF, SIMBA, ALHIKIMA WOTE WAKUBALIANA MASHINDANO YA QURAN NA MPIRA VITAFANYIKA SIKU MOJA TAREHE 17 APRIL 2022
MECHI ya kwanza ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC na Orlando Pirates ya Afrika Kusini itafanyika sambamba na mashindano ya Quran Jumapili ijayo.
Hayo yamesemwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally katika mkutano wake na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam.
“Maswali yamekuwa mengi kuhusu Uwanja wa Mkapa sababu siku ya mchezo dhidi ya Orlando Pirates kutakuwa na mashindano makubwa ya Quran, na inafahamika kwamba uwanja unatakiwa kuwa wazi kwa masaa 72 kabla ya mchezo,”.
“Baada ya mazungumzo baina ya Simba, CAF, TFF na waandaaji wa mashindano ya Quran tumekubaliana matukio yote yatafanyika ndani ya siku hiyo moja na CAF wamebariki hilo,” amesema Ahmed Ally.
Mechi hiyo inatarajiwa kuanza Saa 1:00 usiku.
Safi sana,,,nawasubiri wagalatia ambao hawakupenda iwe hivyo