Kuna umuhimu wa kufutilia mbali vyama vya upinzani vilivyopo ili kuleta mapinduzi ya siasa Tanzania



Nani kakuzuia kuanzisha chama? Vyama ni watu sio mtu
 
Kwa vile umeshasema la kijinga hata sishangai kwa kuanzisha mada kama hii, maana kimtokacho mtu ndicho kilichoujaza moyo wake
 
Kwa sababu hawana mamlaka. Swali jingine. Mnaiacha Takukuru mnakuja kuwabeza upinzani eti hawapambani na ufisadi.
Kinachoshindikana nchi jirani unakiona??? Au nao ingebidi waitwishe mzigo takukuru ya kwao???

Toka lini nyani akatatua shida na mahitaji ya ngedere?
 
Nani kakuzuia kuanzisha chama? Vyama ni watu sio mtu
Sio Kila mtu anaweza kufanya Kila kitu,ndio maana wapo hao waliopo ila bahati mbaya hakuna kitu wanafanya
 
Kupambana na UFISADI ni jukumu la kila mwananchu sio la vyama vya siasa
Mwananchi anapambana vipi na ufisadi wakati kateua watu wamwakilishe katika ilo,Sasa Kama Ni hivyo ataenda kwa shamba muda gani?
 
Yeye yuko wapi sasa, na mawazo yake hayo mfu ?!.

Ufisadi umefanywa na CAG amethibitisha lakini mwenye vyombo vya dola, vya uchunguzi na vya maamuzi. Hawataki hata kujadili. Lakini wewe mawazo yako ni wapinzani. Strange !!
Unategemea vyombo ya dola? Ahah
 
kwahiyo hakuna chochote wanachoweza kufanya kama upinzani kupambania maslahi ya nchi kwasababu wapo nje ya mfumo? Mbona kula na wezi wanaweza? Kwenye kushirikiana na watesi wa watanganyika wanaweza ila kwenye kupambana nao wanakua nje ya mfumo? Sasa wana kazi gani na faida gani kuendelea kuwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…