ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
CCM ndio Ina wataalamu? Au ndio TanRoads/Tarura? Kutojua adui ni kupoteza pambano.Kujua CCM ina laana njoo huku kilwa road ujionee maajabu ya dunia unaweza kufa Kwa kucheka maana barabara inayoitwa ya mwendokasi ni zaidi ya kuzimu...
Sisi tupo nchi za jina baya alilosema mzee trumpet,sii tunajua kula kama mchwa pekee,uzalendo,uadilifu kwetu hauna thamani,na kuwa mwadilifu unatengeneza maadui,hata wakukutoa roho.Katika fuatilia zangu, nimegundua kuwa kuna upigaji mkubwa sana kwenye miradi ya ujenzi hasa majengo mbalimbali na barabara nchini Tanzania.
Kiukweli barabara nyingi nchini zinajengwa chini ya kiwango, kuanzia upana , hadi ubora wa barabara husika na kamwe huoni wakandarasi wakichukuliwa hatua jambo linaloashiria kandarasi husika kupatikana kwa njia ya rushwa.
Nimejaribu kufuatilia namna barabara za wenzetu kwenye mataifa ya hapa hapa Afrika zinavyojengwa mfano Afrika Kusini, Algeria, Ivory Coast, Kenya na hata Morocco na kusema kweli nimekuja kugundua barabara zetu zinajengwa kwa viwango duni sana na kwa gharama kubwa sana tofauti na wenzetu.
Ukitazama barabara nyingi zinazojengwa na Tarura hazina hata sehemu za Watembea kwa miguu (Pedestrians) na nyingi hazifungwi hata taa za kuona usiku kwa watembea kwa miguu na inasemekana fedha hizo huwa zinatengwa kwenye bajeti za ujenzi wa barabara husika.
Tanzania tuna kazi kubwa sana kwa kweli hasa katika uadilifu wa watu wetu na uzalendo wa wstu wetu katika kufanya mambo wakiangalia maslahi ya Taifa badala ya maslahi yao binafsi.View attachment 3097223View attachment 3097224View attachment 3097225
Ndio shida ya kuwa na wahandisi waliokariri mambo na pia kujenga Kwa Maelekezo ya Wanasiasa.Kimara-kibaha highway watu wanavuka kwenye zebra!!maengineer kweli walishindwa kuweka vivuko vya underground!vitu vingine hadi aibu aisee!
Kama flaiova ipi hiyo yenye quality mbovu? Acha kuwa mjingaAwamu hii hata flyover ni quality mbovu ukilinganisha awamu iliyopita
Mfumo wote umeoza sema hivyo huna haja ya kujichosha.Ndio shida ya kuwa na wahandisi waliokariri mambo na pia kujenga Kwa Maelekezo ya Wanasiasa.
Barabara zina ubora hafifu, ndio sababu ya kujaza mizani kila wilaya, ndio sababu barabara za kwenu vumbi City ziko kama matuta ya viazi vitamu, barabara hazizingatii watembea kwa miguu na waendesha baiskeli na ni nyembamba sana pia.Ukweli upi hapo? Hana lolote huyo
Sio kweli,ubora uko vizuri ila madai yake mengi yanahusiana na usanifu duni na aging roads na sio kujengwa chini ya kiwango ndio maana hajathibitisha.Barabara zina ubora hafifu, ndio sababu ya kujaza mizani kila wilaya, ndio sababu barabara za kwenu vumbi City ziko kama matuta ya viazi vitamu, barabara hazizingatii watembea kwa miguu na waendesha baiskeli na ni nyembamba sana pia.
Nyie ndiyo mnaendesha nchi hii Kwa kilakitu na sekta zote zipo chini yenu ndiyo maana tunawalaumu nyieCCM ndio Ina wataalamu? Au ndio TanRoads/Tarura? Kutojua adui ni kupoteza pambano.
CCM ni chama kama Chadema tuu hawana wataalamu wa Barabara,hiyo ni kazi ya serikali so taasisi za serikali ndio zilaumiwe.Nyie ndiyo mnaendesha nchi hii Kwa kilakitu na sekta zote zipo chini yenu ndiyo maana tunawalaumu nyie
ChoiceVariable ulipost Uzi juu ya maandalizi wa ujenzi wa barabara za DAR chini ya tarura...Je Hadi sasa huo mradi umeishia wapi?
Tuliambiwa kuna miradi mingi ya barabara hasa zile za kuunganisha wilaya Kwa wilaya Kwa lami je Hadi Leo ziko wapi?
Ndio....Hili nalo ni la CCM ???
Ccm na serikali huwezi kuvitenganisha....CCM ni chama kama Chadema tuu hawana wataalamu wa Barabara,hiyo ni kazi ya serikali so taasisi za serikali ndio zilaumiwe.
Mradi upo hao ila taratibu za pesa ndio zinasubiliwa kutoka WB.
Pesa ya WB Huwa Ina michakato Mingi sana ya Kisenge na semina zisizoisha.
Unaelewaje unavyosikia barabara imejengwa kwenye viwango vya juu ya ubora?Sasa picha ulizoonesha na mifano ya Barabara kukosa sehemu ya watembea Kwa miguu vinahusianaje na ujenzi chini ya kiwango?
Wewe ni mjinga mmja tuu,design ndio inaamua Barabara ijengwe vipi na mwisho sio kweli kwamba Barabara zetu Hazina watembea Kwa miguu.
Ubora wa barabara unaanzia kwenye usanifu hadi usimamizi wa ujenzi.Tatizo lipo kwenye usanifu na usimamizi wa ujenzi .
Shida inakuwa ni design sio wajenzi.Unaelewaje unavyosikia barabara imejengwa kwenye viwango vya juu ya ubora?
Unasema hakuna shida kwenye ujenzi ila shida ni design, nenda Dodoma kagua barabara inayotoka kwa Waziri Mkuu hadi Shule ya Martin Luther alafu njoo na hizo hoja zako ili ujione ulivyo mjinga.
Ubora wa barabara ni ujumla wake kuanzia usanifu hadi ujenzi. Fedha wanazolipwa zinahusisha kuanzia usanifu hadi ujenzi.Shida inakuwa ni design sio wajenzi.
Wilaya ya ubungo inaongoza kwa kuwa na barabara mbovu,watu wamepania huu uchaguzi wa serikali za mitaa,ccm labda waibe ndio washinde,hamna anaewatakaNyie ndiyo mnaendesha nchi hii Kwa kilakitu na sekta zote zipo chini yenu ndiyo maana tunawalaumu nyie
ChoiceVariable ulipost Uzi juu ya maandalizi wa ujenzi wa barabara za DAR chini ya tarura...Je Hadi sasa huo mradi umeishia wapi?
Tuliambiwa kuna miradi mingi ya barabara hasa zile za kuunganisha wilaya Kwa wilaya Kwa lami je Hadi Leo ziko wapi?
Kila mmoja anapiga kutokana na eneo lake lo hakuna namna