King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Nakubaliana nawe 100%. Kama huu utekaji na uuaji seerikali isingekuwa inahusika kwa namna moja au nyingine, isingechukua muda kwa serikali kujua ukweli wa jambo kubwa kama hili na watu waliohusika kukamatwa. Hata pale viongozi wa polisi wanapoliongelea, body language inaonyesha kabisa wanajua wanachosema sio kweli
Kwa mfano kamanda mmoja wa Polisi anaongea kama vile hana uwezo wa akili sawasawa kwamba tulipomhoji Sativa, akiwa na polisi, alisema alitekwa na washikaji. Kwenye mitandao, akiwa mbali na polisi, kaongea tofauti. Sasa wewe, kama Sativa anaona anahojiwa na Polisi waliomteka, atasema nilitekwa na Polisi, wakati hana nguvu na anajua wanaweza kuja kummalizia kuua ushahidi wowote zaidi alionao? Hivi huyu mtu anawezaje kukomalia argument kama hiyo kama ana akili sawasawa?
Kabisa ,huyo kamanda J4 anajua kinachoendelea ,Sativa kasema wazi kwamba alipelekwa OYSTERBAY na hata simu yake ilionyesha ilikuwa oysterbay polisi maana walisahau kuzima ,Mafwele akatoa order akauliwe ,hao "WASHIKAJI" wakampeleka Polisi ya Arusha akakaa siku 2 ,inakuwaje WASHIKAJI waende kumuhifadhi kituo cha polisi Arusha?
Hawajiulizi kila wanachofanya wanaumbuka? Tukio la Lissu na Sativa limewaacha Uchi kwa ushiriki wao wa waziwazi.