Kuna uwezekano kwamba wanaoteka na kuua wanafanya hivyo kwa maslahi yao bila raisi Samia kujua kwa kuwa wananufaika na uwepo wake madarakani?

Kuna uwezekano kwamba wanaoteka na kuua wanafanya hivyo kwa maslahi yao bila raisi Samia kujua kwa kuwa wananufaika na uwepo wake madarakani?

Nakubaliana nawe 100%. Kama huu utekaji na uuaji seerikali isingekuwa inahusika kwa namna moja au nyingine, isingechukua muda kwa serikali kujua ukweli wa jambo kubwa kama hili na watu waliohusika kukamatwa. Hata pale viongozi wa polisi wanapoliongelea, body language inaonyesha kabisa wanajua wanachosema sio kweli

Kwa mfano kamanda mmoja wa Polisi anaongea kama vile hana uwezo wa akili sawasawa kwamba tulipomhoji Sativa, akiwa na polisi, alisema alitekwa na washikaji. Kwenye mitandao, akiwa mbali na polisi, kaongea tofauti. Sasa wewe, kama Sativa anaona anahojiwa na Polisi waliomteka, atasema nilitekwa na Polisi, wakati hana nguvu na anajua wanaweza kuja kummalizia kuua ushahidi wowote zaidi alionao? Hivi huyu mtu anawezaje kukomalia argument kama hiyo kama ana akili sawasawa?

Kabisa ,huyo kamanda J4 anajua kinachoendelea ,Sativa kasema wazi kwamba alipelekwa OYSTERBAY na hata simu yake ilionyesha ilikuwa oysterbay polisi maana walisahau kuzima ,Mafwele akatoa order akauliwe ,hao "WASHIKAJI" wakampeleka Polisi ya Arusha akakaa siku 2 ,inakuwaje WASHIKAJI waende kumuhifadhi kituo cha polisi Arusha?

Hawajiulizi kila wanachofanya wanaumbuka? Tukio la Lissu na Sativa limewaacha Uchi kwa ushiriki wao wa waziwazi.
 
Kama no hivo yeye kama namba moja nchi imemshinda Hana control ya anao waongoza hivyo aachie ngazi
 
Hivi umeenda shule wewe? Inaonekana nadharia ya thread huelewi kabisa. Huu sio ushahidi au proven facts naweka hapa. Hizi ni plausible scenarios juu ya what is behind utekaji na uuaji, ikimaanisha one of the four could be true, but not necessarily all of them. Elewa context acha kuji-expose weakness yako katika mambo ya uchambuzi. Hata katika upeleleze tunaanza na scenarios, na kisha una-eliminate moja baada ya nyingine. Ndio maana mkeo anaweza kuuwawa wewe kama mume ukawa mshukiwa, hadi iwe proven otherwise
Aisee..!! Mtu akienda shule, haendi shule za mambo yote yaliyopo duniani, na ndiyo maana kunakuwa na specialities..!! Specialist wa hili, ni kilaza wa lile..!!! Na hili si la kukushangaza. Na ndiyo maana haishangazi kuona mtu bingwa wa jambo fulani, lakini gari yake anauipeleka wa aliyemaliza LY ya la saba akamtatulia jambo lihusulo gali yake.

Matumizi ya neno labda, inawezekana, wanaweza yanaonyesha kukosa uhakika wa pointi inayosemwa. Lakini, kama ulivyosema kwenye post yako, haiwezekani rais awe hajui utekaji unafanywaje hapa TZ. Kutokukamatwa kwa watekaji kunatupa shaka kwamba anawajua watekaji. Kwasabu kuna mambo makubwa yaliyofanywa kwa siri sana na hayakuwa na uhusika wao, lakini mwisho wa siku yamejulikana na wahusika wamejulikana.
 
Kama no hivo yeye kama namba moja nchi imemshinda Hana control ya anao waongoza hivyo aachie ngazi
Spot on. Kama raisi wa Tanzania anashindwa kutumia vyombo vyake vya usalama kuweza kujua ukweli wa jambo kama hili mara moja, basi huyo ni hatarishi kwa usalama wa nchi. Hawezi kusimamia intelijensia ya Tanzania ili kuhakikisha nchi iko salama. Ina maana maadui wa ndani au nje wanaweza kutuumiza kirahisi sana. Sasa ni aidha awaondoe viongozi wote wa juu wa Polisi na Usalama wa Taifa, au aondoke yeye kwa kukiri kushindwa kusimamia usalama wa wananchi wa Tanzania
 
Aisee..!! Mtu akienda shule, haendi shule za mambo yote yaliyopo duniani, na ndiyo maana kunakuwa na specialities..!! Specialist wa hili, ni kilaza wa lile..!!! Na hili si la kukushangaza. Na ndiyo maana haishangazi kuona mtu bingwa wa jambo fulani, lakini gari yake anauipeleka wa aliyemaliza LY ya la saba akamtatulia jambo lihusulo gali yake.

Matumizi ya neno labda, inawezekana, wanaweza yanaonyesha kukosa uhakika wa pointi inayosemwa. Lakini, kama ulivyosema kwenye post yako, haiwezekani rais awe hajui utekaji unafanywaje hapa TZ. Kutokukamatwa kwa watekaji kunatupa shaka kwamba anawajua watekaji. Kwasabu kuna mambo makubwa yaliyofanywa kwa siri sana na hayakuwa na uhusika wao, lakini mwisho wa siku yamejulikana na wahusika wamejulikana.
Unatumia shule ya form two kufanya uchambuzi wa thread za level ya university
 
Ongea Mkuu, ongea usiogope!
Msi-umeume maneno. Samia anajua yote kuhusu utekaji. Hakuna kinachofanyika bila rais kujua na kuunga mkono. Never never. Tanzania hii hi ambayo rais anaogopewa kuliko Mungu kiongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama aamuru mtu atekwe au auawe bla rais kujua? Haiwezekani, haiwezekani.
 
Mhusika wa UUWAJI ni kizimkazi Kwa sababu ameshindwa kuvisimamia vyombo vya ulinzi kuacha kuua na kuteka badala yake ameonesha dharau Kwa waliouliwa Kwa kuwaita sisimizi na kusema kifo ni kifo tu tukizoee.
 
Mkuu unajua dhana ya collective responsibility?

Israel Hamas wameteka mateka wa kiisraeli wananchi wanaandamana kumshinikiza Kiongozi wao ahakikishe wanapatikana
Tanzania “wasiojulikana” wanateka na kuua watu Rais mwenye nyenzo zote akishinikizwa ukweli ujulikane mnatokea wajinga kumtetea

Sasa kama vyombo vya dola vyenye wajibu wa kutupa majibu na kukomesha utekaji na mauaji hayo hawafanyi hivyo mnataka nani abebeshwe huo mzigo?
Wabebeshwe wanao tekwa na kuuwawa?

Na kama kuna watu wanamuhujumu mh rais kwa kufanya mauaji hayo huoni kwamba wamemuona NI DHAIFU wanaweza kufanya lolote na hana cha kufanya
Kama unadhani unamtetea kwa hoja yako hiyo nadhani utakua unakosea sana kwa Rais mwenye vyombo vyote vya ulinzi na usalama
 
Nakuelewa kabisa Mkuu. Kwa hiyo hapa unasema unaongeza scenario y kwamba Samia anajua na kuwa consulted na kila kinachofanyika?;
  1. Wanaofanya haya wanafanya haya wakiwa wamemshawishi Raisi Samia kuwaacha wafanye kile ambacho wanaona ni kwa faida yake na serikali/CCM bila yeye kuhusika moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa Raisi Magufuli, kwamba wewe tuachie sisi, tunajua la kufanya, wewe kaa kando.
  2. Samia anajua na anakuwa consulted kuhusu kila kinachofanyika
Mmmh, ni maneno ya kufikirika pia
 
Mhusika wa UUWAJI ni kizimkazi Kwa sababu ameshindwa kuvisimamia vyombo vya ulinzi kuacha kuua na kuteka badala yake ameonesha dharau Kwa waliouliwa Kwa kuwaita sisimizi na kusema kifo ni kifo tu tukizoee.
Kuna maneno ambayo raisi Samia anakosea sana kuyatamka, na nakiri ni maneno ambayo si busara kwa raisi wa nchi yetu kuyasema. Moja wapo ni hili la kusema kifo ni kifo tu juu ya utekaji na uuaji, na lile la kusema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Mkuu unajua dhana ya collective responsibility?

Israel Hamas wameteka mateka wa kiisraeli wananchi wanaandamana kumshinikiza Kiongozi wao ahakikishe wanapatikana
Tanzania “wasiojulikana” wanateka na kuua watu Rais mwenye nyenzo zote akishinikizwa ukweli ujulikane mnatokea wajinga kumtetea

Sasa kama vyombo vya dola vyenye wajibu wa kutupa majibu na kukomesha utekaji na mauaji hayo hawafanyi hivyo mnataka nani abebeshwe huo mzigo?
Wabebeshwe wanao tekwa na kuuwawa?

Na kama kuna watu wanamuhujumu mh rais kwa kufanya mauaji hayo huoni kwamba wamemuona NI DHAIFU wanaweza kufanya lolote na hana cha kufanya
Kama unadhani unamtetea kwa hoja yako hiyo nadhani utakua unakosea sana kwa Rais mwenye vyombo vyote vya ulinzi na usalama
Ndio maana nilisema, "ni vigumu sana kuwazia kwamba watu walio katika mfumo wa vyombo vya dola vya usalama, au viongozi mafisadi serikalini, wanaweza kufanya haya bila raisi Samia kujua. Haiwezekani kabisa kwamba "intelijensia" ya raisi Samia ndani ya serikali na vyombo vya dola vya usalama haina habari juu ya hili jambo ambalo linafanya raisi Samia asiwe na habari juu yake. Siwezi kuamini kwamba raisi Samia hajui juu ya hili kwa sababu tu ya udhaifu wa intelijensia yake binafsi (the president's people) au intelijensia rasmi ndani ya serikali au vyombo vya dola vya usalama, ambayo ingempa habari kamili juu ya jambo hili. Huwezi ukawa raisi wa nchi halafu usiwe na intelijensia ndani ya vyombo vya usalama ya kukuwezesha kujua jambo kama hili - utapinduliwa au kuuawa kirahisi sana!

"Kwa maelezo haya, inafanya raisi Samia astahili lawama zote za utekaji na uuaji unaoendelea, hata kama hahusiki moja kwa moja"
 
Back
Top Bottom