Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

wanaomjua polepole, hawapendi hata kumsikiliza kwenye izo clip zake. ila ninyi ambao hammjui kiundani ndio mnashobokea. anafanya maigizo, ni mmoja wa watu walioharibu sana nchi hii kwenye uchaguzi wa 2020. ndio maana ana gurts hata za kusema jpm hakumaliza wote ambao yeye anatamani wangekuwa wamemalizwa. ni mchafuzi tu ambaye anataka kuturudisha kwenye zile siasa za miaka 6 zilizotuumiza moyo na kutuondolea pesa mifukoni watu wakaishi kama mashetani.

Mpuuzeni au mfukuzeni chama muone ataenda wapo, hana kwa kwenda, hana uzoefu wa maisha, na hakuna atakayempokea mwenezi wa ccm wa 2020. anajifanay ni mwanaccm, lakini haijui ccm, aliokotwa tu akawekwa kwenye chama akaongoza watu waliokotolea jasho la damu, akawanyanyasa na sasaivi anawasema kuwa walitakiwa wamalizwe. poor him.

huyu hana tofauti na bashite, aliyesaidiwa na rizmoko na jk kupewa cheo, aliokotwa tu, lakini mwishoni akajifanya mzalendo sana kiburi kilipokuwa juu, akamsingizia rizmoko kuwa anauza madawa. hata kama alikuwa anauza, usaliti kwa mtu aliyekusaidia wa namna hii ni kwa mtu ambaye hana maana na haaminiki, anaweza kumsaliti hata mzazi wake wa kumzaa.

ila ninachowapendea watz ni kuwa, wana ugonjwa wa kusahau mno, polepole yule wa bunge la katiba, aliyebadilika akawa nyoka wa kijani kwenye uenezi na uchaguzi, leo anabadilika anataka kuwa kondoo anaonewa huruma na atapata wafuasi. wameshasahau na yeye akiamua atawashangaza tena kwa kituko kingine.
 
Mwalimu Nyerere alijihudhuru uwaziri mkuu ili aendelee kupigania alichokiamini; yaani uhuru wa Tanganyika! u-PM ambao ungempa kila kitu haukumfanya abadili msimamo wake!

Tuje kwa Polepole sasa! Ile kupewa u-DC tu akasailiti misimamo yake wakati wa Bunge la Katiba. Msimamo wa ni namna gani cheo hicho hakistahili kuwepo! Alipopewa Uenezi wa CCM, akasaliti misimamo yake yote kuhusu katiba mpya, na mambo mengine yote aliyokuwa anayatetea awali!

Leo hii kaporwa tonge mdomoni, ndo anarudi kuwa Polepole yuleyule wa kabla hajapewa u-DC! Kwa maelezo hayo, please don't insult our father of the nation! NI kweli Polepole anajua sana kujieleza na kujenga hoja lakini kujua kujieleza na kujua kujenga hoja ni jambo moja na kusimamia unachokiamini ni jambo lingine!

Suala la kujua kujenga hoja halina maana yoyote kwa jamii bali muhimu ni kusimamia unachokiamini hata kama kitahatarisha maslahi yako binafsi na ya watu wako wa karibu! Sifa hii tukufu Polepole hana, na wala sisemi hana kwa majungu bali mwenyewe amedhihirisha kutokuwa nayo!
 
Swali la nyongeza:

Je Nyerere aliwahi kujisifia kutembea na Vieitee??
Polepole ni mjamaa mnafiki. Anatetea ujamaa huku akiishi kibepari. Sikuwahi ona bashiru na polepole awakuwahi hata siku moja kupinga au kukataa matumizi ya v8 walizopewa. Thus tunasema ujamaa una unafiki ndani yake.

Check kama Kim wa North Korea ni mjamaa anae ishi kibepari huku anaowatawala wakiishi kijamaa
 
Pascal Mayalla upo sahihi, nimesikiliza mkutano wa Polepole, hakika ameniliza kwa hekima yake. Yaani nilikuwa najiuliza anatoa wapi hizi hekima, kumbe ni kupitia elimu aliyosomeshwa na kodi za Watanzania. Mungu atatuvusha hiki kipindi, naamini ipo siku kuna watu watatamani kuhama nchi! Maana Watanzania wana hasira kubwa sana juu ya hawa wanaojiita wenye chama.
 
polepole ni mchumia tumbo tuu kama wachumia tumbo wengine Polepole halisi tulishamzika siku nyingi... hapa saiv hana upepo anataka kuludi kwenye uwanaharakati
Tunaagalia hoja zenye maslahi kwa nchi, huwezi kumlinganisha pole pole na Makamba au Nape. Ingawa Nape na Makamba wanao muda wa kutubu na kujirudi ila kwa akili zao finyu hawawezi ona.
 
huyu hana tofauti na bashite, aliyesaidiwa na rizmoko na jk kupewa cheo, aliokotwa tu, lakini mwishoni akajifanya mzalendo sana kiburi kilipokuwa juu, akamsingizia rizmoko kuwa anauza madawa. hata kama alikuwa anauza, usaliti kwa mtu aliyekusaidia wa namna hii ni kwa mtu ambaye hana maana na haaminiki, anaweza kumsaliti hata mzazi wake wa kumzaa.

ila ninachowapendea watz ni kuwa, wana ugonjwa wa kusahau mno, polepole yule wa bunge la katiba, aliyebadilika akawa nyoka wa kijani kwenye uenezi na uchaguzi, leo anabadilika anataka kuwa kondoo anaonewa huruma na atapata wafuasi. wameshasahau na yeye akiamua atawashangaza tena kwa kituko kingine.
Kama ni kuokotwa hakuna ambaye hakuokotwa, hata Kikwete wako kuna mahali aliokotwa pia, hivyo hiyo siyo hoja, ni lazima uwe na pa kuanzia na ili uokotwe ni lazima uokoteke pia.
 
Kama ni kuokotwa hakuna ambaye hakuokotwa, hata Kikwete kuna mahali alipkotwa pia, hivyo hiyo siyo hoja, ni lazima uwe na pa kuanzia na ili uokotwe ni lazima uokoteke pia.
Kuna wengine wameokotwa zaidi ya wengine mzee, na pia mtu asiyekumbuka alikotoka sio wa kuaminiwa, anaweza kukusaliti hata wewe unayekuja kumwamini mara ya pili. Peware. Kama alitusaliti kwa vile alivyotoka bunge la katiba na kuendesha mijadala mingi, akatusaliti kabisa alipokuwa mwenezi, sasaivi ameona hana mwelekeo na hatashinda ubunge na hana future CCM anakuja kwako na wewe unampokea, utakuwa umekosa wa kumwamini basi.
 
Kiukweli Polepole ni Nyerere wa nyakati hizi.

Mungu wa mbinguni ambariki sana!
Mmeshasahau kigeugeu alichotufanyia tangu kwenye bunge la katiba, akaja kwenye uenezi na mnayajua aliyoyafanya na bashiru, na sasa anataka kumkwamisha mama mnashangilia, na mtamwamini. watz mna ugonjwa wa kusahau na aliyewaloga kafa.
 
watu tunasahau sanaa
 
Napinga!

Km hako kajamaa kazandiki kangekuwa na baraka km za nyerere, nakuapia angekuwa ameshatambulika na taifa hili zamani tu tangu ktk his earl 20s na wala asingehitaji kutumia nguvu sasa hv za kujitambulisha bila mafanikio katika hiyo miaka yake 50+

Kiongozi we ni mzoefu wa kutosha na ninaamini kwa 100% unaona kabisa kuwa jamaa hana mvuto wala mashiko. Hapo alipofikia ndiyo juu kabisa, hatopiga hatua tena!! Ameishiwa, ameisha
 
namwelewa sana Polepole!wanaomponda na wasiwasi sio wa tz

baada ya jpm ninayeweza kukaa nikamsikiliza ni polepole,very smart kwenye kupanga na kujibu hoja,

ni moja ya top 3 ya watu wangu wanaojua kujibu na kupanga hoja,

Peter msigwa anamjua waliwahi kupiga nae mjadala channel 10.,alinyooshwa

mjadala wa 1.5trillion jamaa aliujengea hoja kwa kudadavua,kitu ambacho NAPE,CHONGOLO hawawezi
 
Back
Top Bottom