Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Wanaomuchukia Polepole ni_
CHADEMA ambao walipigwa kitu kizito kichwani enzi za Polepole wakaambulia Mbunge mmoja.

Wale wanaokula mezani kwa Hangaya na wavia teuzi.
Wananchi wa kawaida
wanamukubari Sana.
 
Wanabodi,
Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa!, ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!.

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere!. Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?.

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!.
Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea...

Ni kama Mwalimu kabisa!.
Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.
Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga!, akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga".

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?.
Paskali
Mimi pia nashindwa kuwaelewa watu wanaomponda HP. Tatizo lake ni nini hasa? Nadhani watu wanamuona kama version ya JPM, Nadhani walokuwa na hasira na JPM wanaona wamalize hasira zao kwa HP. Ila huyu anaweza wasumbua iwapo watataka kushughulika nae, ata wademsha kweli maana akili kiasi fulani na HANA CHA KUPOTEZA. Niseme tu ukweli amejiposition vizuri na ana simphasize na wafuasi wa JPM.
 
Mwl Nyerere alikua anatembea hovyo na warembo wa UVCCM?
Hii ni statement!
1639253407482.png
 
Polepole siyo mtu mstaarabu. Hawezi kushirikiana. Ili ushirikiane inatakiwa kukubali mtazamo wa wengine hata kama hukubaliani nao, kama vile ambavyo wao wanakubaliana na wewe hata wasipokubaliana nawe. Ukiona mtazamo wao ni mbaya sana basi unaacha kushirikiana nao mazima.

Sasa anaonekana kama mtu mgomvi tu. Unashikilia habari ya awamu ya 5 vs 6 ili iweje? Jambo lisilo na faida yoyote kwa nchi! Ni ugomvi na kukosa ustaarabu.

Mtu kama huyu akiwa rais ni rahisi nchi kuingia vitani, hawezi kucompromise.
Shetani alisha kaa nanyi tangu bustani ya eden,
Hamuwezi kutambua kitu kizuli mpaka kitakapo ondoka na mkajikuta kwenye maumivu ndo mnakumbuka uzuri mlio ukataa.
Mungu anasema njooni kwangu huku ndiko palipo salama, nyie mnabisha eti ooh huko hakuana starehe mara wewe mungu ni mukoloni unatubana saana,
Mungu anarudia nyie huko mtaungua moto na nyie mnamwambi aah wapi unatuzuga.
Mkishaenda na kukuta moto mnaanza kilio ooh tusamehe mara nini lakini muda sio rafiki tena.
Sasa ndo nyie.
Mnamuona polepole mpuuzi lakini hajaomba kula pesa ya wananchi kifisadi anacho taka rasilimali za wanachi zitumike vizuri na msukumo wa wananchi kujitawala kiuchumi na haki kwa kila mtu.

Bali mnataka wahuni wawabane na kuwaambia unanijua mimi nani😳😳😳
 
Wanabodi,
Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa!, ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!.

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere!. Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?.

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!.
Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea...

Ni kama Mwalimu kabisa!.
Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.
Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga!, akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga".

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?.
Paskali

Mwalimu Nyerere angekuwa kama huyu chakubanga ambaye hata Corona anafikiri ni siasa kama watu wa vijiweni😂😂😂
 
Mkuu hii generation ni ya kizazi pompompo wazee wa oyaa oyaa kushoto twende kulia twende wala isikushangaze sana [emoji16]
Ni jamii inayotazama nani kaongea na sio nini kimeongelewa.
Mfano hoja nyepesi tu viongozi wawe wazalendo wamtii Mungu wajali maslahi ya watu wasifanye uhuni kwenye raslimali za nchi mbona ni simple content tu na ipo direct TATIZO IMEZUNGUMZWA NA NANI? Polepole aaaah basi haifai hiyo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unaijua V8 wewe V8,ndo tunazotembelea
Paskali kabla ya Polepole kuendelea kutupigia kelele aseme kwanza kwanini alitaka watu wanyamaze walipokuwa wakinyoosha nchi na sasa kwa nini yeye hataki kunyamaza wenzake wanapofungua nchi?

Haki ya kuongea anaitoa wapi ilihali wao hawakutaka wengine wapate haki hiyo alipokuwa akizunguka na Vee Eiteh?
 
wahuni tu ndo hawamwelewi

Polepole siyo mtu mstaarabu. Hawezi kushirikiana. Ili ushirikiane inatakiwa kukubali mtazamo wa wengine hata kama hukubaliani nao, kama vile ambavyo wao wanakubaliana na wewe hata wasipokubaliana nawe. Ukiona mtazamo wao ni mbaya sana basi unaacha kushirikiana nao mazima.

Sasa anaonekana kama mtu mgomvi tu. Unashikilia habari ya awamu ya 5 vs 6 ili iweje? Jambo lisilo na faida yoyote kwa nchi! Ni ugomvi na kukosa ustaarabu.

Mtu kama huyu akiwa rais ni rahisi nchi kuingia vitani, hawezi kucompromise.
Low iq
 
Shetani alisha kaa nanyi tangu bustani ya eden,
Hamuwezi kutambua kitu kizuli mpaka kitakapo ondoka na mkajikuta kwenye maumivu ndo mnakumbuka uzuri mlio ukataa.
Mungu anasema njooni kwangu huku ndiko palipo salama, nyie mnabisha eti ooh huko hakuana starehe mara wewe mungu ni mukoloni unatubana saana,
Mungu anarudia nyie huko mtaungua moto na nyie mnamwambi aah wapi unatuzuga.
Mkishaenda na kukuta moto mnaanza kilio ooh tusamehe mara nini lakini muda sio rafiki tena.
Sasa ndo nyie.
Mnamuona polepole mpuuzi lakini hajaomba kula pesa ya wananchi kifisadi anacho taka rasilimali za wanachi zitumike vizuri na msukumo wa wananchi kujitawala kiuchumi na haki kwa kila mtu.

Bali mnataka wahuni wawabane na kuwaambia unanijua mimi nani😳😳😳
JamiiForums fanya kupin hii comment
 
Back
Top Bottom