Wanabodi,
Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa!, ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!.
Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere!. Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?.
Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!.
Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea...
www.jamiiforums.com
Ni kama Mwalimu kabisa!.
Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.
Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga!, akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga".
Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?.
Paskali