Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

nasikitika kusema hukumfahamu Nyerere. Endelea kumtafiti umjue vizuri
Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.
Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere!. Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!.
P
 
Wanabodi,

Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa!, ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!.

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere!. Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?.

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!.
Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea...

Ni kama Mwalimu kabisa!.
Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.
Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga!, akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga".

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?.
Paskali

Acha kumdhalilisha mwalimu Nyerere kwa kumfananisha ni mtu wa ajabu ajabu.
Kuweka kumbukumbu sawa tu mwalimu Nyerere alikuwa na msimamo, hakuendekeza tumbo na hakuwa malaya wa kisiasa mambo ambayo yanamtofautisha kwa 100% na huyu Pole Pole.

Watu wanauliza hivi yule Pole Pole wa katiba mpya kipindi cha tume ya Warioba yuko wapi? Ukimleta huyo Pole Pole hapa wanajamvi watakuelewa, tofauti na hapo hii edited&duplicated Pole Pole.

Kwa lugha nyepesi tu, Pole Pole ni dalali wa kisiasa, ukija na bidhaa ya kisiasa na ukifika bei utampata Pole Pole kirahisi sana.
 
Kichaa anapolinganishwa na mtu mwenye akili timamu, tena mwenye akili kubwa, ni tusi kubwa sana hili kwa Mwalimu Nyerere.

Huyu Polepole ambaye kwa kushirikiana na Bashiru na Magufuli, walikata majina robo tatu ya waliochaguliwa na wajumbe kwenye kura za maoni 2020, na kuwapachika watu waliowataka wao, leo eti wa kumlinganisha na Mwalimu! Lazima uwe mjinga kuelekea kwenye uwendawazimu kuliamini hilo.

Polepole huyu aliyesema katiba mpya ni muhimu na hitaji la Watanzania kwa sasa, baada ya kupewa kacheo, akasema Watanzania wanachohitaji ni barabara na maji, na siyo katiba mpya, ndiyo umlinganishe na Mwalimu, basi wewe lazima utakuwa ni kichaa.

Polepole huyu huyu aliyesema maDC na maRC hawana kazi, nafasi zao zinatakiwa kufutwa, baada ya kuteuliwa kuwa DC, akasema kazi ni nyingi, na yupo busy kutatua matatizo ya wananchi, leo eti wa kulinganishwa na Mwalimu! Lazima akili yako iwe retarded completely kuweza kufanya hivyo.

Wale ambao hawafahamu, wakati wa Mwalimu Nyerere, licha ya kwamba ulikuwa mfumo wa chama kimoja, demokrasia iliyokuwemo ndani ya chama ilikuwa ni ya kiwango cha juu kabisa. Hakuna aliyechaguliwa kwa maagizo au kukatwa jina lake na kakikundi ka watu kama ilivyokuwa enzi za akina Polepole. Kama kanuni inasema jina lipitishwe na Halmashauri kuu, ni kweli litapitishwa na Halmashauri kuu, siyo na Mwenyekiti, Katibu Mkuu na mwenezi kama enzi za akina Polepole.

Polepole ni rubbish katika siasa za kidemokrasia. Polepole ni uchafu katika uongozi kwa sababu ni kigeugeu. Polepole ni takataka katika siasa za kimaadili kwa sababu anahongeka kwa cheo. Polepole ni mnafiki kwa sababu hakuna anachokisimamia, msimamo wake unategemea yupo wapi, kwenye benchi au ndani ya Serikali.

Hiyo shule anayoiita ya uongozi, utawafundisha vipi watu uongozi wakati wewe mwenyewe huna sifa ya uongozi? Hiyo shule, hakuna chochote anachokilenga, zaidi ya kuwalenga waliopo kwenye Serikali mpya, kuonesha hawafai bali yeye na ile Serikali yake ya utekaji, data za uwongo, uminyaji wa uhuru, haki na demokrasia, walikuwa wanajua kuongoza.
 
Tatizo ni kwamba ukiwa mkweli utachukiwa. Na ukiwa mtu wa haki utatengwa. Polepole ni miongoninmwa watu Smart niliopata kuwafahamu.
 
Je anayoyazungumza haya huyo Polepole kwanini hakuyazungumza awamu ile akiwa na position kubwa?

Je ni kweli mabaya mengi tu ya awamu ile hakuyaona?

Dosari za kwenye chaguzi zote mbili Serikali za mitaa (2019) na uchaguzi "uchafuzi" mkuu (2020) Polepole hakuziona kama hakuwa sehemu ya ulaghai ule?

Polepole hakuona mwenendo wa wanasiasa/wanaharakati wenye mawazo kinzani na boss wake wa wakati ule walipokuwa wakizimwa na hadi wengi kukimbilia ng'ambo??

Polepole hakua sehemu ya maamuzi juu ya katiba mpya ila ghafla akabadilika kama kinyonga na kuwaacha watanzania midomo wazi??

Polepole huyu huyu alishuhudia sheria kandamizi za kimtandao ila hakuongea bali alikua akishushia mvinyo na kupongeza "one man show" ya boss wake..?

It's not over until it's over...Karma is a bitch
 
Well said,naanza kuamn uzee Paskali unamjia kwa kasi sana
Kichaa anapolinganishwa na mtu mwenye akili timamu, tena mwenye akili kubwa, ni tusi kubwa sana hili kwa Mwalimu Nyerere.

Huyu Polepole ambaye kwa kushirikiana na Bashiru na Magufuli, walikata majina robo tatu ya waliochaguliwa na wajumbe kwenye kura za maoni 2020, na kuwapachika watu waliowataka wao, leo eti wa kumlinganisha na Mwalimu! Lazima uwe mjinga kuelekea kwenye uwendawazimu kuliamini hilo.

Polepole huyu aliyesema katiba mpya ni muhimu na hitaji la Watanzania kwa sasa, baada ya kupewa kacheo, akasema Watanzania wanachohitaji ni barabara na maji, na siyo katiba mpya, ndiyo umlinganishe na Mwalimu, basi wewe lazima utakuwa ni kichaa.

Polepole huyu huyu aliyesema maDC na maRC hawana kazi, nafasi zao zinatakiwa kufutwa, baada ya kuteuliwa kuwa DC, akasema kazi ni nyingi, na yupo busy kutatua matatizo ya wananchi, leo eti wa kulinganishwa na Mwalimu! Lazima akili yako iwe retarded completely kuweza kufanya hivyo.

Wale ambao hawafahamu, wakati wa Mwalimu Nyerere, licha ya kwamba ulikuwa mfumo wa chama kimoja, demokrasia iliyokuwemo ndani ya chama ilikuwa ni ya kiwango cha juu kabisa. Hakuna aliyechaguliwa kwa maagizo au kukatwa jina lake na kakikundi ka watu kama ilivyokuwa enzi za akina Polepole. Kama kanuni inasema jina lipitishwe na Halmashauri kuu, ni kweli litapitishwa na Halmashauri kuu, siyo na Mwenyekiti, Katibu Mkuu na mwenezi kama enzi za akina Polepole.

Polepole ni rubbish katika siasa za kidemokrasia. Polepole ni uchafu katika uongozi kwa sababu ni kigeugeu. Polepole ni takataka katika siasa za kimaadili kwa sababu anahongeka kwa cheo. Polepole ni mnafiki kwa sababu hakuna anachokisimamia, msimamo wake unategemea yupo wapi, kwenye benchi au ndani ya Serikali.

Hiyo shule anayoiita ya uongozi, utawafundisha vipi watu uongozi wakati wewe mwenyewe huna sifa ya uongozi? Hiyo shule, hakuna chochote anachokilenga, zaidi ya kuwalenga waliopo kwenye Serikali mpya, kuonesha hawafai bali yeye na ile Serikali yake ya utekaji, data za uwongo, uminyaji wa uhuru, haki na demokrasia, walikuwa wanajua kuongoza.
 
Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.
Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere!. Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!.
P
Basi wewe kama mkatoliki mzuri nenda ukaungame kwa dhambi ya kumfananisha Nyerere na Polepole kwa makusudi.
 
wanaomjua polepole, hawapendi hata kumsikiliza kwenye izo clip zake. ila ninyi ambao hammjui kiundani ndio mnashobokea. anafanya maigizo, ni mmoja wa watu walioharibu sana nchi hii kwenye uchaguzi wa 2020. ndio maana ana gurts hata za kusema jpm hakumaliza wote ambao yeye anatamani wangekuwa wamemalizwa. ni mchafuzi tu ambaye anataka kuturudisha kwenye zile siasa za miaka 6 zilizotuumiza moyo na kutuondolea pesa mifukoni watu wakaishi kama mashetani. mpuuzeni au mfukuzeni chama muone ataenda wapo, hana kwa kwenda, hana uzoefu wa maisha, na hakuna atakayempokea mwenezi wa ccm wa 2020. anajifanay ni mwanaccm, lakini haijui ccm, aliokotwa tu akawekwa kwenye chama akaongoza watu waliokotolea jasho la damu, akawanyanyasa na sasaivi anawasema kuwa walitakiwa wamalizwe. poor him.

huyu hana tofauti na bashite, aliyesaidiwa na rizmoko na jk kupewa cheo, aliokotwa tu, lakini mwishoni akajifanya mzalendo sana kiburi kilipokuwa juu, akamsingizia rizmoko kuwa anauza madawa. hata kama alikuwa anauza, usaliti kwa mtu aliyekusaidia wa namna hii ni kwa mtu ambaye hana maana na haaminiki, anaweza kumsaliti hata mzazi wake wa kumzaa.

ila ninachowapendea watz ni kuwa, wana ugonjwa wa kusahau mno, polepole yule wa bunge la katiba, aliyebadilika akawa nyoka wa kijani kwenye uenezi na uchaguzi, leo anabadilika anataka kuwa kondoo anaonewa huruma na atapata wafuasi. wameshasahau na yeye akiamua atawashangaza tena kwa kituko kingine.
Mwalimu Nyereee hakuwa kinyonga
 
Aisee, Mkuu, Kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai na nguvu zake akasoma huu uzi angekucharaza viboko wewe na Polepole 😆
 
Back
Top Bottom