Kuna viashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani siku zijazo…

1. Mbona umekwepa kuwataja TISS kupewa kinga zaidi dhidi ya vitendo vya jinai wanavyotenda wakiwa kazini..kinga za namna hii hazina afya kabisa kwa jamii inayotaka kustaarabika..
2. Umekwepa pia tatizo la UDINI lipo wazi kwa sasa, watu wanatetea MABAYA vile tu yamefanywa na mtu wa IMANI yao..unafiki wa aina hii una madhara mabaya tena ya haraka!
3. Sijajua kama hilo baraza la usalama huwa linasubiri kuamshwa pale mambo yanapoashiria mwelekeo wa hali ya hatari..inawezekana baraza nalo lina upande, kwa watawala au kwa wananchi.
4. Maelezo yako ni kama uko kati pamoja na kueleza viashiria vya hatari inayokuja kwa taifa..ni vyema hata hivyo kuwaeleza watawala kuwa WAACHE hayo wanayofanya katiba iko wazi kwenye ibara ya 8 MAMLAKA YOYOTE ILIYOPO INATOKANA NA WANANCHI..wao ndiyo mamlaka ya kuamua hatma yao wenyewe, kama jambo wamelikataa unashupaza shingo kwa nini? Waache na si kuwaambia wafanyie kazi!
 
Umeongezea nukta muhimu sana. Haya mambo pia yafaa kuzingatiwa.
 
Ningekuwa moderator ningeku BAN life kabisa hapa JF. Watu ka ninyi sijui kwa nini mlizaliwa. Muacheni Mama afanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania. Bila CCM hakuna amani, ndiyo maana tunaendelea kushinda chaguzi zote.
Exactly
 
Wananchi wapo busy na shughuli za maendeleo hako kakikundi kanakopinga maamuzi ya serikali ni wana chadema wanafuta mileage ya kisiasa. Baraza la usalama la Taifa siyo chombo kidogo kudil na vitu vya kipuuzi hivi.
 
Huu ndiop ukweli, na ndio maneno yanayozungumzwa waziwazi hadi vijijini!
Na tatizo kubwa ni rushwa, ufisadi na wizi unaofanywa na watawala!
Inafikirisha: matumizi makubwa ya kuendesha SERIKALI yangu mimi na wewe, ... YETU ... sisi WATANGANYIKA!
ANASA inakua kipaumbele na mbadala wa KUFANYIA kazi viapo vile na kujikita kwenye ANASA hadi ubongo unanenepeana. Haijalishi SISI tunaendelea kuzidiwa na UFUKARA ule ule ... kule ulikotokea wewe KIONGOZI mwizi, FISADI mla rushwa wewe! Leohii baada ya kujaaliwa madaraka unaona saizi yako ni ANASA. Amin nasema, LAANA inakuhusu wewe na vizazi. Karma is a bad assed bitch!
 
Mimi siyo Mkatoliki, lakini naona dhahiri kabisa kwamba kumekuwa na mvutano mkubwa ambapo wasomi wengi wa kiislamu wanafurahia hicho kinachofanyika kwasababu wanadhani wanawakomoa Wakatoliki. Imefikia hadi wengine kusema mbona wakatoliki wanapiga kelele kuhusu mkataba wa DP-WORLD ilhali wao wamesaini Memoranda of Understanding (MoU) na serikali kwenye masuala ya elimu na afya.

Kihistoria, Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa kupitia muafaka (Compromise) baina hizi dini kubwa mbili hapa nchini. Ili mambo yaende vizuri nchini ni lazima mzani ukae sawa (The Scale has to balance/Balance of Power). Upande mmoja wa mzani ukionesha unataka kuzidi mwingine tunaishia kupata matatizo makubwa. Changamoto ya hatari zaidi ni kwamba Tanzania ina uzoefu wa kupambana na ukabila, ila siyo udini katika kiwango kikubwa hivi.

Wafuasi wa dini hizi kubwa mbili (Waislamu + Wakristo) hapa nchini wako kwenye kada zote nyeti ndani ya hili taifa na wote wameshatoa hadi maraisi zaidi ya mara moja. Ikionesha kwamba upande mmoja unamwaga ugali mwingine utamwaga mboga. Kiuhalisia tulipofika sidhani kama nchi itakuja kurudi kuwa na ule umoja na kuvumiliana kama zamani (National Cohesion & Tolerance). Hili linaloendelea hapa nchini lilitokea nchini Singapore na linawagharimu hadi leo:

Singapore kuna jamii aina tatu zenye dini zao. Wachina ambao ni wengi ni Buddhists, Wahindi wanaofuatia ni Hindus, na Wamalay ambao ni wachache zaidi ni Muslims. Hizi jamii zilishindwa kuvumiliana kabisa utawala wa Lee Kuan Yew unapoanza, hasahasa Muslims waliwahi kusababisha maandamano makubwa nchini hadi kupelekea nchi kutaka kuanguka. Alikuwa akiingia kiongozi wa Kihindi basi Wachina na Wamalay wanaanza kulalamika na kuleta taharuki za dini na kikabila kwamba wanaonewa.

Mwishowe kabisa Lee-Kuan-Yew kuokoa nchi akaamua kwenda kutafuta watu wa vyombo vya usalama kama polisi kutoka nchi nyingine. Mpaka leo hii nayozungumza Singapore inatumia polisi kutoka nchi ya Nepal waitwao The Ghurkas Regiment. Wangetumia polisi wa nchini kwao na ikatokea polisi wa kichina kamuua muhindi basi matatizo yataanza upya. Leo hii nchini Singapore ukifanya kosa huwezi kuachwa wala kusamehewa. Baada ya huu mkakati kuna watu walijaribu na walikiona cha mtema kuni.

Ukiangalia nje, unaweza kusema Singapore ina maendeleo makubwa kiuchumi, lakini ule upendo wa mtu wa jamii moja au dini nyingine kucheka na mwingine haupo kabisa. Wananchi wameungana kwasababu ya maslahi ya pamoja kiuchumi, ila siyo upendo wa kitaifa. Leo hii Singapore ikifilisika au kukosa uchumi ambao unawaunganisha hawa watu, ni lazima kuchafuke.

Mwalimu Nyerere aliwahi kulizungumzia hili la Singapore miaka ya 90's mwanzoni akihojiwa na vyombo vya habari vya Marekani. Akasema mbali na umasikini wetu ila sisi watanzania tunapendana sana na tunaelewana. Ila leo hii tumeruhusu Bandari imetuvuruga kiasi ambacho tumeyaamsha mambo ambayo yalikuwa yamelala kwa muda mrefu. Hivi kweli uwekezaji wa Bandari ni muhimu kuliko amani ya nchi, ??? Kuna wale ambao wanasema NDIYO...

NB 1: Ila tatizo kubwa zaidi ni vyombo vya dola kuamini kwamba tatizo lolote likitokea nchini basi litaishia humu-humu ndani ya mipaka na watalimaliza. Hili tatizo la bandari halijaanzia Tanzania na kuna wasiwasi wa wahusika wengine kutoka nje ya Tanzania kuhusika na huu mgogoro kwa namna moja ya nyingine. Mambo ni mabaya sana....

 
Acha upuuzi wewe,nyie wachochezi ndio mnatakiwa kushughulikiwa.

Hiyo lugha Huwa unasikia wewe tuu? Mbona Mimi sijawahi sikia wakiongea?

Serikali msiwakalie kimya watu dizaini ya huyu mtoa mada.

Pengine “umeziba masikio”.

Au unasikia tu kile unachopenda sikia.
 
tumia muda wako kufanya mambo ya maana siyo kuja kuandika huu upupu usio na kichwa wala miguu. Hao wanacnhi unakuwaga nao pengine usingizini siyo hawa tunaoishi nao. Inakuwaje mtu na akili zako unakaa unatunga stori za kipuuzi km hizi, nani anakulipa kwa muda ulioupoteza kuandika mambo ya kipuuzi namna hii?
 
upendo wa mtu wa jamii moja au dini nyingine kucheka na mwingine haupo kabisa. Wananchi wameungana kwasababu ya maslahi ya pamoja kiuchumi, ila siyo upendo wa kitaifa.
Siku hizi vijana wa Tanzania wanasema pesa ndio kila kitu.
 
Ukisoma maneno ya mitandao vinywele vinaweza sisimka ukashindwa kutoka hata nje ilihali life linasonga kama kawa na watu wanakula bata.
we unazingatia maupuzi ya kwenye mitandao, yale yaache kule kule, wananchi wetu wengi kwanza hawana muda wa kufuatilia hayo maupuuzi wako kwenye site zao za uzalishaji. Hao ni wale wavivu wachache wanaofikiri kuna serikali itawapelekea mkate nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…