Kuna viashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani siku zijazo…

Me mwenyewe nimechoka na ujinga wa viongozi wa CCM. Bora kibanda kiungue tuanze kukijenga upya
Kibanda kikiungua na wewe huna jeuri hata ya kufika hapo Kenya utakufa kwa mateso makubwa wakati viongozi waliokujaza ujinga kichwani wakiwa Ulaya wanakula kuku kwa mrija.
 
Ndugu wajumbe,

Natumia nafasi hii kama raia mtiifu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwaandikieni nyinyi ikiwa ni sehemu ya wajibu wangu wa kiraia na wa kikatiba (1) Mosi kulinda amani ya nchi (2) Pili Kutoa maoni ya kuleta usitawi kwa nchi yangu (3) kutumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni.

Nawaandikieni barua kwa sababu zifuatazo

1. Kuna viashira na kila dalili kuwa wananchi sasa wameanza kuzungumza lugha ambazo miaka michache iliyopita walikuwa wanajicensor wenyewe, au wanazuiana wenyewe kuzitumia wakiwa wanaona kuwa kulinda amani ni jukumu lao kwa mfano

a) Napitia mitandaoni sana, nasoma comment za watu sana, na kusikiliza sauti zao sana. Zimeanza kuwepo dalili watu kuanza kuzungumza zungumza habari za kutamani mapinduzu ya kijeshi nchini. Watu hawa wanatoa sababu eti, mifumo ya kawaida ya kuendesha nchi imefeli kwenye Checks and balances, wanasema Mahakama, Bunge na serikali vimefunga ndoa haramu na hivyo ni kupoteza muda kutegemea mahakama kusimamia haki pindi kunapokuwepo mgogoro baina ya wananchi na serikali yao au hata bunge lao. Na wanasema kuwa Bunge haliwezi kuizuia serikali kufanya udhalimu dhidi ya wananchi, wanatolea mifano vitendo vya kutisha vya uonevu wa raia dhidi ya wananchi katika hifadhi kama huko Umasaini Ngorongoro, utwaaji wa ardhi Mbarali, Operesheni za kuharibu mali za raia kwa jina la kupanga miji vizuri ( operesheni dhidi ya wamachinga) n.k

2. Wananchi wameanza kuonyesha Dalili za kuona Bunge, Mahakama na serikali si vyombo vyao tena bali ni vya kikundi cha watu wachache wenye masilahi yao.
Wananchi mitandaoni wanasema wazi kuwa Namna Serikali ilivyolithibiti bunge, mfano mzuri kitendo cha Spika wa bunge kuondolewa kwa sababu ya kutoa maoni yake, Na namna Spika wa sasa anavyoliendesha bunge utadhani ni idara tiifu ya mhimili wa Executive( serikali), kwamba yuko tayari kufanya lolote serikali isiwajibishwe bungeni na kwamba amejigeuza kuwa mwanasheria mkuu wa serikali bungeni badala ya kufanya kazi za uspika. Kunawafanya wananchi wengi niliofuatilia michango yao waone kuwa bunge hili si lao bali ni bunge la serikali hususan chama cha Mapinduzi.

Kwa upande wa mahakama, wananchi wanasema, Kitendo cha kuwepo kwa Jaji Mkuu kinyume cha katiba, Na kauli ya Jaji huyo kutamka kuwa "Mahakama ikifanya hukumu iangalie na mihimili mingine inataka nini", badala ya kwamba mahakama iangalie sheria za nchi zinataka nini, nayo pia imepelekea wananchi wengi ninaowasoma kukosa imani kwa mhimili wa mahakama.
Lakini pia ukizingatia na aina ya mashauri na namna mashauri hayo yalivyoendeshwa mahakamani ikiwemo Kesi ya Ugaidi ya Mbowe, Jinsi majaji walivyokuwa wakibadilishwa bila sababu za kuonyesha mashiko za na Jaji mwingine kupandishwa cheo wakati shauri likiendelea ambayo iliyafsirika ni rushwa ya serikali kwa majaji ili wasitende haki. Kimsingi mambo haya yanaondoa imani ya wananchi katika mfumo wa serikali na mahakama.
Lakini pia ongezeko la Mahakama kukwepa wajibu wake wa kutoa haki nchini kwa kutumia mtindo wa "Kutupa kesi za msingi na za haki muhimu za wananchi kirahisirahisi tu based on technicalities". Haya mambo yamepelekea imani ya wananchi kupungua sana kwa mifumo ya kawaida ya kuongoza nchi.

3. Uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 umeacha donda kwa wananchi.

Watu mitandaoni na mitaani hawana imani kuwa wanaweza kuweka serikali waitakayo madarakani kwa Sanduku la kura. Tena hili ni jambo la muhimu sana la kuzingatia. Wananchi wanasema kwamba, kwa mujibu wa katiba hii ya sasa jinsi ilivyo na tume hii jinsi ilivyo, Ni rahisi kuwa abused na wenye madaraka kuminya haki za uchaguzi wa wananchi, wanasema tume inayoteuliwa na mshindani wa wengine katika uchaguzi itakataje mkono ulioipa ulaji?, Sheria zinazokataa matokeo ya urais kupingwa mahakamani, wakitangaza mshindi ambaye si halali then kura zina thamani gani?, Kwamba Ukivuruga uchaguzi halafu una kinga ya kisheria ya kutoshitakiwa kwa hayo unayoyafanya, sasa Uchaguzi una faida gani. Watu wanatoa maoni hayo

4. Wananchi wanalalamikia mnyororo wa kulindana na kutoa nafasi ya watu kuabuse mamlaka.

Ndugu, Wajumbe kwa kadri nilivyofuatilia comments za watu mitandaoni, na katika mazungumzo ya wananchi katika vijiwe vya kahawa. Wananchi wanahoji hii kinga ya Kutoshitakiwa mahakamani ya Jaji Mkuu, Spika, Naibu Spika, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais ya nini?, na Ililenga nini?- Kwa upande wa rais angalau pamoja na kwamba na yenyewe ina shida kwa baadhi ya makosa ikiwemo kwa mfano haki za binadamu za wananchi lakini angalau kwa yale makosa aliyoyatenda huku akitimiza wajibu wake anavumilika kutokana na uzito wa ofisi yake kama mkuu wa nchi. Je hawa wengine nao Kinga ya kutoshitakiwa ya nini?.
Ndugu Wajumbe jambo hili nalo wananchi wanasema ni miongoni mwa mambo yanayopelekeana kulindana kwa mifumo na hivyo kuondoa uwezekano wa wananchi kuheshimiwa na mfumo, ndiyo maana baadhi yao wanazungumzazungumza habari za kuondoa mfumo kwa kutumia nguvu.

5. Imeanza kuwepo minong'ono ya malipizi ya visasi.

Katika pitia yangu mitandaoni, ile ya maandishi na Sauti. Nimeanza kusikia habari za watu kushauriana na kukubaliana kuanza kutumia njia za malipizi ya visasi kwa matendo yanayofanywa na jeshi la polisi.
Watu sasa wameanza kuzungumza habari za "Polisi mnajua wanapokaa mnashindwaje kudeal nao mmojammoja" , "Mnashindwaje magari ya wabunge na mawaziri kuyatia moto", "Tit-for-tat is a fair game". Hizi kauli zimeanza kuwa ni hoja za kushauriana namna ya kudeal na hicho ambacho wanasema ni kudeal na injustice.

6. Kibaya zaidi watu sasa wameanza kuzungumza kuhusu kudeal na viongozi na familia zao.

Ndugu wajumbe wa Baraza la Usalama, hii nukta ninayoizungumza hapa ni muhimu mkaizingatia sana kwa sababu athari zake ni kubwa mno. Katika kusikiliza na kusoma mitandaoni, Watu wameanza kuzungumza na kushauriana kuwa. Maadamu Bunge halipo nao, Maadamu Mahakama haipo nao, Maadamu serikali haiwasikilizi basi njia ya kudeal na watu wenye maamuzi ni kuwapelekea maumivu ili ama wastuke, au wajute au ama watende haki wanayoitaka. Miaka iliyopita, suggestions za hivi zilikuwa zinakataliwa mara moja na wachangiaji wa mada wao wenyewe kwa wenyewe, lakini sasa inaonyesha kuwa thinking ya hivyo imeanza kupenya katika kukubaliana baina ya watu wafanyao mijadala hiyo. Hii ni hatari kubwa sana, Ipo haja ya kulifanyia kazi.

7. Wananchi wameanza kuzungumza kwa sauti za kuukataa muungano, na kudai serikall ya Tanganyika.

Watu kuitaka serikali ya Tanganyika siyo tatizo, lakini Sauti hizi zimeanza kuwa nyingi sana. Na hili limeanza kutokea baada ya watu kuanza kufunguka macho zaidi juu ya muundo wa muungano ambao umekaa kiuzungumkutiuzungumkuti. Watu wanazungumzia muundo wa muungano ambao Katiba za Zanzibar na ya Muungano zinapingans waziwazi kstika issues kadha wa kadha lakini watu wamefukia vichwa vyao udongoni kama mbuni. Watu wanazungumzia kuwa inakuwaje Wazanzibar wawe na Sauti ya kimaamuzi kwenye mambo ya Tanganyika yasiyo ya muungano, wakati Hakuna Mtanganyika anayeweza kuwa na Sauti kwenye mambo ya Zanzibar yasiyo ya muungano. Na pia watu kutoka Zanzibar wanalalamika juu ya Tanfanyika kuvaa koti la muungano.

Ushauri wangu kwa Baraza la Usalama

1. Likae chini lijadili kwa kina na lichukue hatua za kudeal na manung'uniko ya wananchi namna nchi yao inavyoongozwa. Mifumo ya Serikali , Bunge na Mahakama viache "Ushosti". Kila kimoja kifanye kazi kwa uhuru na kwa haki na si kulindana kisiasa

2. Zinahitajika reforms nchini za kuongeza nguvu zaidi kwa wananchi, haki zaidi kwa wananchi,kuweka accountability kwa viongozi na kuondoa impunity ambayo baadhi ya sheria zimewapa watu.

3. Chaguzi ni jambo Sacred katika nchi, Ukiiba kura, au kuchezea chaguzi unazalisha bunge lisilojiamini, unazalisha executive dmbayo haisikilizi raia maana siyo walioiweka madarakani, na hapa lazima migongano mbeleni itokee

4. Baraza lisidharau "Lone actors". Pengine inaweza kudhania kuwa ni rahisi kuthibiti vikundi vyenye kubeba silaha vya watu wengiwengi kwa kutumia taarifa za Intelijensia iliyojisimika ktk society yetu. Lakini Baraza lijue kuwa ni vigumu kudeal na mtu mmojammoja mwenye dhamira yake, aliyeamua kuifanyia mazoezi yeye mwenyewe ili aitekeleze yeye mwenyewe bila kuhusisha "wengi".
Na njia mojawapo ni kuondoa hizi dissatisfactions nyingi miongoni mwa raia.

5. Baraza liishauri serikali iache kamatakamata hizi zisizo na tija, iache hizi bambikizia kesi zisizo na tija. Hivi vitu vinachochea hasira, na vinasaidia kuwafanya watu waamini kuwa njia pekee ya kudeal na watu wa mifumo ni violence ya tit-for-tat

Kwa mapenzi mema ya Taifa langu, na kwa kutimiza wajibu wangu nawasilisha.

Mwenye masikio na asikie!
Wao wanajali mishahara yao 15m na maposho juu
 
Serikali ndio ufanya maisha ya watu yawe magumu,
Serikali ndio uleta tatizo la ajira nchini, kuvuna mabua ni kitu kisichokwepeka
Wewe usisomeshe watoto wako utegemee kuilaumu serikali.

Usitafute ajira kulingana na elimu yako uishie kuilaumu serikali.

Ufuge ujinga kichwani mwako uishie kuilaumu serikali!, tunateketea kwa ukosefu wa maarifa.
 
Yote haya yanakuja wakati rais ni wa kutoka Zanzibar na mwanamama wa kiislam!.

Mmesahau awamu ya tano namna watu walivyopotezwa na kuteswa mchana kweupe?.

Wengine walisulubiwa kwa kupigiliwa misumari miguuni kama Yesu alivyoteswa!.

Suala la DPW ni muendelezo wa sera za awamu ya tano zilizojenga SGR kwa jumla ya trilioni 17, tulitegemea pesa zote hizo mzigo wa kusafirishwa uwe ni mahindi na mihogo?.

Hata JPM alipofanya maamuzi magumu alisema anajua wapo watakaomchukia na wapo watakaofurahishwa na maamuzi yale. Na hiyo ndio sifa ya rais kuamini katika maamuzi unayofanya pasipo kujali kelele za kitanzania.

Mtanzania ni mlalamikaji siku zote, mtendee mema kumi na baya liwe moja tu, atajikita katika kujadili hilo baya moja bila ya kujali uwepo wa mema kumi!. Ni akili za kimaskini sana zinatusumbua.
Hoja mfu kabisa 🚮🚮🚮
 
Nondo ambazo zinaweza kuwa msaada mkubwa kwa serikali.

Lakini mzee Wambura na wenzake wameshajiwekea tafsiri moja tu kwamba kukosoa mienendo isiyofaa ya watawala ni UHAINI.

Wanapaswa kuangalia taathira za kauli na maamuzi yao yasije kuleta donda lisiloponyeka kwa muda mrefu
 
Acha upuuzi wewe,nyie wachochezi ndio mnatakiwa kushughulikiwa.

Hiyo lugha Huwa unasikia wewe tuu? Mbona Mimi sijawahi sikia wakiongea?

Serikali msiwakalie kimya watu dizaini ya huyu mtoa mada.
Mnaomzunguka Hangaya na kumhadaa ndo mnasababisha hizi sintofahamu kushamiri.

Mtaani yanasemwa mengi. Mimi nayasikia na kuyaona.
 
Kwa ground mambo ni tofauti sana.

Maisha yanakuchapa mpaka huoni umuhimu ata wa siasa
Kama ndiyo wewe umepigika na maisha mpaka huoni umuhimu wa siasa basi huna akili kabisa
Ungekuwa na akili japo kidogo basi ungegundua kuwa siasa ndiyo inaathiri maisha

Niko na wanangu hapa wa bodaboda wanalalamika mambo magumu kila ukifanya kazi unaishia tu kununua mafuta,
Mafuta ya elfu 5 hupati hata lita mbili

Nusu ya hela inayopatikana inaishia kwenye mafuta
 
Mtanzania wa kawaida kama mm siasa haina msaada zaidi ya kunitengenezea mazingira magumu kila sector. Kuanzia elimu, hospitali mpaka Uchumi

Ni basi huwez ku opt. Kutojihusisha nazo
 
Wazanzibari ndio wa kwanza kupigia kelele muungano,cha ajabu wabara wakawa vinara wa kuwapinga.
Basi mmepata bahati kwa sababu ya ccm inayoamini katika Fikra sahihi za Mwenyekiti wa CCM hata kama anaiuza nchi kwao sawa maana wanadumisha Chama cha Mapinduzi na wala hawana uchungu na Watanzania.
 
B
Yote haya yanakuja wakati rais ni wa kutoka Zanzibar na mwanamama wa kiislam!.

Mmesahau awamu ya tano namna watu walivyopotezwa na kuteswa mchana kweupe?.

Wengine walisulubiwa kwa kupigiliwa misumari miguuni kama Yesu alivyoteswa!.

Suala la DPW ni muendelezo wa sera za awamu ya tano zilizojenga SGR kwa jumla ya trilioni 17, tulitegemea pesa zote hizo mzigo wa kusafirishwa uwe ni mahindi na mihogo?.

Hata JPM alipofanya maamuzi magumu alisema anajua wapo watakaomchukia na wapo watakaofurahishwa na maamuzi yale. Na hiyo ndio sifa ya rais kuamini katika maamuzi unayofanya pasipo kujali kelele za kitanzania.

Mtanzania ni mlalamikaji siku zote, mtendee mema kumi na baya liwe moja tu, atajikita katika kujadili hilo baya moja bila ya kujali uwepo wa mema kumi!. Ni akili za kimaskini sana zinatusumbua.
Bora akili za kimaskini zinazoamini katika utu na haki ya urithi kuliko akili za kitajiri zinazoamini katika utegemezi,rushwa na ujinga wa kumilikiwa na mwenye pesa.
 
Mnaomzunguka Hangaya na kumhadaa ndo mnasababisha hizi sintofahamu kushamiri.

Mtaani yanasemwa mengi. Mimi nayasikia na kuyaona.
Kama yapi hayo yanayosemwa mengi? Unadhani chuki zako ndio zitabadili nini labda?
 
Wewe usisomeshe watoto wako utegemee kuilaumu serikali.

Usitafute ajira kulingana na elimu yako uishie kuilaumu serikali.

Ufuge ujinga kichwani mwako uishie kuilaumu serikali!, tunateketea kwa ukosefu wa maarifa.
Kwa majority waliosoma na hawana ajira vipi,na Hilo rundo la watu wanaojaa kwenye interview dodoma unasemaje kosa ni la nani.

Kodi komozi, kuzuia watu kwenda nje kufanya kazi,rushwa ufisadi, mipango miji mibovu, kuingia mikataba mibovu, matumizi mabaya ya kodi haya yanafanywa na nani.
 
Hakuna Kodi komozi labda uzitaje

Kujaa watu kwenda kwenye usaili inatokana na Fikra finyu ambazo watu wamekaririshwa kwamba kazi ni lazima za serikali maana humo unakuta watu wanaofanya Private Kwa kujiajiri au kuajiriwa wanataka kuja Serikalini.

Matumizi mabaya ya Kodi ni kama yapi?
Kuna Nchi Haina Rushwa Dunia hii?
Mikataba mibovu ni ipi?

I acknowledge kwenye mipango Miji tuu
 
Kama yapi hayo yanayosemwa mengi? Unadhani chuki zako ndio zitabadili nini labda?
Udhaifu wako ktk mjadala upo too personal.

Mimi napanda daladala, naendq sokoni na pia nakunywa kahawa huku nikiangalia soka la timu za mtaani.

Thubutu kuwa kama mimi kwanza ili uyafehemu ya wananzengo.

Itisheni kura ya maoni leo uone mziki wake. Hata wewe haupo wima na Hangaya unajikosha tu
 
Back
Top Bottom