Kuna viashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani siku zijazo…

Me mbona sioni chochote au kwa kuwa nashinda bar kutwa nzima...naona raia wanakula konyagi,k vant,smart,safari,kilimanjaro,Heineken, savana,caste lite na serengeti...na mara moja moja wanapopata hela wanachoma chama na kucheza mziki...naona wanasikitika tu hawana hela...ila mambo ya sijui mapinduzi au kuandamana ni stories tu kusogesha siku maisha yasonge
Naunga mkono hoja. Hayo machafuko anayo zungumzia mtoa mada ni ya mitandaoni sio kwenye .maisha halisi.
 
Ndugu wajumbe,

Natumia nafasi hii kama raia mtiifu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwaandikieni nyinyi ikiwa ni sehemu ya wajibu wangu wa kiraia na wa kikatiba (1) Mosi kulinda amani ya nchi (2) Pili Kutoa maoni ya kuleta usitawi kwa nchi yangu (3) kutumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni.

Nawaandikieni barua kwa sababu zifuatazo

1. Kuna viashira na kila dalili kuwa wananchi sasa wameanza kuzungumza lugha ambazo miaka michache iliyopita walikuwa wanajicensor wenyewe, au wanazuiana wenyewe kuzitumia wakiwa wanaona kuwa kulinda amani ni jukumu lao kwa mfano

a) Napitia mitandaoni sana, nasoma comment za watu sana, na kusikiliza sauti zao sana. Zimeanza kuwepo dalili watu kuanza kuzungumza zungumza habari za kutamani mapinduzu ya kijeshi nchini. Watu hawa wanatoa sababu eti, mifumo ya kawaida ya kuendesha nchi imefeli kwenye Checks and balances, wanasema Mahakama, Bunge na serikali vimefunga ndoa haramu na hivyo ni kupoteza muda kutegemea mahakama kusimamia haki pindi kunapokuwepo mgogoro baina ya wananchi na serikali yao au hata bunge lao. Na wanasema kuwa Bunge haliwezi kuizuia serikali kufanya udhalimu dhidi ya wananchi, wanatolea mifano vitendo vya kutisha vya uonevu wa raia dhidi ya wananchi katika hifadhi kama huko Umasaini Ngorongoro, utwaaji wa ardhi Mbarali, Operesheni za kuharibu mali za raia kwa jina la kupanga miji vizuri ( operesheni dhidi ya wamachinga) n.k

2. Wananchi wameanza kuonyesha Dalili za kuona Bunge, Mahakama na serikali si vyombo vyao tena bali ni vya kikundi cha watu wachache wenye masilahi yao.
Wananchi mitandaoni wanasema wazi kuwa Namna Serikali ilivyolithibiti bunge, mfano mzuri kitendo cha Spika wa bunge kuondolewa kwa sababu ya kutoa maoni yake, Na namna Spika wa sasa anavyoliendesha bunge utadhani ni idara tiifu ya mhimili wa Executive( serikali), kwamba yuko tayari kufanya lolote serikali isiwajibishwe bungeni na kwamba amejigeuza kuwa mwanasheria mkuu wa serikali bungeni badala ya kufanya kazi za uspika. Kunawafanya wananchi wengi niliofuatilia michango yao waone kuwa bunge hili si lao bali ni bunge la serikali hususan chama cha Mapinduzi.

Kwa upande wa mahakama, wananchi wanasema, Kitendo cha kuwepo kwa Jaji Mkuu kinyume cha katiba, Na kauli ya Jaji huyo kutamka kuwa "Mahakama ikifanya hukumu iangalie na mihimili mingine inataka nini", badala ya kwamba mahakama iangalie sheria za nchi zinataka nini, nayo pia imepelekea wananchi wengi ninaowasoma kukosa imani kwa mhimili wa mahakama.
Lakini pia ukizingatia na aina ya mashauri na namna mashauri hayo yalivyoendeshwa mahakamani ikiwemo Kesi ya Ugaidi ya Mbowe, Jinsi majaji walivyokuwa wakibadilishwa bila sababu za kuonyesha mashiko za na Jaji mwingine kupandishwa cheo wakati shauri likiendelea ambayo iliyafsirika ni rushwa ya serikali kwa majaji ili wasitende haki. Kimsingi mambo haya yanaondoa imani ya wananchi katika mfumo wa serikali na mahakama.
Lakini pia ongezeko la Mahakama kukwepa wajibu wake wa kutoa haki nchini kwa kutumia mtindo wa "Kutupa kesi za msingi na za haki muhimu za wananchi kirahisirahisi tu based on technicalities". Haya mambo yamepelekea imani ya wananchi kupungua sana kwa mifumo ya kawaida ya kuongoza nchi.

3. Uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 umeacha donda kwa wananchi.

Watu mitandaoni na mitaani hawana imani kuwa wanaweza kuweka serikali waitakayo madarakani kwa Sanduku la kura. Tena hili ni jambo la muhimu sana la kuzingatia. Wananchi wanasema kwamba, kwa mujibu wa katiba hii ya sasa jinsi ilivyo na tume hii jinsi ilivyo, Ni rahisi kuwa abused na wenye madaraka kuminya haki za uchaguzi wa wananchi, wanasema tume inayoteuliwa na mshindani wa wengine katika uchaguzi itakataje mkono ulioipa ulaji?, Sheria zinazokataa matokeo ya urais kupingwa mahakamani, wakitangaza mshindi ambaye si halali then kura zina thamani gani?, Kwamba Ukivuruga uchaguzi halafu una kinga ya kisheria ya kutoshitakiwa kwa hayo unayoyafanya, sasa Uchaguzi una faida gani. Watu wanatoa maoni hayo

4. Wananchi wanalalamikia mnyororo wa kulindana na kutoa nafasi ya watu kuabuse mamlaka.

Ndugu, Wajumbe kwa kadri nilivyofuatilia comments za watu mitandaoni, na katika mazungumzo ya wananchi katika vijiwe vya kahawa. Wananchi wanahoji hii kinga ya Kutoshitakiwa mahakamani ya Jaji Mkuu, Spika, Naibu Spika, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais ya nini?, na Ililenga nini?- Kwa upande wa rais angalau pamoja na kwamba na yenyewe ina shida kwa baadhi ya makosa ikiwemo kwa mfano haki za binadamu za wananchi lakini angalau kwa yale makosa aliyoyatenda huku akitimiza wajibu wake anavumilika kutokana na uzito wa ofisi yake kama mkuu wa nchi. Je hawa wengine nao Kinga ya kutoshitakiwa ya nini?.
Ndugu Wajumbe jambo hili nalo wananchi wanasema ni miongoni mwa mambo yanayopelekeana kulindana kwa mifumo na hivyo kuondoa uwezekano wa wananchi kuheshimiwa na mfumo, ndiyo maana baadhi yao wanazungumzazungumza habari za kuondoa mfumo kwa kutumia nguvu.

5. Imeanza kuwepo minong'ono ya malipizi ya visasi.

Katika pitia yangu mitandaoni, ile ya maandishi na Sauti. Nimeanza kusikia habari za watu kushauriana na kukubaliana kuanza kutumia njia za malipizi ya visasi kwa matendo yanayofanywa na jeshi la polisi.
Watu sasa wameanza kuzungumza habari za "Polisi mnajua wanapokaa mnashindwaje kudeal nao mmojammoja" , "Mnashindwaje magari ya wabunge na mawaziri kuyatia moto", "Tit-for-tat is a fair game". Hizi kauli zimeanza kuwa ni hoja za kushauriana namna ya kudeal na hicho ambacho wanasema ni kudeal na injustice.

6. Kibaya zaidi watu sasa wameanza kuzungumza kuhusu kudeal na viongozi na familia zao.

Ndugu wajumbe wa Baraza la Usalama, hii nukta ninayoizungumza hapa ni muhimu mkaizingatia sana kwa sababu athari zake ni kubwa mno. Katika kusikiliza na kusoma mitandaoni, Watu wameanza kuzungumza na kushauriana kuwa. Maadamu Bunge halipo nao, Maadamu Mahakama haipo nao, Maadamu serikali haiwasikilizi basi njia ya kudeal na watu wenye maamuzi ni kuwapelekea maumivu ili ama wastuke, au wajute au ama watende haki wanayoitaka. Miaka iliyopita, suggestions za hivi zilikuwa zinakataliwa mara moja na wachangiaji wa mada wao wenyewe kwa wenyewe, lakini sasa inaonyesha kuwa thinking ya hivyo imeanza kupenya katika kukubaliana baina ya watu wafanyao mijadala hiyo. Hii ni hatari kubwa sana, Ipo haja ya kulifanyia kazi.

7. Wananchi wameanza kuzungumza kwa sauti za kuukataa muungano, na kudai serikall ya Tanganyika.

Watu kuitaka serikali ya Tanganyika siyo tatizo, lakini Sauti hizi zimeanza kuwa nyingi sana. Na hili limeanza kutokea baada ya watu kuanza kufunguka macho zaidi juu ya muundo wa muungano ambao umekaa kiuzungumkutiuzungumkuti. Watu wanazungumzia muundo wa muungano ambao Katiba za Zanzibar na ya Muungano zinapingans waziwazi kstika issues kadha wa kadha lakini watu wamefukia vichwa vyao udongoni kama mbuni. Watu wanazungumzia kuwa inakuwaje Wazanzibar wawe na Sauti ya kimaamuzi kwenye mambo ya Tanganyika yasiyo ya muungano, wakati Hakuna Mtanganyika anayeweza kuwa na Sauti kwenye mambo ya Zanzibar yasiyo ya muungano. Na pia watu kutoka Zanzibar wanalalamika juu ya Tanfanyika kuvaa koti la muungano.

Ushauri wangu kwa Baraza la Usalama

1. Likae chini lijadili kwa kina na lichukue hatua za kudeal na manung'uniko ya wananchi namna nchi yao inavyoongozwa. Mifumo ya Serikali , Bunge na Mahakama viache "Ushosti". Kila kimoja kifanye kazi kwa uhuru na kwa haki na si kulindana kisiasa

2. Zinahitajika reforms nchini za kuongeza nguvu zaidi kwa wananchi, haki zaidi kwa wananchi,kuweka accountability kwa viongozi na kuondoa impunity ambayo baadhi ya sheria zimewapa watu.

3. Chaguzi ni jambo Sacred katika nchi, Ukiiba kura, au kuchezea chaguzi unazalisha bunge lisilojiamini, unazalisha executive dmbayo haisikilizi raia maana siyo walioiweka madarakani, na hapa lazima migongano mbeleni itokee

4. Baraza lisidharau "Lone actors". Pengine inaweza kudhania kuwa ni rahisi kuthibiti vikundi vyenye kubeba silaha vya watu wengiwengi kwa kutumia taarifa za Intelijensia iliyojisimika ktk society yetu. Lakini Baraza lijue kuwa ni vigumu kudeal na mtu mmojammoja mwenye dhamira yake, aliyeamua kuifanyia mazoezi yeye mwenyewe ili aitekeleze yeye mwenyewe bila kuhusisha "wengi".
Na njia mojawapo ni kuondoa hizi dissatisfactions nyingi miongoni mwa raia.

5. Baraza liishauri serikali iache kamatakamata hizi zisizo na tija, iache hizi bambikizia kesi zisizo na tija. Hivi vitu vinachochea hasira, na vinasaidia kuwafanya watu waamini kuwa njia pekee ya kudeal na watu wa mifumo ni violence ya tit-for-tat

Kwa mapenzi mema ya Taifa langu, na kwa kutimiza wajibu wangu nawasilisha.

Mwenye masikio na asikie!
Point. Acha waendelee kuziba masikio
 
Kweli kabisa,yeye kila siku ni kunyonya damu za viumbe wenzie.
Na sababu anategemea kuishi juu ya mgongo wa mwingine haoni haja ya kupambana na maisha
Asipo uwawa na yule anayemnyonya damu atakufa juu ya kiumbe huyo ikiwa kiumbe uyo atakufa
Dawa na kibamiza uko wanakotoa damu
 
Kama ni wanyama basi watanzania wengi ni Kondoo na Ngamia. Ni wapole, wavumilivu sana, wasikivu na kikubwa zaidi walichojaaliwa wamekuwa ni watu WAKUSHANGAA TU BASI.
Kwa hiyo hizo vurugu na machafuko haziwezi kutokea nchi hii kwasababu watanzania wameridhika sana na maisha yao. Katika nchi nzuri za kutawala ni pamoja na Tanzania ,yaani utasikia tu wananchi wakisema jamani hivi ni kwanini inakuwa hivi, tunamuachia Mungu tu.
 
Wewe nae ni juha tu. Unadhani wao hawana surveillance report hadi uwaambie wewe..?? Watu wana briefings za every 12 hours, detailed reported, ndo waje wapokee barua za kipopoma hizo kutoka JF. Mnakuwaga na viherehere kweli. Hii nchi iko salama kuliko mnavyoweza kudhani, people are working tirelessly 24/7.
 
Mtu aache kutafuta mlo wake aende kuandamana mitaani, hakuna mwenye muda huo.
 
Barua inajitosheleza yenyewe, hakuna cha ziada cha kuongezea hapo.

Tatizo tu ni hao wanaoandikiwa hiyo barua:"Baraza la Usalama la Taifa"?

Ni akina nani hawa. Wanayo tofauti gani na hawa wengine, kama Spika wa Bunge au 'Chief Justice' wa nchi hii?

Hii barua ingeandikwa kuelekezwa kwa Spika au Jaji Mkuu ingeleta maana yoyote kwa watu hao?

Kwa hiyo, kwa maoni yangu ni kuwa, hii barua hasa imelengwa kwa wananchi wa nchi hii. Hawa ndio walioandikiwa barua yenye maana kubwa sana kwa nchi yao.

Ikimpendeza mwandishi wa barua hii, aibadilishe na kuielekeza kwa wahusika, wananchi wenyewe.
Hawa ndio wanaoshikilia hatma ya nchi hii mikononi mwao.

Siwezi kunyamaza, bila kumpongeza mwandishi wa barua hii, amabye, pamoja na kuwa na mashaka naye kwa wakati fulani, sasa kajipambanua wazi kabisa kuwa ni mtu anayejali maslahi ya nchi hii kwa kila hali bila kujali matabaka yaliyomo katika jamii yeyu.

Ahsante sana mkuu 'Missile of the Nation', kwa uzalendo wako.
 
Wewe nae ni juha tu. Unadhani wao hawana surveillance report hadi uwaambie wewe..?? Watu wana briefings za every 12 hours, detailed reported, ndo waje wapokee barua za kipopoma hizo kutoka JF. Mnakuwaga na viherehere kweli. Hii nchi iko salama kuliko mnavyoweza kudhani, people are working tirelessly 24/7.
Tukuamini wewe kwa sababu zipi hasa, kwa kuandika hapa vimistari vitatu, tena visivyokuwa na maana yoyote?
Sasa sikiliza, hivyo visenti vya waarabu visikutie upofu na kushindwa kuona alama za nyakati.
Kiyama chenu kinakuja. Safari hii hamponi, ng'oo!
 
Ningekuwa moderator ningeku BAN life kabisa hapa JF. Watu ka ninyi sijui kwa nini mlizaliwa. Muacheni Mama afanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania. Bila CCM hakuna amani, ndiyo maana tunaendelea kushinda chaguzi zote.

We ni choko kama choko tu, Mama amekuwa Mungu asiambiwe anakosea wapi, acha kujitegua bolt akilini, Mama ako mwambie aone ya kuwa wanainchi hatulizishwi na Namna vile anavyoiongoza, Nchi inanuka ufisadi kila Sehemu na amekaa kimya.

Wapumbavu kama ninyi Mnaishushia heshima hii platform.
 
Ningekuwa moderator ningeku BAN life kabisa hapa JF. Watu ka ninyi sijui kwa nini mlizaliwa. Muacheni Mama afanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania. Bila CCM hakuna amani, ndiyo maana tunaendelea kushinda chaguzi zote.
Na wewe ni walewale nani aliyekuambia kwamba bila CCM hakuna amani. Vurugu na uvunjifu wa amani utaletwa na CCM ,maana nyinyi hamtaki kushindwa kupitia sanduku la kura.
Mkizidiwa mnatumia vyombo vya dola kupora uchaguzi.
IMG_20230326_120630.jpg

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Acha upuuzi wewe,nyie wachochezi ndio mnatakiwa kushughulikiwa.

Hiyo lugha Huwa unasikia wewe tuu? Mbona Mimi sijawahi sikia wakiongea?

Serikali msiwakalie kimya watu dizaini ya huyu mtoa mada.
Mambo Kama hapo na yameanza kusemwa semwa sana siku hizi acha kumtisha mtoa maada
Yeye ameshauri tu ,Wala hajavunja sheria yeyote.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Tukuamini wewe kwa sababu zipi hasa, kwa kuandika hapa vimistari vitatu, tena visivyokuwa na maana yoyote?
Sasa sikiliza, hivyo visenti vya waarabu visikutie upofu na kushindwa kuona alama za nyakati.
Kiyama chenu kinakuja. Safari hii hamponi, ng'oo!
Wewe endelea kujificha nyuma ya keyboard muone kama hayo mabadiriko mtayapata.
 
CHAWA maana yake ni uchafu, uadui, chukii, unyonyaji, kujipatia kipato kisicho halali na kisababishi cha hasara ya kiuchumi, kiafya na kiusalama.

Kama unajiita wewe ni chawa basi sifa zako na tabia zako ni hizo hapo juu
Liambie hilo duduna
 
Kuna mambo Mimi yananishangaza hata sielewi kwa kweli!! Kwa nini issue ya bandari ilete machafuko makubwa kiasi hichi? Eti vita vya kiuchumi? How? Kama tungekuwa tunajenga wenyewe then mtanzania akatuinukia hapo ningesema vita vya kiuchumi!! Kama vile tulivyoamua kujenga Bwawa la nyerere then watanzania fulani wakatuinukia .hii kweli ilikuwa vita ya kiuchumi.Sasa hatika vita hii tunapambana na Nani? Ili iweje?tumeishi kwa amani kwa miaka mingi bila ufanisi mkubwa wa bandari.tufahamu kuwa unaweza kuwa tajiri lakini ukakosa amani,ukakosa pakutembelea na gari lako la kifahari. Tunavutana pasipo sababu yoyote.unless Kuna hidden ajenda .nasikia kulia nionapo Jambo dogo linapotaka kuleta sintofahamu.

Maybe we need national dialogue
 
Wewe endelea kujificha nyuma ya keyboard muone kama hayo mabadiriko mtayapata.
Haya hayazuiliki, imebaki ni lini tu.
Kama unayo akili timamu, lipeleke hilo benki ukadai kitata chako, kwa sababu ni la uhakika.

Sasa naelewa wazi, huwezi kujua nilichoandika hapa kutokana na ufinyo wa akili yako.
 
Back
Top Bottom