Kuna video inasambaa mitandaoni, kiingereza kwa Watanzania wengi ni shida sana!!

Kuna video inasambaa mitandaoni, kiingereza kwa Watanzania wengi ni shida sana!!

Naishia hapa, uzi umevamiwa na majuha wengi wanateteana ujinga!!
 
Mdada ni Mnigeria ana pikipiki zile za masafa marefu, yupo mpakani kasimamishwa na wana mamlaka wetu. Wakaanza kuongea nae kiingereza, aibu nimeona mimi.

Mdada ana camera kaifunga nadhani kwenye pikipiki so alikuwa anarekodi matukio na kuyapost mtandaoni.

Tusomeshe watoto jamani dunia ya sasa kiingereza hakiepukiki
Mjerumani, mjapani, mfaransa, mhindi, mreno wote hao hawajui kuongea vizuri kiingereza.

Ukiona mtu anaongea vibaya lugha, ujue ana lugha yake mama. Sisi kiswahili chetu kinatosheleza kuwasiliana, kwanini tuangaike na lugha zingine?
 
Pamoja na kwamba kiingereza ni lugha muhimu, namna tunavyokichukulia ni utumwa mtupu. Wachina wanakuja hapa kiingereza tia maji tia maji, kiswahili 'not reachable'; na bado wanatupiga hela!!
 
Mdada ni Mnigeria ana pikipiki zile za masafa marefu, yupo mpakani kasimamishwa na wana mamlaka wetu. Wakaanza kuongea nae kiingereza, aibu nimeona mimi.

Mdada ana camera kaifunga nadhani kwenye pikipiki so alikuwa anarekodi matukio na kuyapost mtandaoni.

Tusomeshe watoto jamani dunia ya sasa kiingereza hakiepukiki
Kuna wachina,Wahindi,hawajui Kingereza na still wana make money, Kingereza ni lugha wewe pimbi hakina uhusiani ba kusomesha
 
Walikuwa much nicer kwakuwa tu yai linawachenga! Awaulize wapinzani wa nchi hii.

Wapinzani nao wangekuwa wanaendesha kampeni kwa yai polisisiem wangekuwa watu wapole na wastaarabu zaidi nchi hii
Siku jaa halafu ongea kiingereza mwanzo mwisho.

Ndio utajua police wanaelewa lugha zote duniani😂😂😂
 
ukishaona kada inapokea ma 4m4 felia hata wenye ziro wamo basi hapo hakuna kazi.....

alisikika njagu mmoja akisema i am not your friend my friend
 
Mjerumani, mjapani, mfaransa, mhindi, mreno wote hao hawajui kuongea vizuri kiingereza.

Ukiona mtu anaongea vibaya lugha, ujue ana lugha yake mama. Sisi kiswahili chetu kinatosheleza kuwasiliana, kwanini tuangaike na lugha zingine?
Hapa ndo umeandika nini? Usipende kukurupuka, soma uzi wangu uelewe vizuri wewe kiazi
 
Mdada ni Mnigeria ana pikipiki zile za masafa marefu, yupo mpakani kasimamishwa na wana mamlaka wetu. Wakaanza kuongea nae kiingereza, aibu nimeona mimi.

Mdada ana camera kaifunga nadhani kwenye pikipiki so alikuwa anarekodi matukio na kuyapost mtandaoni.

Tusomeshe watoto jamani dunia ya sasa kiingereza hakiepukiki
Kwanini usidhangae huyo mdada kujaribu kuongea Kiswahili??.

Hivi Ubongo zenu mmezijaza matope ???.
 
alokwambia kingereza dili ni nani??
dunia haiongee kingereza babu ushamba wako tu !
Ujerumani wanaongea kijeruman
Ufaransa wanaongea kifaransa
China wanaongea mandarin
India ndo balaaa wanalugha kibao lakin si kingereza
Japan kijapan

Dunia nzima wanaoongea kingereza 1.5Bilion na duniani tupo bilioni 8
Haya akili kumkichwa na Kasumba yako
Huwezi kupita mpaka rasmi wa nchi yoyote (incl. bandari na uwanja wa ndege) ukute askari na maafisa wasiojua kiingereza.
 
Huwezi kupita mpaka rasmi wa nchi yoyote (incl. bandari na uwanja wa ndege) ukute askari na maafisa wasiojua kiingereza.
una uhakika mpaka tati ya tunisia na aljeria sheria ni kujua kingereza,
China na north korea,?
mpaka wa yemeni na oman
yemeni na Saudi Arabia

Mkuu ebu jielimishe basi
 
una uhakika mpaka tati ya tunisia na aljeria sheria ni kujua kingereza,
China na north korea,?
mpaka wa yemeni na oman
yemeni na Saudi Arabia

Mkuu ebu jielimishe basi
Wewe nafikiri huna experience ya kimataifa kabisa. Unaweza kuwa mdogo sana. Unafikiri hiyo mipaka wanapita watu wa nchi hizo tu? Hata katika safari za ndege kati ya hizo nchi huwa na raia wa kigeni. Hata katika safari za ndani.

Mimi sio mtu wa leo ni wa enzi. Nimesafiri kati ya Aljeria, Tunisia na Morocco mara kadhaa. Najua Kifaransa cha kutosha lakini nimetumia kingereza sana katika nchi hizo katika kazi zangu. Ungeandika pia mpaka wa Senegal na Mali useme kama kiingereza hakipo. Ukienda Dakar sokoni hata kina mama ntilie na wanaouza batiki wana kiingereza cha kutosha. Wanawasiliana na watalii vizuri tu.

Kiingereza kinatumika vizuri sana serikalini na katika circles za wasomi huko Yemen, Oman na Saudi Arabia. Btw Kiingereza ndiyo lugha ya sekta ya usafiri wa anga (aviation language) duniani.

Sijui kama unaifahamu China ya leo. Sio kiingereza tu. Vijana wa Kichina wanajifunza lugha zote kubwa za Ulaya kama kazi. Nilikuwa nao katika timu wakati fulani tulipotembelea Equatorial Guinea. Walitusaidia sana kuwasiliana na Waafrika wenzetu kwa KiSpanish. Halafu unaleta mambo ya North Korea? Nani anaenda huko hermit kingdom?

Sitashangaa wewe ukiwa ni mmoja wa wanaoamini kuwa maRais wa China, Urusi na Ufaransa na Chancellor wa Ujerumani hawajui kiingereza. Unaweza kuwa mdogo sana unasikiliza kelele za wanasiasa wa nchi hii. Dunia imebadilika sana. Ni aibu kwamba Kenya ndio wameteka soko la kufundisha Kiswahili duniani. Kwingine vijana wa DRC wanafanya kazi hiyo.

Watanzania wengi hawana uwezo wa kufundisha mataifa mengine Kiswahili kwa vile wao hawawezi kuwasiliana na hao watu kwa lugha zao au kwa kiingereza ambacho ni universal. Imagine mtu wa DRC anafundisha Kiswahili katika shule huko Pretoria SA akitumia Kiswahili na Kiingereza ilhali yeye kasoma kwa kifaransa hadi chuo kikuu!

Huwa nasikitika sana wanasiasa wanapowajaza vijana false confidence kuwa Kiswahili pekee kinawatosha! Ni unafiki wa hali ya juu. Ni kuwaweka gizani wasiwe na uwezo wa kusaka maarifa na fursa zaidi duniani. Ajabu, hata Kiswahili chenyewe wanakiua kwa ufundishaji mbovu. Sijui lengo ni lipi hasa?
 
Back
Top Bottom