una uhakika mpaka tati ya tunisia na aljeria sheria ni kujua kingereza,
China na north korea,?
mpaka wa yemeni na oman
yemeni na Saudi Arabia
Mkuu ebu jielimishe basi
Wewe nafikiri huna experience ya kimataifa kabisa. Unaweza kuwa mdogo sana. Unafikiri hiyo mipaka wanapita watu wa nchi hizo tu? Hata katika safari za ndege kati ya hizo nchi huwa na raia wa kigeni. Hata katika safari za ndani.
Mimi sio mtu wa leo ni wa enzi. Nimesafiri kati ya Aljeria, Tunisia na Morocco mara kadhaa. Najua Kifaransa cha kutosha lakini nimetumia kingereza sana katika nchi hizo katika kazi zangu. Ungeandika pia mpaka wa Senegal na Mali useme kama kiingereza hakipo. Ukienda Dakar sokoni hata kina mama ntilie na wanaouza batiki wana kiingereza cha kutosha. Wanawasiliana na watalii vizuri tu.
Kiingereza kinatumika vizuri sana serikalini na katika circles za wasomi huko Yemen, Oman na Saudi Arabia. Btw Kiingereza ndiyo lugha ya sekta ya usafiri wa anga (aviation language) duniani.
Sijui kama unaifahamu China ya leo. Sio kiingereza tu. Vijana wa Kichina wanajifunza lugha zote kubwa za Ulaya kama kazi. Nilikuwa nao katika timu wakati fulani tulipotembelea Equatorial Guinea. Walitusaidia sana kuwasiliana na Waafrika wenzetu kwa KiSpanish. Halafu unaleta mambo ya North Korea? Nani anaenda huko hermit kingdom?
Sitashangaa wewe ukiwa ni mmoja wa wanaoamini kuwa maRais wa China, Urusi na Ufaransa na Chancellor wa Ujerumani hawajui kiingereza. Unaweza kuwa mdogo sana unasikiliza kelele za wanasiasa wa nchi hii. Dunia imebadilika sana. Ni aibu kwamba Kenya ndio wameteka soko la kufundisha Kiswahili duniani. Kwingine vijana wa DRC wanafanya kazi hiyo.
Watanzania wengi hawana uwezo wa kufundisha mataifa mengine Kiswahili kwa vile wao hawawezi kuwasiliana na hao watu kwa lugha zao au kwa kiingereza ambacho ni universal. Imagine mtu wa DRC anafundisha Kiswahili katika shule huko Pretoria SA akitumia Kiswahili na Kiingereza ilhali yeye kasoma kwa kifaransa hadi chuo kikuu!
Huwa nasikitika sana wanasiasa wanapowajaza vijana
false confidence kuwa Kiswahili pekee kinawatosha! Ni unafiki wa hali ya juu. Ni kuwaweka gizani wasiwe na uwezo wa kusaka maarifa na fursa zaidi duniani. Ajabu, hata Kiswahili chenyewe wanakiua kwa ufundishaji mbovu. Sijui lengo ni lipi hasa?