Usalama wa Taifa wapo wengi sana na si ajabu. Wengine ni bodaboda, wakulima, walimu, wafanyakazi wa serikali, mapadre, wachungaji, mashekhe etc. Kazi yao wengi mnao wajua ni kupeleka tu taarifa kuhusu mambo mbali mbali mengine ya maana na mengine yanakuwa hayana hata maana. Kuna watu kwenye idara za serikali huwa wanaombwa kufanya kazi hiyo ya kukusanya taarifa na kuziwasilisha lakini hakuna lolote special kuanzia mishahara, mafunzo, elimu etc.
Watu wakisikia Usalama wa Taifa wanadhani ni dude flani lenye watu shupavu, geniuses, patriotic etc. Ni hao hao walimu wenzenu, wakulima wenzenu, bodaboda wa kawaida, Watumishi wa Mungu etc. Ndiyo maana hata hapa jukwani unaweza kuta kila member anawafahamu walau watu watano wa Usalama wa Taifa. Ila ifahamike kuwa wapo Usalama wa Taifa original ambao wana mafunzo na wameajiriwa rasmi kwa ajili ya kazi hiyo tofauti na hawa ambao mleta mada kawalenga ambao kimsingi ndio wengi.