Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?

Kuna viongozi wengi ni Usalama wa Taifa!?

Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa 💯 ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.
Wengine ni akina nani?
Kwangu , watanzania wote ni Usalama wa Taifa, sema kuna wachache wanalipwa mshahara na sisi hatulipwi lakini tukiona uhalifu ama mtu anataka kutenda uhalifu tunatoa taarifa Polisi, kwahiyo sote ni usalama.
 
Wengine ni akina nani?
Kwangu , watanzania wote ni Usalama wa Taifa, sema kuna wachache wanalipwa mshahara na sisi hatulipwi lakini tukiona uhalifu ama mtu anataka kutenda uhalifu tunatoa taarifa Polisi, kwahiyo sote ni usalama.
Ila mara nyingine unaweza kutoa taarifa halafu................
 
Usalama wa Taifa wapo wengi sana na si ajabu. Wengine ni bodaboda, wakulima, walimu, wafanyakazi wa serikali, mapadre, wachungaji, mashekhe etc. Kazi yao wengi mnao wajua ni kupeleka tu taarifa kuhusu mambo mbali mbali mengine ya maana na mengine yanakuwa hayana hata maana. Kuna watu kwenye idara za serikali huwa wanaombwa kufanya kazi hiyo ya kukusanya taarifa na kuziwasilisha lakini hakuna lolote special kuanzia mishahara, mafunzo, elimu etc.
Watu wakisikia Usalama wa Taifa wanadhani ni dude flani lenye watu shupavu, geniuses, patriotic etc. Ni hao hao walimu wenzenu, wakulima wenzenu, bodaboda wa kawaida, Watumishi wa Mungu etc. Ndiyo maana hata hapa jukwani unaweza kuta kila member anawafahamu walau watu watano wa Usalama wa Taifa. Ila ifahamike kuwa wapo Usalama wa Taifa original ambao wana mafunzo na wameajiriwa rasmi kwa ajili ya kazi hiyo tofauti na hawa ambao mleta mada kawalenga ambao kimsingi ndio wengi.
Ingekuwa enzi zetu.......kijiweni kwetu ningesema....mama tupimie pombe nyingine.....
 
Hata Wewe ni usalama wa Taifa

Kuwa Mzalendo 😀
Kila raia au mwananchi anayejielewa lazima alinde usalama wa taifa lake iwe directly au indirectly.
Hii ni muhimu kwa sababu kuna wakati mwingine wanaoitwa usalama wa taifa hugeuka kuwa maadui wa taifa na hivyo kulazimika kuondoshwa kwa gharama yoyote.
 
Kuna viongozi wengi sana ambao ni usalama wa taifa. Mmoja ambaye nina uhakika naye kwa 💯 ni Professor Mkumbo ambaye ni waziri kwa sasa. Miaka yote hata kabla ya kuingia Chadema alikuwa usalama wa taifa.

Tanzania Usalama wa Taifa wapo kila kona. Kuanzia kwenye Vyama, Makanisani, Misikitini, Vyuoni, Mashuleni, Machinga, Bodaboda ..... Kila eneo wamekaba.
 
Hivi mbona mnautukuza sana huo usalama wa Taifa?
Wangekuwa wa maana kwa rasilimali hizi tusingekuwa nà raia waonalala nyumba moja na mbuzi.
TISS is overrated, nothing more.
Tiss wetu mentally wapo kutulinda na ndicho wanachojitahidi(usalama nje na ndani)

Lakini jukumu la kutafuta fursa wamechemka, au sijui wanaona labda sio jukumu Lao.

Mf: ishu ya Rwanda kuitupa bandari yetu na kuhamia kenya ilibidi waijue mapema na kufanya Well calculated move.

Wameshindwa kuupenyeza mziki wetu globally, tumeishia kupata mtu mmoja(Diamond) ambae na yeye anachechemea, tiss walishindwa vipi kuupenyeza mxiki wetu kimataifa kama wanigeria? Kazi hii tiss walitakiwa waifanye kipindi wanigeria wanaanza kutoboa ingebidi watoboe na wabongo kwa pamoja coz kipindi kile mziki wetu na wao tulikua sawa tu.
 
Mkuu Mundu, Kamundu , kwa lengo la kusaidiana tuu, kukusaidia wewe na wengine wasiojua, kumtaja kwa majina mtu yoyote wa TISS na kumu expose kuwa ni TISS, huyo mtu akiwa ni TISS kweli, then kumtaja kwa jina ni kosa la jinai!.

I can just imagine, kama sisi tuliajaliwa jicho la tatu, ma Tiss tunawajua kwa kuwaona tuu sura, je tungewataja ma Tiss wote tunaowajua, tungebaki salama?
Huwezi kutoboa boti mnayasafiria. Ikizama mnakufa wote!, au kulikata tawi la mti uliolalia!.

Kwa taarifa yako ma TISS ni wengi kuliko unavyodhania hata Sultani naye ni Tiss, hata Mkuu nanilii pia ni Tiss
Ila sio kila Tiss ni Tiss

Kuna Tiss wa aina 3.
  1. Staff hawa ni waajiriwa, wafanyakazi wa Tiss, ni watumishi wa mishahara, hawa staff wako wa aina mbili, kuna open staff, hawa wanajulikana kama DGIS na maofisa wote wa TISS wanaojulikana kama RSO, ma DSO etc, hawa kuwataja hakuna tatizo, ila kuna ma SS, secret service, hawa hawatakiwi kujulikana, na ikitokea ukawajua, huruhusiwi kuwataja!.
  2. Viongozi wote, wateuliwa wote na watendaji wote, hawa ni ma Tiss kwa mujibu wa positions zao, wakiwemo mabenki yote yana mtu wa kitengo cha FIU hawa ni ma TISS, taarifa ya FIU lazima ipite kwa bank manager hivyo mameneja wote wa financial institutions zote ni ma Tiss.
  3. Informers, hawa ni watu wa kawaida wanakuwa recruited kuripoti Tiss na kulipwa posho tuu, huku wakiendelea na shughuli zao.
NB. Mimi nina damu ya TISS kwenye veins zangu kwa wazazi wangu wote wawili, na tumezaliwa 8, haiwezekani sisi wote nane tukawamo!. Kunidhania mimi ni mmoja wao rukhsa na angalia hapa ninavyoisifia ofisi yangu TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Hapa namtishia bosi wangu Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Na kunapotokea matishio ya kiusalama, badala ya kuripoti ofisini, mimi naripoti jf Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

P.
Njaa itakuua na hawakuoni
 
Back
Top Bottom