Pre GE2025 Kuna vita ya chinichini inaendelea dhidi ya viongozi wa dini wanaokosoa Serikali
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kwanini wanapotosha, kwanini hakuna anayeweka uthibitisho wa video habari hii ya madai kuwa Tundu Lissu amethibitisha Padre Dkt. Charles Kitima kushiriki vikao vya siri vya CHADEMA?

Katika video ya mahojiano na Waandishi wa Habari pale Uwanja wa Ndege hakuna mahali Lissu amemtaja Kitima lakini namna imeripotiwa ni kama viongozi wa dini hawapaswi kufanya upatanishi.

Hata hivyo ukifuatilia wote waliotoa habari hii maelezo yao ni copy and paste mwanzo mwisho kuonesha script waliyopewa ni moja.

Halafu kama kikao walichoshiriki ni kikao cha upatanisho kuna ubaya gani wao kushiriki? Maana yeyote waliyemuona na busara za kuwapatanisha ndiye aliyealikwa kwanini wahusishe na kuiponda serikali?

Lakini pia kama wanakemea uovu unaofanywa na viongozi serikalini kuna tatizo gani? Kwani kazi ya vyombo vya dini ni kusifia tu viongozi na serikali na siyo kukosoa pale wanapoona mambo hayaendi vizuri?

Hiki ndicho Lissu alizungumza

==

IMG_2362.jpeg

Katika tukio lililotokea jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, amethibitisha hadharani kuwa Fr. Charles Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), alihudhuria vikao vya siri vya chama hicho vilivyofanyika katika ukumbi mdogo wa Macapuchino ulioko eneo la kanisa, Msimbazi Centre, jijini Dar es Salaam.

Mwanzoni mwa mwezi Desemba, taarifa za ndani zilisambaa zikidai kuwa Fr. Kitima, Kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki, alihusishwa moja kwa moja na vikao vya CHADEMA.

Taarifa hizo zilizua mijadala mitandaoni, huku baadhi ya wadau wakitilia shaka ukweli wake na wengine wakihoji nafasi ya kiongozi huyo wa kidini katika siasa za vyama.

Hata hivyo, jana Lissu amekiri waziwazi ushiriki huo, akiondoa shaka kuhusu madai hayo ambayo awali yalionekana kama uzushi.

Ukaribu wake na Fr. Kitima unatokana na ukweli kwamba wote wanatoka kijiji kimoja mkoani Singida. Ukaribu huu, kulingana na vyanzo vya karibu, umesababisha Fr. Kitima kuwa mmoja wa wapangaji wakuu wa mikakati ya kampeni za Lissu na hatua za kuipinga serikali.

Uthibitisho huu umetajwa kama "kuvuliwa nguo kwa kanisa," huku baadhi ya wadau wakidai kuwa hatua ya Lissu kufichua ushiriki wa Katibu wa TEC katika siasa za vyama imeweka wazi mgongano wa maadili unaohusiana na nafasi ya viongozi wa dini katika masuala ya kisiasa.

Kanisa Katoliki linatakiwa kutoa tamko rasmi kufuatia kauli ya Lissu, ingawa mjadala mkubwa umeibuka mitandaoni, huku waumini na wadau wa siasa wanakosoa hatua hiyo kama kinyume na maadili ya kidini.

Tukio hili linaongeza mvutano kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika siasa za Tanzania.
IMG_2361.jpeg

IMG_3035.jpeg
IMG_3036.jpeg
IMG_3037.jpeg

IMG_3038.jpeg
 
Padre kitima apongezwe endapo kama kweli alihusika kwenye suala hili. kupatanisha watu ni ibada takatifu ya kumtukuza Mungu, na kufarakanisha watu ni ibada ya Shetani. Padre kitima amefanya kazi ya Mungu, apongezwe, viongozi wengine wa kiroho waige mfano huu mzuri kutoka kwa Padre kitima
 
Hoja yako ni nn hujui upatanish ni sehemu ya kaz za kidini mpumbavu wewe sjui mijitu ya ccm ina akili gn ona kama hili
Acha kujitia upofu makusudi. Hivi ingekuwa Lipumba na Maalim Seif wameenda kushiriki vikao vya siri Msikiti wa Umar AlFarouq BAKWATA Kinondoni I ungechukulia poa?
 
Afu tunategemea kwa uwezo huu wa kufikiri na kuchambua mambo nchi hii itaendele ? Kweli Mkuu hapo hoja yako ni nini?
Tuletee ushahidi wa clip za Lissu akithibitisha hayo unayosema!

Lissu alikuwa anaongelea swala la kupatanishwa kati Yale na FAM
 
N
Kwanini wanapotesha, kwanini hakuna anayeweka uthibitisho wa video habari hii ya madai kuwa Tundu Lissu amethibitisha Padre Dkt. Charles Kitima kushiriki vikao vya siri vya CHADEMA?

Katika video ya mahojiano na Waandishi wa Habari hakuna mahali Lissu amemtaja Kitima lakini namna imeripotiwa ni kama viongozi wa dini hawapaswi kufanya upatanishi.

==

View attachment 3195838
Katika tukio lililotokea jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, amethibitisha hadharani kuwa Fr. Charles Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), alihudhuria vikao vya siri vya chama hicho vilivyofanyika katika ukumbi mdogo wa Macapuchino ulioko eneo la kanisa, Msimbazi Centre, jijini Dar es Salaam.

Mwanzoni mwa mwezi Desemba, taarifa za ndani zilisambaa zikidai kuwa Fr. Kitima, Kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki, alihusishwa moja kwa moja na vikao vya CHADEMA.

Taarifa hizo zilizua mijadala mitandaoni, huku baadhi ya wadau wakitilia shaka ukweli wake na wengine wakihoji nafasi ya kiongozi huyo wa kidini katika siasa za vyama.

Hata hivyo, jana Lissu amekiri waziwazi ushiriki huo, akiondoa shaka kuhusu madai hayo ambayo awali yalionekana kama uzushi.

Ukaribu wake na Fr. Kitima unatokana na ukweli kwamba wote wanatoka kijiji kimoja mkoani Singida. Ukaribu huu, kulingana na vyanzo vya karibu, umesababisha Fr. Kitima kuwa mmoja wa wapangaji wakuu wa mikakati ya kampeni za Lissu na hatua za kuipinga serikali.

Uthibitisho huu umetajwa kama "kuvuliwa nguo kwa kanisa," huku baadhi ya wadau wakidai kuwa hatua ya Lissu kufichua ushiriki wa Katibu wa TEC katika siasa za vyama imeweka wazi mgongano wa maadili unaohusiana na nafasi ya viongozi wa dini katika masuala ya kisiasa.

Uthibitisho huu umetajwa kama "kuvuliwa nguo kwa kanisa," huku baadhi ya wadau wakidai kuwa hatua ya Lissu kufichua ushiriki wa Katibu wa TEC katika siasa za vyama imeweka wazi mgongano wa maadili unaohusiana na nafasi ya viongozi wa dini katika masuala ya kisiasa.

Kanisa Katoliki linatakiwa kutoa tamko rasmi kufuatia kauli ya Lissu, ingawa mjadala mkubwa umeibuka mitandaoni, huku waumini na wadau wa siasa wanakosoa hatua hiyo kama kinyume na maadili ya kidini.

Tukio hili linaongeza mvutano kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika siasa za Tanzania.View attachment 3195839
Naomba kipande cha video ambacho Lissu anaonekana na anasikika akisema hayo ya kuwa Fr. Kitima Ph.D, ndiye aliyekuwepo wakati wa vikao kwa siku tatu.
 
Hoja yako ni nn hujui upatanish ni sehemu ya kaz za kidini mpumbavu wewe sjui mijitu ya ccm ina akili gn ona kama hili
Hoja yangu ni kwamba kwanini vyombo vya habari viiripoti habari hii kama uchonganishi kwa tabaka tawala na kiongozi huyu wa kidini ambaye hata kwenye mahojiano Lissu hakumtaja kwa jina?
 
N

Naomba kipande cha video ambacho Lissu anaonekana na anasikika akisema hayo ya kuwa Fr. Kitima Ph.D, ndiye aliyekuwepo wakati wa vikao kwa siku tatu.
Rudia kusoma nilichoandika kisha rudi hapa uulize swali lako mkuu inaonekana umepitisha macho tu
 
N

Naomba kipande cha video ambacho Lissu anaonekana na anasikika akisema hayo ya kuwa Fr. Kitima Ph.D, ndiye aliyekuwepo wakati wa vikao kwa siku tatu.
Hoja yangu ni kwamba kwanini vyombo vya habari viiripoti habari hii kama uchonganishi kwa tabaka tawala na kiongozi huyu wa kidini ambaye hata kwenye mahojiano Lissu hakumtaja kwa jina?
hata kama tundu lisu amemtaja kwa majina, Padre kitima hapaswi kuona aibu au kuona kwamba amefanya makosa bali anapaswa kujitokeza hadharani na kukiri kuhusika kwani kitendo alichofanya ni Kitendo kitakatifu, amefanya kazi ya kumtukuza Mungu.kupatanisha watu ni ibada ya kumtukuza Mungu, kufarakanisha watu ni ibada ya Shetani. endapo kama kweli alihusika kwenye suala hili la kupatanisha watu, atakuwa amefanya kazi ya Mungu
 
hata kama tundu lisu amemtaja kwa majina, Padre kitima hapaswi kuona kwamba amefanya makosa bali anapaswa kujitikeza hadharani na kukiri kuhusika kwani kitendo alichofanya ni Kitendo kitakatifu, amefanya kazi ya kumtukuza Mungu.kupatanisha watu ni ibada ya kumtukuza Mungu, kufarakanisha watu ni ibada ya Shetani
Exactly sio huu unafiki ambao baadhi ya vyombo vya habari vimeuripoti afu bila hata hiyo video ikiwa mengine aliyoongea wameweka video
 
Wengi hamjamuelewa Mtoa mada.

Mtoa mada , ni mfuasi wa LISSU.

Ila baada ya kuona Vyombo vya habari vinaandika habari ya LISSU kuthibitisha Et anapatanishwa na Padre Kitima.

Ndo hapo Mtoa mada anafikiria Kwa jicho la tatu kua Kuna Vita ya kimya kimya baina ya Dola na Dini , ndio maana vyombo vya habari vimeanza kushambulia Kanisa.
 
😂 mimi sio mkereketwa wa Lissu ila sipendi kuona vyombo vya habari vinaripoti tofauti na kilichozungumzwa, ni kama wanafitinisha hivi
 
Back
Top Bottom