Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ha ha ha ha ha ha


Kwa upande wangu me nadhani kama una expect ugeni ni vema basi ukaandaa chakula ambacho wageni watakula na kufurahia na sio kujibana bana na kujutia.

Lakini kama ugeni ulikuwa ni wa ghafla ni vema ukawachukua wageni mkaenda mgahawani mkapiga menyu huko.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu kisa kakaribishwa kaambiwa jiskie uko nyumbani. Kakaanga mayai tisa toka kwny tray. [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Uroho mwingine bwana...... Sasa mayai 9 kweli jamani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ila vijana ambao wanatokea maisha ya kipato cha chini wajifunze kutoa uroho kipindi cha kujitegemea. Kama kwenu walikuwa hawapiki vyakula unavyopenda kama kuku, chips, mayai, samaki, nyama, sijui maziwa etc. Then utakapo anaza jitegemea hebu anza kwanza kuishi pekee yako kwa muda ukiwa unajinunulia hizo vitu pekee yako na kuvila hadi uvizoee. Ukienda kwa mtu au ugenini hata ukikaribishwa hautaona ajabu kuviona hivyo vitu..... Na havitakushawishi sana....

Ila unakuta mtu maisha yake yote amezoea kula kuku kibawa au shingo, hajawahi kujiachia kula hata nusu kuku pekee yake..... Au kuku mzima.....

Kaa mwenyewe amua tu kwa kutenga bajeti, nunua hivi vitu na uvile kwa hamu hadi usaze. Utaona namna utavizoea na kuona hali ya kuvikifu mtu akikukaribisha kwake na kukupatia....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha nimemkumbuka jamaa fulani family friend wa dingi yangu mdogo ilikuwa kama kuna ka event hapo kwa mdingi mdogo basi yeye anawaambia kabisa kila mtu apakue ale ashibe yeye ni wamwisho kula maana anapita na kila kitu yani kiujumla jamaa alikuwa hapakui kwenye sahani bali kama ni hot pot anakula humo humo.

Halafu wala hakuwa na aibu na ni mtu mzima na mke wake yupo hapo hahaha.
 
Aisee watu wanaopakua milima huwa siwaelewi hata kidogo...... Yaani why mtu unachota chakula as if hautakuja kula tena.....?!

Ulafi ni tabia mbaya sana na unapokuwa mlafi unaonekana wazi wewe ni mbinafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingine aliniuzi sana alikunywa chupa nzima ya chai ya maziwa na mkate nzima mdogo kisa hajawahi kula mkate wa karanga eti ni mtamu sana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kuna watu hadi ukitoka nae hapo unajiapiza huyu mbwa sitakwenda nae popote siku nyingine. Mtu anakula as if amekuja duniani kula tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nilifundishwa na wazazi ukienda kwa mtu bila ya ahadi na ukakuta wanakula usile maana katika bajeti hujuwepo kabisa na ukiangalia ni sawa,mpaka leo hili nimeliweka kichwani.
Muda mwingine inakuwa ngumu sababu unapata picha gani umekwenda kwa watu wao wote wanakula halafu wewe umeketi tu hauli.

Hapo unachofanya unashika sahani unapakuwa kidogo sana cha kuzuga japo vijiko vitatu au tonge tatu. Then unakula taratibu sana ili uende sambamba na wenyeji wako. Baada ya hapo unatulia unaenda kunawa unaendelea na ratiba zingine.

Si kila familia watakuelewa mgeni ukija halafu usile. Kwao inawajengea picha mbaya kuwa wao ni wachoyo au sio wakarimu na pia wewe kuwa wakija kwako pia wasile.

Mfano mimi ukija kwangu kula ni lazima ule. Usije ukaja umekula, utatapika ule tena, kula ni lazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23] mkuu umeona useme ukweli eeeh
 
Usiombee ikukute mkuu
 
Kuna baadhi ya watu bado haiwasaidii.
Bado wanaulimbukeni wa chakula.
Yaani akitoka akala au akapika kitu kizuri anaona siifa hadi anatangaza.
 
Hiyo namba 2 hata mimi imenikuta sana
 
Kama mambo yenyeww ndio kusimangana hivi, mimi ndio maana huwa siwezi kwenda kwa watu. Mimi kwangu nusu ya dona nikipika unga unabaki kidogo sana hata kuupika tena inakuwa ngumu na bakuli linajaa nyama au samaki. Nikitaka samaki naenda mwenyewe Kunduchi kununua ninaowataka. Sasa wewe unikaribishe nyumbani kwako na habari za ubwabwa upawa mbili na kamchuzi na kakipande ka kasamaki, si bora nibaki kwangu tu. Huwa ni bora nisile kabisa, kuliko kuichokoza njaa kwa kichakula cha masimango.

Wasukuma Tunajuana
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwenye kula unaweza ukajisahau jamani! Mpaka ukishtuka ushatia aibu tayari ,[emoji1]
 
Kula mwenyewe raha sana. Unakula kwa style unayopenda.

Hizi table manners zikizidi huwa zinakera. Mfano wale wa hakuna kuongea wakati wa kula. Nyumbani kwangu ndo muda wa story maana kukaa pamoja tena ni muda wa kula kesho jioni.
 
Oya
dogo interview yako iliendaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…