Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kakupatia ulinunua? [emoji3][emoji3] Ukishacheza rafu unamuombe dua shemejio Mungu ambariki, kama ni Mimi naitikia tu sawa wala sitabasamu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan nimecheka. Halaf huyo mgeni hapo ana mandevu kidevu chote mpaka timbalendi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119] amechonga na O
 
Wakati wa likizo huu unapokea watoto wamekuja likizo. Asubuhi umezoea kuwakaangia watoto wako mayai manne lakini wenyewe umewafundisha kuwa ni lazima kila mtu apate.

Wanakuja watoto wageni wanamaliza mayai yote wanao wanabaki wanaangalia. Kama wangefundishwa wote wangegawana na wote wangepata hata kipande kidogo.
We nae kama unaona mgeni atakumalizien chakula si mjiwekee shea yenu jikoni aargh.
 
Sijui ni ulafi au Uzungu, wewe kama umepika wachache si shida ni yako? kwanini usiweke kwenye sahani na mkashea hasa kwenye upande wa mboga? Hivyo vipande vitatu ni vya gram ngapi kila kimoja? Chakula cha manung'uniko bhana mwisho mtu anigwe na mfupa kisa jicho la usuda la kuchukua samaki mmoja (tena kagawanywa vipande vitatu) mwenye gram 400.

Kwani haufahamu siku hizi chakula ni mboga, YAANI MBOGA INAKUWA KUBWA ZAIDI YA WALI/UGALI?
Hahahahah yani mtu analalamika wee, mie kwetu mboga ni nyama au samaki. Unakula tani yako awe mgeni au mwenyeji. Uchoyo kwetu mwiko
 
Unakaribishwa chakula kwenye familia, mabakuli makubwa ya chakula na mbogamboga yanawekwa katikati. Inakuja wakati kila mtu ajiwekee chakula anachopenda.

Mezani mpo nane. Wewe ni mtu wa tatu kujiwekea chakula, utamsikia shemeji leo umenipatia kweli, hawa samaki ndiyo ugonjwa wangu. Anachukua vipande vitatu pasi kufikiria watano wanaomsubiri watapata samaki.

Ustaarabu ni kuchukua chakula kidogo, subiri round ya kwanza iishe. Kama ulipenda sana samaki unaweza kujiongezea katika round ya pili kama watakuwa wamebaki. Wakati huo ndiyo unaweza kusema kama hakuna anaeongeza ninatongeza hawa samaki maana hiki ndiyo chakula ninachokipenda, leo shemeji umenipatia.

Kuna wengine anakula huku anashika smart phone yake mezani anaangalia messages. Jamani hao wanaokutumia hawawezi kusubiri mpaka umalize kula na wenzako? Kama una ujumbe wa muhimu sana deal la mahela unaweza kuwataarifu wenyeji wako kuwa kuna ujumbe ninautegemea lakini ni ustaarabu kuachana na simu wakati mko mezani.
Table Manners,kuna watu ni washenzi wanaongea na chakula mdomoni ,haya mambo lazima kufundishwa ukiwa na 4 yrs ,
 
My dear Sky Eclat

Ndio maana siku zote wazazi huwa wanashauriwa kuwa wanakula meza moja na watoto wao ili wawafundishe TABLE MANNERS ikiwamo kuwafikiria wengine na hata namna ya kutafuna chakula.

Inawezekana hao wageni ndio wale waliopelekwa boarding wakiwa bado wadogo sana (darasa la tatu) wakakosa muda wa kufundishwa tabia njema na wazazi/walezi wao.
Sorry hata hapa nipo nakula restaurant lakn nachezea cm
 
[emoji3][emoji3][emoji3] eti shemeji apo umenipatia hahahaa unautani nawatu! Halafu ukute hawajaoa !
Hii ni kweli kabisa mkuu, miaka kadhaa nyuma nilimkaribisha jamaa tuko naye kazini kwa lunch maana tulitoka wote vijijini... Wife alipika roast nyama ya nguvu lakini ni mboga ya kula mpaka jioni... Aisee jamaa alitukomesha huku akimwaga sifa kwa wife, alikomba nyama karibia pori liishe na wala haoni aibu.
 
Hii ni kweli kabisa mkuu, miaka kadhaa nyuma nilimkaribisha jamaa tuko naye kazini kwa lunch maana tulitoka wote vijijini... Wife alipika roast nyama ya nguvu lakini ni mboga ya kula mpaka jioni... Aisee jamaa alitukomesha huku akimwaga sifa kwa wife, alikomba nyama karibia pori liishe na wala haoni aibu.
Haaa haaa wapo wengi, unajua watu wanashindwa kuelewa mjini hakuna mashamba ukiendekeza kula bila utaratibu utashindwa hata kununua hata kijiko.
 
Hayo ndio matokeo chanya ya watu wa mikoani.
Siku nyingine siku nyingine anaondoka na chupa la chai.
 
Hivi watu wanawezaje kufanya hivyo ugenini au ndo ucheshi na uchangamfu? sitasahau siku 1 nilipo karibishwa chakula mezan tuko watu 5 nilipakua chakula kidogo kuliko wenyeji na nikadanganya kuwa nimeshakula huko nilipo toka.
Baada ya dakika 10 akaingia mtt wao katoka shule akakuta chakula kimeisha alilia sana hata alipo ambiwa asubir apikiwe chake bado aliendelea kulia huku ananiangalia kwakweli nilijiskia vbaya sana, baba wa mtoto akamtandika mtoto wake kwa kosa la kutokua na adabu na Mimi nikiwepo ndo nikaendelea kukosa amani kabisa nikajiona Mimi ndo chanzo Cha yote.
Hadi leo hii nikiwa ugenini ukifika mda wa kula ndo muda ninao uchukia zaidi na ninaweza kukataa kula kabisa kama ikiwa tu ni sehem nilienda kusalimia na kupita
 
Tungeiga tu utaratibu wa wazungu , nadhan wapo straight sana , mgeni hatarajii kukirimiwa na chakula anapomtembelea mwenyeji wake ,

Hii ya kulazimisha kulishana ilhali Hali hairuhusu ndio huanzisha masimango kwa jina la table manners.
Mbona wazungu wanakaribishana chakula.
 
Mmenikumbusha mbali kuna wageni wawili walikuja nyumbani sasa tuna utaratibu wa kupakua chakula cha wote mezani wacha wale ugali wote wa watu sita tena usiku ikabidi tuanze kupika mwingine tena
Hii iliwahi nitokea
Niliweka ugali kwenye hotpot na mboga kwenye hotpot

Jamaa walikuwa wawili wakanawa wakasogeza hotpots zote wakapiga msosi nafika na visahani vyangu tukate ugali,
Shughuli imeisha
 
+1
Mimi sili kabisa kwa watu , no matter what. Sana sana nitakunywa Maji,
Unakaribishwa chakula hapo hapo unakuwa under surveillance jinsi gani utakula, hapana
Bora tu umejichagulia utaratibu japo pia utasemwa jamaa kaona chakula chetu cha hovyo nini?
 
Back
Top Bottom