Kuna wakati wabongo walitaka kutuaminisha na hii kauli "hata hao wazungu wana uchawi wao"

Kuna wakati wabongo walitaka kutuaminisha na hii kauli "hata hao wazungu wana uchawi wao"

Aliwahi kusema marehemu Mengi

pesa haiwezi kumilikiwa na mtu mjinga
Hakika.

Watu wanajiuliza kwanini wachaga, wayahudi, wazungu, ni watu wenye mali nyingi

Sio kwa sababu eti ni jamii teule, hapana ni jamii zilizoamua kuwekeza fikra katika kutatua fumbo la kumiliki na kumeneji pesa kwa sasaa na kwa baaadae.
min -me
mcTobby

Ila unakuta mtu anakuambia eti wanatambikia makuburi mara iluuminati😁😁
 
Hakika.

Watu wanajiuliza kwanini wachaga, wayahudi, wazungu, ni watu wenye mali nyingi

Sio kwa sababu eti ni jamii teule, hapana ni jamii zilizoamua kuwekeza fikra katika kutatua fumbo la kumiliki na kumeneji pesa kwa sasaa na kwa baaadae.
min -me
mcTobby

Ila unakuta mtu anakuambia eti wanatambikia makuburi mara iluuminati😁😁
Mbona mimi natambika ila bado naganga njaa tu😅
 
Acha uvivu, acha ushirikina.

Mbinu zinazoonekana na halisia ndio hutatua matatizo au changamoto.

Wekeza katika fikra halisia na sio za kufikirika.

Biashara ni mtaji sio kuchinja kuku.

Kupanda cheo ni bidii au kupendelewa sio kuchinja mbuzi.

Hakuna cha nyota kuchukuliwa wala sijui kufifia, kama umezaliwa kapuku au fikra finyu tegemea kufa kapuku labda uende outside of the box kuvunja matrix ilio kushikiria na sio kwenda kuchanjwa kwa mganga.

Mzungu kwenda mwezini ni jitihada zilizofanyika miongo na miongo ila wewe unataka ufuge majini ya pesa utajirike kama mkinga ndani ya miaka 2[emoji16]
We unaamini walienda kweli mwezini mkuu
 
Hakika

Its like this,

Mzungu aliamua kuwekeza katika kutatua changamoto katika mbinu za kushikika na halisia ila sisi hadi leo tunafanya vice versa.

Mzungu alifanya kujichallenge ikawa ndio jadi na utamaduni wake, yani akitengeneza panga baada ya miaka atattengeneza bunduki then bomu then so and so

So stori ya mzungu its about investing in his thoughts by employing tangible measures
Ubaya wa teknolojia ya kiafrika ni metaphysical- na kanuni zake hazijaandikwa popote. Kwa mfano, katika orodha ya mashujaa wa taifa kuna mama anaitwa Liti Kidanka. Huyu mama alikuwa anatoka mkoa wa Singida na aliongoza mapigano dhidi ya wakoloni kwa kutumia nyuki. Swali linaweza ni kanuni gani ambayo mtu anaweza kutumia nyuki kushambulia
 
Ndio limitations zake hizo
Sasa huwa unazichukuliaje hizo shuhuda za Joe dispenza ambazo zinakuwa zimevuka limitation? Ukiachana na Dispenza pia kuna hii case moja kubwa tu kuhusu nguvu ya akili katika uponyaji, ni case ya Dr. Albert mason ambaye aliweza kumtibu mtoto ugonjwa wa ngozi(congenital ichthyosis) ambao ulikosa tiba pamoja na kujaribu sana na kushindikana ila alienda kupona kwa tiba ya nguvu ya akili kupitia hyponosis na mgonjwa ngozi yake ikawa laini kama watu wengine.
 
Hakuna pesa za majini ni ujinga na blabla tu za kukosa maarifa , unasema pesa za majini na huna hizo pesa wewe si mwehu
Hapo unaonyesha jinsi unavyopinga na kuona ni ujinga kitu ambacho wewe hukiamini, jambo ambalo mwengine anaweza kuona wewe ndio hauna hayo maarifa katika hilo jambo.

Wewe haukubalini na uwepo wa majini hivyo ni wazi kutoweza kukubali chochote chenye kuhusishwa na majini, lakini kama ungefanya kauchunguzi pengine ungeweza kujua ukweli ni upi kwenye hiyo dhana ya uwepo wa pesa za majini.
 
Ninakubaliana na wewe 100%.
Ila ningependa kuweka mwanga kwenye hii ishu umeongelea.
Kufanikiwa ni siri kubwa sana. Kwa sababu ni vigumu sana kutokukata tamaa pale unapofeli zaidi ya mara moja...inahitaji imani ya hali ya juu, au ikiwezekana hata uchiz flan kuamin kufanya kitu ambacho kila mtu anajua hakiwezekani na mwisho wa siku pamoja na changamoto zote ukatoboa, mfano kwenda mwezini.
So kuna element ya imani, resilience , will power au tuseme psychological ina play part kubwa sana kwenye kufanikiwa sehem yoyote ile...
Sasa asilimia kubwa ya Waganga nk sio watu waliosoma na wengi wamerithishwa tu huo ujuzi bila kuuliza deeply maana halisi ya wanachokifanya na jinsi gani hasa vinafanya kazi ila ninataka kukuhakikishia kuwa asilimia 98 ya uganga na rituals wanazofanya ni psychological au mental manipulation zinazosaidia watu wajitume, waondoe uoga, wajaribu tena hata baada ya kufail na kujiamini.
Nitakupa mfano.
Mtu anaenda kwa mganga anapewa dawa ya kuoga aondoe mikosi , anaambiwa aoge asubuh na usiku.
Ukienda kwa psychologist atakuambia namna ya kufikia lengo lolote ni lazima uanze kuweka maisha yako in order,(Order vs Chaos) :-ni concept pana ila inaonyesha psychologically usipokua kwenye mpangilio hata physically hautakua kwenye mpangilio pia na kubadilisha kimoja kunaweza kubadilisha kingine eg ushaona chumba kiko rough, mambo hayaendi, nywele unachana unazivuruga bila kujua, ukiandika mwandiko unakua rough? au unagombana na mtu asubuhi na kila kitu kinaenda vibaya siku hiyo, unajiwangia soda, unajigonga mlangoni, simu inaisha charge muda una maongezi mazuri(downward spiral )
Sasa kurudi kwenye point ya mganga anayekupa masharti nje ya imani za superstitions, cha kwanza kinachofanyika ni kuweka maisha yako kwenye order...utaoga asubuh utaoga usiku(kitu ambacho usingefanya kama una depression au umejikatia tamaa). Baada ya dawa khisha hata kama haijafanya kitu supernatural imekubadilisha to the point utaanza kuona matokeo chanya kwenye maisha.
Ntakueleza kwanini viongozi wakubwa duniani, au hata wachawi wanasemekana wanakula nyama za watoto au kubaka watoto...mmoja nimeona ametolea mfano wa Epstein .
Hizi ritual wanazofanya hata kama kuna satanic elements ila ni psychological 98%.
To be the best you have to think you are the best, you have to be a wolf na wengine uwaone ni kondoo, inabidi ujione simba na kila mtu ni swala..
hiyo confidence hata kama ni delusional itakupush mbali sana na kila unayekutana naye atafeel huyu sio mtu wa kuchezea.. so hizo ritual ni kwa ajili ya power( wapate nguvu)
Emagine mtu yuko above moral principles anakula binadamu mwenzake kama kuku...if he walks like predator anajijua yeye ni predator kwli na yupo on top of food chain, top above humans as top most predator.

Imagine confidence, kiburi, kukosa utu na huruma huyo mtu aliyonayo ?
na hizo ndio traits za powerful people zipo hapo kwa sababu zinadetermine success kuliko kuwa mtu mwema.

So hizi rituals mbaya za kichawi na kiganga...ni dark ways to turn your psychology into bullets proof, killer na apex predator na once uko hvo chance ya kufanikiwa ni kubwa.

Ndio maana ninakubaliana na wewe 100%, watu wajitume na wapange ili wapate mafanikio...ila kama unaweza kutrick ubongo wako ukaamini zamu yako inakuja Mungu ni mpaji na ikakufanya usikate tamaa then usiache, kama kufeel the best in game inabidi ukae na watu waliokuzidi fanya hvyo(japo same thing mganga kwa elimu yake atakuambia unatumia nyota zao) ila vyovyote point ni kuwa na killer instinct, tremendous self belief, na 20% ya delusion.
Asante .
Masuala ya waganga kuna mambo mengi sana mkuu ambayo hata yanapoelezwa hapa huwa yanaonekana ni story za kubuni, mara zote mnapojaribu kuhusisha haya mambo na saikolojia huwa mnaishia kuelezea kati ya mtu na matokea ambayo yenye kutarajiwa kwa mtu husika mwenyewe. Ila kuna wakati mtu anaweza kwenda kwa mganga akataka lifanyike jambo na athari za matokeo ya hilo jambo zinatarajiwa kuonekana kwa mtu mwengine au katika jambo fulani, mambo kama haya huwa sioni ni kwa vp napo saikolojia inafanyaje kazi?
 
Mtazamo wa imani hizi unaweza kufelisha na kufanya watu wazidi kubaki gizani zaidi , tembelea tu vijiji vya Tanzania vile vyenye imani kali za ushirikina utaleta mrejesho.
Nachoelewa mimi sehemu kama hizo shida ni ujinga na hausababishwi kwa kuwa wanaamini uchawi kwa sababu ujinga ni ujinga tu hata kama hakuna imani za dini wala uchawi.
 
Masuala ya waganga kuna mambo mengi sana mkuu ambayo hata yanapoelezwa hapa huwa yanaonekana ni story za kubuni, mara zote mnapojaribu kuhusisha haya mambo na saikolojia huwa mnaishia kuelezea kati ya mtu na matokea ambayo yenye kutarajiwa kwa mtu husika mwenyewe. Ila kuna wakati mtu anaweza kwenda kwa mganga akataka lifanyike jambo na athari za matokeo ya hilo jambo zinatarajiwa kuonekana kwa mtu mwengine au katika jambo fulani, mambo kama haya huwa sioni ni kwa vp napo saikolojia inafanyaje kazi?
jamaa kaandika too deep usimpinge anajua sana
 
Back
Top Bottom