Kuna wakati wabongo walitaka kutuaminisha na hii kauli "hata hao wazungu wana uchawi wao"

Aliwahi kusema marehemu Mengi

pesa haiwezi kumilikiwa na mtu mjinga
Hakika.

Watu wanajiuliza kwanini wachaga, wayahudi, wazungu, ni watu wenye mali nyingi

Sio kwa sababu eti ni jamii teule, hapana ni jamii zilizoamua kuwekeza fikra katika kutatua fumbo la kumiliki na kumeneji pesa kwa sasaa na kwa baaadae.
min -me
mcTobby

Ila unakuta mtu anakuambia eti wanatambikia makuburi mara iluuminati😁😁
 
Mbona mimi natambika ila bado naganga njaa tu😅
 
We unaamini walienda kweli mwezini mkuu
 
Ubaya wa teknolojia ya kiafrika ni metaphysical- na kanuni zake hazijaandikwa popote. Kwa mfano, katika orodha ya mashujaa wa taifa kuna mama anaitwa Liti Kidanka. Huyu mama alikuwa anatoka mkoa wa Singida na aliongoza mapigano dhidi ya wakoloni kwa kutumia nyuki. Swali linaweza ni kanuni gani ambayo mtu anaweza kutumia nyuki kushambulia
 
Ndio limitations zake hizo
Sasa huwa unazichukuliaje hizo shuhuda za Joe dispenza ambazo zinakuwa zimevuka limitation? Ukiachana na Dispenza pia kuna hii case moja kubwa tu kuhusu nguvu ya akili katika uponyaji, ni case ya Dr. Albert mason ambaye aliweza kumtibu mtoto ugonjwa wa ngozi(congenital ichthyosis) ambao ulikosa tiba pamoja na kujaribu sana na kushindikana ila alienda kupona kwa tiba ya nguvu ya akili kupitia hyponosis na mgonjwa ngozi yake ikawa laini kama watu wengine.
 
Hakuna pesa za majini ni ujinga na blabla tu za kukosa maarifa , unasema pesa za majini na huna hizo pesa wewe si mwehu
Hapo unaonyesha jinsi unavyopinga na kuona ni ujinga kitu ambacho wewe hukiamini, jambo ambalo mwengine anaweza kuona wewe ndio hauna hayo maarifa katika hilo jambo.

Wewe haukubalini na uwepo wa majini hivyo ni wazi kutoweza kukubali chochote chenye kuhusishwa na majini, lakini kama ungefanya kauchunguzi pengine ungeweza kujua ukweli ni upi kwenye hiyo dhana ya uwepo wa pesa za majini.
 
Masuala ya waganga kuna mambo mengi sana mkuu ambayo hata yanapoelezwa hapa huwa yanaonekana ni story za kubuni, mara zote mnapojaribu kuhusisha haya mambo na saikolojia huwa mnaishia kuelezea kati ya mtu na matokea ambayo yenye kutarajiwa kwa mtu husika mwenyewe. Ila kuna wakati mtu anaweza kwenda kwa mganga akataka lifanyike jambo na athari za matokeo ya hilo jambo zinatarajiwa kuonekana kwa mtu mwengine au katika jambo fulani, mambo kama haya huwa sioni ni kwa vp napo saikolojia inafanyaje kazi?
 
Mtazamo wa imani hizi unaweza kufelisha na kufanya watu wazidi kubaki gizani zaidi , tembelea tu vijiji vya Tanzania vile vyenye imani kali za ushirikina utaleta mrejesho.
Nachoelewa mimi sehemu kama hizo shida ni ujinga na hausababishwi kwa kuwa wanaamini uchawi kwa sababu ujinga ni ujinga tu hata kama hakuna imani za dini wala uchawi.
 
jamaa kaandika too deep usimpinge anajua sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…