Kuna wanaume humu wapo kuvamia members wapya wanaodhani ni Wasichana

Kuna wanaume humu wapo kuvamia members wapya wanaodhani ni Wasichana

We jamaa mwandiko wako huwa haubadiliki...

JF ni kijiwe nongwa kuna pia IDs za kike lakini kimsingi ni njemba zinazotafuta fursa za kupiga mpunga...
 
Ukishazungumzia Social media , tambua uko ulimwengu wa Binadamu, uliumbwa na wao na ukakuzwa na wao. Kama vipi endelea kula mitongozo tu [emoji23][emoji23]
 
Sio JF tu....nadhani maisha yanabadilika kwa kasi...

Wanaume wamekuwa wa hovyo kabisa....hata Whatsapp siku hizi mwanaume anakutext kisha anakuambia nilikuwa nakusalimia...

Enzi zetu tunapiga simu ukiwa na jambo la muhimu. Mwanaume hauwezi ukanitumia text kisha unaniambia tu kirahisi nilikuwa nakusalimia.
😂si umeona mambo kama hayo sasa Mkuu,wanaume tunatakiwa kuwa kama wanajeshi ukikutana na muuni unampa salamu kikakamavu
 
mleta mada kazungumza kitu muhimu sana,kuna wakati nilibadili ID na kujiita "Misfortune" kwa sababu zangu nazozijua,kuna jamaa si likaja DM nimeniandikia "Mambo" ikabidi nilitukane nibadili na jina tena
Nimecheka sana aisee. Sasa kosa la hilo jamaa ni nini wakati mwenyewe ulijiita Miss Fortune [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom